Mshahara umetoka, nyongeza ipo lakini lazima ucheke tu

Mshahara umetoka, nyongeza ipo lakini lazima ucheke tu

Hongereni watumishi, bado anaupiga mwingi?? 😀
 
Hivi Elfu 20/mwezi unaipunguzia nini? Wafanyakazi wa Tanzania hawana hitaji lisilo la lazima, mshahara wenyewe hata wiki 2 hautoshi na hilo ni kula, pango, umeme, nauli labda na vocha, sasa hapo anapunguza nini ?
Na ninyi acheni kulalama kuna wengine hata laki mbili hapati kwa mwezi na matumizi yote hayo yanamtegemea ningekupa mfano binafsi ila utaniita motivation speaker
 
Utumishi wa umma ni wito hiyo elfu 50 wengine haitoshi hata kulipia kingamuzi sijui mnalipaje bills zenu[emoji3064]
Ukiachana na wachache ambao ni wezi na wala rushwa waliobakia maisha ni magumu sana..
 
Katiba mpya itasimamia vema fedha za serikali ili wanasiasa wasijineemeshe pekee yao kama ilivyo Sasa!!

Mapato ya siasa yatapunguzwa na kuongezwa kwenye uweledi Ili kuleta tija ya maendeleo kwa Taifa letu na Sio Kama Sasa ambapo Mama Samiah na Mwigulu wanagawana hata fedha za mkopo wa mishahara ya watumishi ili watumishi wafie kwenye umaskini!


Wakuu msisahau mbinyo wa mishahara ni spinning ya vugu vugu la katiba mpya AMBALO limepamba Moto Hadi Sasa nchini! Msivunjike Moyo na kuacha KUIMBA WIMBO WETU huu hapa;-

"Rasimu ya Warioba irudi mezani SASA iwe KATIBA MPYA""!!
 
Na ninyi acheni kulalama kuna wengine hata laki mbili hapati kwa mwezi na matumizi yote hayo yanamtegemea ningekupa mfano binafsi ila utaniita motivation speaker

Mimi sijalalama popote, na ni kweli usemavyo Watanzania wengi wana maisha magumu sana ila Kiongozi wao kila siku safari na msululu wa watu kwa ndege ya kukodi na shopping, halafu badala ya kuwaambia watu ukweli anawadanganya na kuwapiga blah blah, pure evil!
 
Kuweni wavumilivu nchi ina Mambo mengi sio mishahara tu, Kuna madawa hospitalini,miundombinu na vingine vingi
 
Back
Top Bottom