Msanii Mkubwa Bongo Fleva atabiriwa kifo na Wachungaji kutoka Kenya na Zimbambwe
Huyo nabii wa Kenya amenyooka kwenye maelezo yake hajaremba kama wa Zimbabwe naona bwana devil baada ya kumpa mali na umaarufu anataka kumnywa damu sasa
Steve Nyerere, Haji Manara na mimi natabiri ndiyo watakuwa wakusanyaji rambirambi
 
Huyo Mchungaji ni tapeli wa maneno kama KWELI kaona kifo atuambie Siku na saa ya hicho kifo .la SIVYO yeye na manyau nyau tofauti yao ni vilinge tu
 
Huwezi kukwepa kifo kwa maombi, waache ujinga huo
Au kama kuna watu wametoa hela ndefu kwa wachungaji hao ili wakamilishe mission zao
Yaani hata akifa kwa ajali watasema duu hata wale jamaa walitabiri

Hakuna unabii zama hizi bali ni ujambazi na wizi tu
Kuna watu wanataka wapige hela hapo tena wanaweza au anaweza kuwa mtu wa karibu au mke, mtalaka au hata ndugu wa karibu ambae anategemea wakifa watapata mirathi

Dunia ya sasa kila plan na utapeli tunasoma kwenye mitandao wala huhitaji kujiumiza kichwa kupata ideas
 
Yule jamaa aliyetabiri ajali ya ndege yuko wapi kwani amalize utata.
 
Mtumishi wa Mungu, Dr. Ian Ndlovu, ametabiri kifo cha mwanamziki nyota, kutoka nchi ya Afrika ya Mashariki, iliyokuwa na mpiganiaji uhuru maarufu wa Afrika ambaye sasa ni marehemu. Ingawa hakutaja moja kwa moja, wengi wanahisi anamaanisha Tanzania. Ndlovu alisema alipokea maono haya wakati wa maombi ya kufunga mwezi Januari na pia mara mbili mwezi Aprili. Amewataka waumini wake kumuombea mwimbaji huyo ili apate wokovu na ulinzi. Wengi wanaamini kuwa mwimbaji huyo nyota anayetajwa ni Diamond Platnumz. Dr. Ndlovu ameomba ujumbe huu umfikie mwimbaji husika moja kwa moja.

Dr. Ian Ndlovu alishawahi tabiri kifo cha Magufuli

View: https://youtu.be/5Sa2qL_q_sw?si=-sxDRHlxzhWX_F--
 
Atakuwa mwanachama mwenzake,wanachama wa freemason huwa wanaujua mwisho wa wenzao wanajua Fulani kashindwa masharti au hatoyaweza masharti kafika mwisho, kwa kikao kijacho lazima atolewe kafara atoke duniani akatumikie kuzimu.
Kama yule msanii aliyezikwa kinondoni yupo kuzimu kwa cheo cha alfan star jukumu lake ni kupanda roho ya uharibifu makanisani.
 
Yule mwenye mapete yenye maantena ya kuomba usaidizi wa nguvu toka kuzimu ili kuvuta watu alalae hovyo na wanawake maarufu ili kufifisha nyota zao ili yeye azidi kuwa juu na hao wanawake kuwa down kiroho na kiuchumi pana nabii mwingine wa uongo ndani ya afrika hii kamtabiri kwamba mkataba wake umefika mwisho.
Afanye toba awe salama.
 
Sijawahi ona kwenye Biblia toka nilipoanza kuisoma nikiwa mdogo hadi uzee huu Nabii anamtabiria mtu kifo.

Kufa kupo kwa kila mtu na hatujui saa wala siku ambayo tutakufa. Huyo nabii ni janja janja ili kama ikitokea msanii yoyote kafa ionekane alishatabiri japo pia anaweza kufa kwanza yeye kabla ya huyo msanii. Inasikitisha kwa kweli.
 
Mtumishi wa Mungu, Dr. Ian Ndlovu, ametabiri kifo cha mwanamziki nyota, kutoka nchi ya Afrika ya Mashariki, iliyokuwa na mpiganiaji uhuru maarufu wa Afrika ambaye sasa ni marehemu. Ingawa hakutaja moja kwa moja, wengi wanahisi anamaanisha Tanzania. Ndlovu alisema alipokea maono haya wakati wa maombi ya kufunga mwezi Januari na pia mara mbili mwezi Aprili. Amewataka waumini wake kumuombea mwimbaji huyo ili apate wokovu na ulinzi. Wengi wanaamini kuwa mwimbaji huyo nyota anayetajwa ni Diamond Platnumz. Dr. Ndlovu ameomba ujumbe huu umfikie mwimbaji husika moja kwa moja.

Dr. Ian Ndlovu alishawahi tabiri kifo cha Magufuli

View: https://youtu.be/5Sa2qL_q_sw?si=-sxDRHlxzhWX_F--

Utabiri huo unamtukazaje Mungu?
Kama ameona hilo linakuja, anataka sisi au huyo mwanamuziki afanye nini?
Kwanini asitabiri afya njema na maisha marefu zaidi kwa mhusika?
 
Back
Top Bottom