Moshi: Meya Juma Raibu ang'olewa kwa kupigiwa kura za kutokuwa na imani naye

Moshi: Meya Juma Raibu ang'olewa kwa kupigiwa kura za kutokuwa na imani naye

Huyo Meya ni mzembe na hajui kusimama ktk mstari wa sheria, ametolewa labda ktk tuhuma zingine na sio ushoga, na km ushoga kweli ndo tuhuma iliyomtoa, basi sioni Elimu, upeo na ufahamu wake ktk kupambanua na kuchanganua mambo mbali mbali.

Mbna suala dogo hivi kashindwa kuli solve, au kashinikizwa na mamlaka ya juu zaidi kujitoa ktk nafasi hiyo, ili kuisafisha na kuiosha taasisi hiyo,

Ila hii nchi bhana, ina shangaza sana, badala ya kushughurika na mambo ya msingi kwa maslahi ya umma, wao wako buzzy na suala binafsi la mtu khaaaah. Huku haijui isimamie lipi na iache lipi,

Suala la ushoga kwa Tanzania iko wazi ni ruksaa, hata ktk sheria ipo inayolinda hilo, sasa serikali inataka kufurahisha umma kwa kukataa ushoga kisingizio eti tamaduni na desturi, utadhani ndo jambo la maana sana, khaaah.

Ifike hatua iwekwe clearly km ushoga n ruksa au ni jinai, ili kila mtu aelewe, na km ruksa bas wahusika waachwe huru kufanya mambo yao binafsi wazi, na km jinai bas kuwepo na adhabu au muongozo sahihi juu ya wahanga hao na ufuatwe kulingana na taratibu husika, kwan itapunguza sintofahamu na mikanganyilo isiyo na ulazima.

Poleeeeeh Meya ila usikate tamaa, simamia unachokiamini usiyumbishwe na lolote, wee n wee na utabaki kuwa wee.
 
Watoto wa kike walivyo pisi kali hivi, janaume zima linakuwa shoga.

Mambo ya kipumbavu sana.

Hongera sana madiwani
FB_IMG_1649677160035.jpg
Screenshot_20220411-145621.jpg
 
Huyu Meya ni Muda sana Amekuwa akisemwa na wananchi wa moshi kwa tuhuma mbalimbali. Wengi walisema hafiki mbali na kweli imetimia
 
Subirini baba wa mashoga(US) ajue mmetema mtu wao, mtanyimwa misaada yote😂
 
"Kushiliki sherehe za watu wa jinsia moja"

Hapo kuna Mawili Mkuu Kula au Kuliwa
 
Kwanza naomba niseme kwamba sijalijua kwa undani sakata la huyo Meya, ila nitatafuta muda nilipitie kwa undani kidogo, kwa hiyo kwangu si muda muafaka kutoa mawazo kwamba usahihi uko vipi

Lakini kwa sasa nataka nizungumzie kwa ujumla kuhusu jambo hili. Binafsi nimekuwa nina mtazamo tofauti na wengi wa wanaochangia mada kuhusu mashoga na ushoga. Nimeyatofautisha kwa makusudi maneno hayo mawili kwa kufahamu kwamba mashoga ni watu, na ushoga ni tabia za watu.

Kumekuwapo na mtazamo kwamba mtu aliye na ukaribu au anayetaka kuwa na ukaribu na kundi fulani, mfano mashoga, basi moja kwa moja naye anajihusisha na tabia za kundi hilo, yaani ushoga! Jambo hilo mimi huwa nalipinga, maana kama hakuna ushahidi wa dhahiri, mtu anawezaje kufahamu dhamira ya huyo aliyejiweka karibu na mashoga?

Yaani akitokea mwanaharakati wa kuwasaidia watumiaji wa madawa ya kulevya, na akatumia mbinu ya kuwakusanya na kuwa karibu nao ili kuwaelimisha taratibu namna ya kuachana na drugs, eti naye tunamuita mtumiaji au mfanyabiashara wa madawa ya kulevya! Vivyo hivyo mtu akiwa karibu na mashoga, bila hata kufanya uchunguzi kuhusu dhamira yake, eti naye tunamuita shoga!

Tutawakatisha tamaa wanaharakati wenye lengo zuri la kurekebisha tabia za vijana wetu. Hata maandiko yanasema Yesu alisema mwenyewe kwamba alikuja kwa ajili ya wenye dhambi, akala na kushinda pamoja na waliochukuliwa kama wadhambi, mfano yule mtoza ushuru na yule mwanamke kahaba. Baadhi ya Wayahudi walihoji hivi hivi kama tunavyohoji, kwamba inakuwaje fulani ana ukaribu na wale!

Kwa ufupi nilitaka tuwe tunatumia muda wetu kujiridhisha na dhamira za watu kabla hatujawapa majina mabaya

NB: Nimesema post hii haihusiani moja kwa moja na huyo Meya, ipo katika ujumla wake, labda hadi nitakapopata muda wa kufuatilia sakata lake
 
Kura 18 zimemkataa.

Alikuwa na kashfa ya kushiriki birthday ya shoga mmoja hapo Moshi.

Ni kashfa iliyotrend sana kwenye vyombo mbalimbali vya habari kama magazeti.

Nafikiri ndio hiyo imemng'oa labda kama kuna sababu nyingine tutajua

Kapigiwa kura Leo, 18 zimemkataa na 10 zimemkubali.

=========================
Meya wa Moshi ang'olewa, ni yule aliyehudhulia sherehe ya mashoga

Bazara la Madiwani Manispaa ya Moshi Mjini, Mkoani Kilimanjaro, leo Jumatatu Aprili 11, 2022 limemng’oa Meya wa Manispaa hiyo, Juma Raibu, kwa tuhuma mbalimbali zilizokuwa zikimkabili ikiwemo kuhudhuria sherehe ya mashoga na kuwaahidi ushirikiano.

Pia soma
Nae alikuwa kiherehere sana acha apumzike kama Ndugai
 
Kwanza naomba niseme kwamba sijalijua kwa undani sakata la huyo Meya, ila nitatafuta muda nilipitie kwa undani kidogo, kwa hiyo kwangu si muda muafaka kutoa mawazo kwamba usahihi uko vipi

Lakini kwa sasa nataka nizungumzie kwa ujumla kuhusu jambo hili. Binafsi nimekuwa nina mtazamo tofauti na wengi wa wanaochangia mada kuhusu mashoga na ushoga. Nimeyatofautisha kwa makusudi maneno hayo mawili kwa kufahamu kwamba mashoga ni watu, na ushoga ni tabia za watu.

Kumekuwapo na mtazamo kwamba mtu aliye na ukaribu au anayetaka kuwa na ukaribu na kundi fulani, mfano mashoga, basi moja kwa moja naye anajihusisha na tabia za kundi hilo, yaani ushoga! Jambo hilo mimi huwa nalipinga, maana kama hakuna ushahidi wa dhahiri, mtu anawezaje kufahamu dhamira ya huyo aliyejiweka karibu na mashoga?

Yaani akitokea mwanaharakati wa kuwasaidia watumiaji wa madawa ya kulevya, na akatumia mbinu ya kuwakusanya na kuwa karibu nao ili kuwaelimisha taratibu namna ya kuachana na drugs, eti naye tunamuita mtumiaji au mfanyabiashara wa madawa ya kulevya! Vivyo hivyo mtu akiwa karibu na mashoga, bila hata kufanya uchunguzi kuhusu dhamira yake, eti naye tunamuita shoga!

Tutawakatisha tamaa wanaharakati wenye lengo zuri la kurekebisha tabia za vijana wetu. Hata maandiko yanasema Yesu alisema mwenyewe kwamba alikuja kwa ajili ya wenye dhambi, akala na kushinda pamoja na waliochukuliwa kama wadhambi, mfano yule mtoza ushuru na yule mwanamke kahaba. Baadhi ya Wayahudi walihoji hivi hivi kama tunavyohoji, kwamba inakuwaje fulani ana ukaribu na wale!

Kwa ufupi nilitaka tuwe tunatumia muda wetu kujiridhisha na dhamira za watu kabla hatujawapa majina mabaya

NB: Nimesema post hii haihusiani moja kwa moja na huyo Meya, ipo katika ujumla wake, labda hadi nitakapopata muda wa kufuatilia sakata lake
Maelezo yaliyojaa ukweli na uhakika.
 
Back
Top Bottom