Uchaguzi 2020 Mpangilio wa Majina ya vyama kwenye Karatasi ya kupigia kura ulizingatia nini?

Uchaguzi 2020 Mpangilio wa Majina ya vyama kwenye Karatasi ya kupigia kura ulizingatia nini?


Nimeona Mfano wa karatasi ya kupigia kura za Urais inayosambaa mitandaoni na ambayo inadaiwa kutolewa na Tume ya Uchaguzi (NEC).

Nina swali dogo tu ambalo naomba nijibiwe. Huu mpangilio wa Majina ya vyama uliowekwa kwa namba ulitokana na vigezo gani, yaani ni kigezo gani kilizingatiwa ili huyu awe namba 1 na yule awe namba 5 ama awe namba 8?

Nitasema Kweli Daima Fitna kwangu Mwiko .

Unajua mkuu ili document iwe halali ni lazima iwe na sahihi, na kawaida sahihi huwa inawekwa mwishoni kabisa, hivyo basi tarehe 28/10 kinachokwenda kuhalalisha zoezi ni utiaji sahihi kwenye hiyo karatasi!
Kumbuka kuweka sahihi yako vyema...
 
Hapo wamerahisisha kazi ndugu zangu . Ww ukifika chukua karatasi yako ifungue usihangaike sana pepesa macho mwisho kabisa wa karatasi yako yaani angalia kwa umakini picha zilizo za mwisho chini ya karatasi yako ujue ni Yeye basi cha kufanya piga tiki yako hakikisha tiki yako isivuke kile kisanduku husika . Hapo ondoka nenda umbali wa mita 100 ama 200m subiria kushangilia
 
Hiyo Ballot paper jinsi ilivyo:

1. Itawachosha wapiga kura kutafuta jina la Lissu, maana watu wana tabia ya kuscan vitu top- bottom

2. Kutakuwa na confusion kati ya CHADEMA na CHAUMA, maana CHAUMA inaanza kutokea kabla ya CHADEMA

3. Kwenye column za majina wameweka majina ya Wagombea wenza kwanza kabla ya mgombea urais, hii itawaconfuse wale wasiotake time kuscan paper nzima. Kwa upande wa CCM itakuwa ni rahisi kumtambua mama Samia kuwa ndiye mwenza wa Magufuli, ila kwa wale wanaomjua Lissu tu kabla ya Salum Mwalimu wanaweza kushindwa kumlink Salum na Lissu. Ilitakiwa majina ya wagombea urais yawe Column ya kwanza na wagombea wenza Column ya pili

4. Kwa mpiga kura process ya utafutaji mtu wa kumpigia kwenye hiyo karatasi, iwapo watu wasipojua in advance mtu wamtakaye alipo, inaweza kuchukua muda mrefu kwa mpiga kura mmoja mmoja kukaa ndani ya kile chumba cha kupigia kura . Kwa hiyo hizo ballot paper zilivyotengenezwa zitapelekea muda wa kupiga kura uishe kabla ya watu wengi hawajapiga.

Hii ni advantage kwa CCM kama watahamasisha watu wao wapige mapema, yaani watakuwa mbele kwenye queue na kumaximize time ya upigaji Yaani kama ikichukua sekunde 2 kwa mpiga kura wa CCM kuweka tiki kwenye jina la JPM, itamchukua sekunde si chini ya 8 kwa mpiga kura wa Lissu kusearch jina la Lissu(kama hajui lilipo). Hii itapelekea wapiga kura wengi wa CCM kufanya yao huku wapiga kura wa CHADEMA wakiwa nyuma huko kwenye queue na matokeo yake muda umeisha halafu wamepiga kura kiduchu.

Solution ya hii ni kuelimisha wapiga kura, sasa sijajua kama muda wa kuelimisha wapiga kura nchi nzima kwa sasa ni wa kutosha maana nchi ni kubwa sana hii, na watu wengi huenda ujumbe ukachelewa kuwafikia

Lakini kuneutralize hilo ni kuwahi kwenda kupiga kura ikitokea randomness ya kutosha kwenye queue za kupiga kura, basi advantage hiyo ya juu hapo haitokuwepo sana, Ila wakiwahi wa CCM na kupiga mapema, Upinzani itakula kwao.

Kwa hiyo kiufupi solution ya hilo suala ni kama ifuatavyo:.

1. Elimu kwa wapiga kura, juu ya hiyo karatasi ilivyokaa

2. Kutumia nembo ya chama ya vidole viwili kama search method, yaani wapiga kura waambiwe, ilinkumtafuta Lissu alipo tafuta nembo ya vidole viwili, hapo utaliona jina la Lissu

3. Kuhakikisha wapiga kura wa Lissu wanawahi vituoni ili kuwaondolea CCM advantage ya kupiga kura zao nyingi mapema

4. Kuanzia sasa kila mkutano atakaopiga Lissu hasa kwenye maeneo na mikoa yenye Literacy level ndogo awahimize wananchi kutafuta jina lake (asiwaambie liko mwisho, isije ikatokea liko katikati) kwa kutumia alama ya vidole vya nembo ya Chama cha Chadema, Kauli ya Lissu itasambaa kwa haraka, na pia wabunge na madiwani wa Chadema waelezwe kutoa elimu hii ya kutafuta mgombea kwa kutumia nembo ya chama kwenye mikutano yao ya kampeni!
 

Nimeona Mfano wa karatasi ya kupigia kura za Urais inayosambaa mitandaoni na ambayo inadaiwa kutolewa na Tume ya Uchaguzi (NEC).

Nina swali dogo tu ambalo naomba nijibiwe. Huu mpangilio wa Majina ya vyama uliowekwa kwa namba ulitokana na vigezo gani, yaani ni kigezo gani kilizingatiwa ili huyu awe namba 1 na yule awe namba 5 ama awe namba 8?

Nitasema Kweli Daima Fitna kwangu Mwiko .

veri jinias hapo ni kwamba ukipigia wa mwisho c tunachana karatasi halafu tunasema kura imeharibika. wagombea wa chama cha mwisho hawaonekani.... au tunaunguz upande wa chini tu.. kwa kifupi kuwa wa mwisho kutatengeneza loop hole nying za kupata visingizio
 
2015 walifata mpangilio Alphabetically.
Projection design/structure ya presidential ballot paper ilikuwa negotiated na kukubalika baina ya vyama vyote tangu 1995 kuwa logic ya kupanga majina ya vyama vya Siasa kwenye ballot paper iongozwe na mpangilio wa herufi
 
Nenda kwenye kisanduku cha mwisho

Maliza kazi Linda kura yako
 
Nina swali dogo tu ambalo naomba nijibiwe.
Ukinijibu swali hili na la kwako litakuwa limepata jibu.
Kama umeshawahi kupanda mishkaki kwenye boda boda, ni kigezo gani huwa unatumia huyu akae katikati na mwingine akae nyuma? Ni ukubwa wa umbo, ni yule anayelipa ndio anakaa nyuma, unazingatia jinsia au huwa mnakaa randomly?
 

Nimeona Mfano wa karatasi ya kupigia kura za Urais inayosambaa mitandaoni na ambayo inadaiwa kutolewa na Tume ya Uchaguzi (NEC).

Nina swali dogo tu ambalo naomba nijibiwe. Huu mpangilio wa Majina ya vyama uliowekwa kwa namba ulitokana na vigezo gani, yaani ni kigezo gani kilizingatiwa ili huyu awe namba 1 na yule awe namba 5 ama awe namba 8?

Nitasema Kweli Daima Fitna kwangu Mwiko .

Chadema huwa wananiburudisha sana, kwa kulalama 24/7. Unapokuwa na orodha ya vitu au watu lazima kuwe na first and last.

Anayedhani huu mpangilio una significance yoyote, asubiri matokeo aone kama performance ya kila chama itafanana na position yao kwenye huu mpangilio!
 
Back
Top Bottom