Msaidizi wangu wa ndani anagawa vitu vyangu kwa wanandoa

Kata mshahara akigawa kitu! Au anajitolea?

Mwambie anachoweza kugawa kwa watu hapo ndani ni papuchi yake tu.
 
KENZY
 
Ushauri wa maana kabisa ni kufungia vitu vyako....mi nishalala hadi na vitunguu uvunguni kisa huu ujinga.

Wakimaliza kula vitu vyako watamtafutia kazi kwingine, jipange.
 
Njia rahisi ni hivi; nunua mahitaji yako kwa jumla lakini ukifika nyumbani gawanya kidogo kidogo kwa makadirio ya siku kadhaa kadhaa mfano siku Tano au wiki, vingine fungia kabatini ufunguo kaa nao mwenyewe. Vikiisha unagawanya tena hadi atajifunza

Kuna baadhi ya watu Wana madhaifu ya hivo. Akiona vitu kwa wingi hafikirii kuwa mnunuaji amelenga kutonunua tena kwa muda mrefu badala yake atagawa tu kwakuwa anaona vitu vipo tu kwa wingi
 
Kumbe kila mwamba ana udhaifu wake!

Miss huwa nakuona mbabe flan amaizing sana hapa Jf kutokana na comments zako konki pamwe thread!

Leo suala dogo tu la kisaikolojia umeshindwa kulitanzua kweli!

Binadamu tunategemeana katika kuendesha maisha, mbona hapo inaonekana kama huyo house girl wewe ndiye unayemtegemea kuliko yeye anavyokutegemea?

Kama mnategemeana, kwa nini usimweleze wazi mipaka yake na majukumu yake pamoja na madhara ya kugawa vitu?

Nakushauri mkuu, usije ukamtegemea binadamu kupita kiasi, kuna leo na kesho bhana.

Tumia lugha ya kidiplomasia kumuongoza mfanyakazi wako lakini siyo kumuogopa.
 
Namuogopa asije akachukia akaondoka
Unampenda sio unamuogopa, mna bond ya muda mrefu ni faraja yako hata km anakosea kuna namna ya kumwambia unaempenda ili usimkwaze kwanza kabla hujamwambia hakikisha amekula akashiba halafu anza na story km 2/3 za mafunzo kuhusu kugawa vitu na madhara yake na kila moja mpe funzo na yeye mpe nafasi ya kuchangia usiwe mzungumzaji peke yako usimkaripie usifanye km amri mpe uhuru wa kuamua na kuchagua kutokana na maelekezo yako usifanye km una mlazimisha kufanya hivyo ndani ya muda mfupi ataacha tu, nakumbuka kuna sehemu nilitembelea nikakuta eti msichana wa kazi anachapwa fimbo yaan akikosea adhabu yake ni fimbo anatandikwa bakora mpaka anatokwa na alama malengelenge mwilini na haondoki maana akiangalia alipotoka na alipo bora alipo kuliko alipotoka kwa hio pamoja na mateso yote ila anajikuta tu anabakia hapo, sehemu nyingine pia niliwahi tembelea yule msichana haruhusiwi kuongea na mtu yoyote akionekana anaongea na mtu yoyote basi ni kipigo anashushiwa kipigo sio kawaida na boss wake eti kwanini unaongea na watu usiowajua, kwingine nilikuta msichana haruhusiwi kujenga ukaribu na watu wa nje si tukazoeana na mimi mwezi uliofuata nikakuta wamemfukuza wameleta msichana mwingine sababu nini eti anazoeana sana na watu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…