Katika Mkutano wake Mkubwa wa hadhara wa Morogoro Mjini leo hii , ambao bila shaka umevunja rekodi ya Mahudhurio , Pamoja na Mambo mengine Tundu Lissu anahoji anayebandika mabango nchi nzima yakiwa na picha yake na ya watu wengine kwamba eti wamepatanishwa , amehojiwa kama wamepatanishwa , wamepatanishwa na nani ?
Anadai kwamba hizo ni propaganda za kichovu , na kwamba anawezaje kupatanishwa huku kukiwa na watu waliouawa , kutekwa na kuumizwa na hatima yao wala habari zao hadi leo hazijulikani ?
Akiongea kwa uchungu , Lissu anadai yeye mwenyewe alitandikwa risasi na hadi leo hakuna yeyote aliyekamatwa , anawezaje kupatanishwa na watu wa aina hiyo , anadai sasa hivi anaitwa CHIBA kutokana na majeraha ya wauaji wake (kwa wasiolewa chiba ni lugha ya mjini ikimaanisha mlemavu wa mguu) ,
amezungumzia kupotezwa kwa watu wengi sana akiwemo Ben Saanane , ambao hawajulikani walipo hadi leo , huku wenye madaraka au vyombo vya dola vikinyamaza , anasema katika hali hii anawezaje kupatanishwa na waliokuwa madarakani unyama huu ukitendwa ? na kwamba ambaye hayupo miongoni mwa watenda unyama huo ni mmoja tu , lakini wengine wote bado wapo , hapa unapanishwaje ?
Lissu anadai Arusha ndio mkoa unaoongoza kwa Mabango ya uongo yaliyopachikwa upatanishi , huku sisi wengine tukidhani lengo lao ni kudanganya watalii ili waone nchi sasa iko shwari.