Msichana mjasiriamali na mhitimu wa Uhasibu. Natafuta kazi naomba mnisaidie
Tuliza wenge utapata mtu atakusaidia hii jf ina watumiaji wengi sana, sasa wewe unataka leo leo au ?? just cool calm down
Katingishwa kidogo kafuta namba wakati wanaomweleza afute namba wamechukua namba na wana plan zao Binti hajui anataka nini wenge limemshika kila anapogusa anaona km kagusa Moto balada atulie tu mambo yanajiset yenyewe anakua na paparapupa
 
Habari wakuu,

Mimi ni msichana wa miaka 24 nimemaliza chuo kikuu mwaka huu kwa masomo ya Uhasibu na Biashara(bachelor in accounting and finance). Tangu nikiwa chuo nimekuwa nikifanya ujasiriamali wa kuuza vipodozi na nguo za kike had hivi juzi juzi nilipohitimu ila sasa kama mnavyojua ndugu zangu ujasiriamali ni mgumu ukizingatia hela ya ujasiriamali nilikuwa natoa katika hela ya kujikimu chuoni (boom).

Kwa sasa biashara hainiendei vizuri hivyo nimekuja kwenu wanajukwaa naomba mnishike mkono kupatiwa kazi yoyote iliyo ya halali ambayo haitanitweza utu wangu.

Nipo hapa hapa Dar es salaam

NB: nje ya masuala yangu ya ujasiriamali pia nina kipaji kutengeneza maudhui mitandaoni (content creator) na uanamitindo na urembo.

Pia kama kuna mtu ana namna anaweza kuniunganisha na masuala haya ya urembo na uanamitindo nitashukuru sana kwa kweli hali ya kukaa bila kuwa na ishu ya kuingiza pesa ya ziada inanipa deprression kubwa.

Yeyote atakaeguswa na ombi langu basi anicheki PM

Asante
Drop your number Pm kama upo tayari kufanya kazi kwa malipo kidogo kwa siku.
 
Kwa mujibu wa maelezo yako wewe tayari unakazi. Ukitumia hivyo ulivyonavyo, hautataka kuajiriwa bali kuajiri
 
TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI

Anahitajika RECEPTIONIST

VIGEZO
Awe jinsia ya kiume
Umri ( Asizidi Miaka 30)
Awe na elimu ya Certificate au Diploma course yoyote
Awe na good customer care
Awe mwaminifu
Awe anaweza kutekeleza majukumu yake kwa ufasaha

MAENEO YA KAZI
Mkoa wa Kigoma
(Kigoma mjini)

MAWASILIANO
0745966232
0679190103 (WhatsApp )

Asante
_________________________
Kwa mara ya kwanza naona Vijana wa kiume wanapewa upendeleo au nisema kipaombele kwenye kazi km hii yaan hapo kogezo uwe wa kiume Wanawake mmewafanya nini maboss?
 
Habari wakuu,

Mimi ni msichana wa miaka 24 nimemaliza chuo kikuu mwaka huu kwa masomo ya Uhasibu na Biashara(bachelor in accounting and finance). Tangu nikiwa chuo nimekuwa nikifanya ujasiriamali wa kuuza vipodozi na nguo za kike had hivi juzi juzi nilipohitimu ila sasa kama mnavyojua ndugu zangu ujasiriamali ni mgumu ukizingatia hela ya ujasiriamali nilikuwa natoa katika hela ya kujikimu chuoni (boom).

Kwa sasa biashara hainiendei vizuri hivyo nimekuja kwenu wanajukwaa naomba mnishike mkono kupatiwa kazi yoyote iliyo ya halali ambayo haitanitweza utu wangu.

Nipo hapa hapa Dar es salaam

NB: nje ya masuala yangu ya ujasiriamali pia nina kipaji kutengeneza maudhui mitandaoni (content creator) na uanamitindo na urembo.

Pia kama kuna mtu ana namna anaweza kuniunganisha na masuala haya ya urembo na uanamitindo nitashukuru sana kwa kweli hali ya kukaa bila kuwa na ishu ya kuingiza pesa ya ziada inanipa deprression kubwa.

Yeyote atakaeguswa na ombi langu basi anicheki PM

Asante
GGM wametangaza nafasi za internships Finance ingia uombe
 
Back
Top Bottom