hizi kauli ufanya watu kuogopa biashara, unapotaka kumtenga mtu na Mungu wake inakuwaje???je unataka investment ya muda mfupi au mrefu, specify,pili biashara hiyo utasimamia mwenyewe au unataka uweke mtu wa kuisimamia? Je unataka biashara hiyo ndo uitegemee kwa maisha ya kila siku? Uko tayari kwenda kinyume cha imani yako(kama una imani/dini) ?
hizi kauli ufanya watu kuogopa biashara, unapotaka kumtenga mtu na Mungu wake inakuwaje???
Mkuu, wewe ni mtu muhimu sana katika kuelimisha jamii ila napata shida kwa jinsi ambavyo umejibu swali langu, kuna baadhi ya kauli zako hapa zimekuwa za jazba. Maana yangu ni kuwa kwani haiwezekani mtu akafanya biashara isiyokinzana na imani yake ya dini na bado akafanikiwa? Mimi binafsi nimejiajiri na ushauri mwingi nimesoma hapa na kuufanyia kazi lakini kujiajiri kwangu hakukinzani na imani yangu na ninaona mafanikio................Hapa unakwepa ukweli ulio dhahiri ktk maisha ya kila siku.
Wenye dini zao hawafanyi biashara zinazokinzana na dini zao mkuu,wewe uko wapi ambako huyaoni hayo? Pombe zinauzwa hadharani kabisa, na wenye dini zao hawafanyi biashara hiyo. Nguruwe wanafugwa, wanauzwa na kuliwa peupe lakini kuna wenye dini zao wanakaa kando.
Wasio na dini wanabeba sembe, wanakula swine,wanapika pombe, wanalima bange na kufanya mengine yanayofanana na hayo mkuu ndani ya bongo hii hii. Halali yako ni haramu ya mwenzio na ndio maana sheria zikawekwa.Nchi yetu haina dini ili tusio na dini tupate nafasi ya kufanya tuwezavyo bila kumkanyaga mtu mguu wake.
Mkuu, huku ni biashara, jukwaa la dini lipo. Nimemshauri huyo ndugu ili achague moja kt ya kumfuata muumba wake au biashara ambayo inakinzana na imani yake, nikamuuliza je uko tayari. Kwa sababu ningeweza kumwambia afungue bar kumbe imani yake inamkataa. Hapo ubaya uko wapi?
Mkuu, wewe ni mtu muhimu sana katika kuelimisha jamii ila napata shida kwa jinsi ambavyo umejibu swali langu, kuna baadhi ya kauli zako hapa zimekuwa za jazba. Maana yangu ni kuwa kwani haiwezekani mtu akafanya biashara isiyokinzana na imani yake ya dini na bado akafanikiwa? Mimi binafsi nimejiajiri na ushauri mwingi nimesoma hapa na kuufanyia kazi lakini kujiajiri kwangu hakukinzani na imani yangu na ninaona mafanikio................
Wewe ndio umekuja na neno lililojificha nyuma ya pazia. Naomba turudi kwenye topic husika. Dini ina jukwaa lake. Huku tukate mabizinezi. Nimefafanua kwa nini nilimshauri mtu yule achague.
we nawe ...hiyo hela njoo nayo tukakupeleke kwenye bar zenye mademu wakali tupige monde ...mambo ya biashara achia wachaga
Samahani mkuu malila, hayo mashamba ya laki nne kuna vyanzo vya maji? Mimi kiu yangu kubwa ni kufanya hotculture, na nikipata shamba karibu na dar naona ndiyo haswaa nitakuwa karibu na soko.
......wakati tunamsubiri Malila, fikiria upatikanaji wa maji kwa kuchimbisha visima.
'Wataalamu' wapo wengi tu waliofanya uwekezaji katika sector hiyo.[/QUOTE
Yapo mashamba Mkuranga ambayo yapo kando ya mito. Ni km 60 toka Tazara pale kwenye mataa. Hivi vijito havikauki. Yapo karibu na barabara na usafiri public kwa maana ya daladala upo. Kazi kwako.
Samahani mkuu malila, hayo mashamba ya laki nne kuna vyanzo vya maji? Mimi kiu yangu kubwa ni kufanya hotculture, na nikipata shamba karibu na dar naona ndiyo haswaa nitakuwa karibu na soko.