Mtaji wa Milioni 5-10 (TZS): Biashara gani unaweza kufanya?

Mtaji wa Milioni 5-10 (TZS): Biashara gani unaweza kufanya?

je unataka investment ya muda mfupi au mrefu, specify,pili biashara hiyo utasimamia mwenyewe au unataka uweke mtu wa kuisimamia? Je unataka biashara hiyo ndo uitegemee kwa maisha ya kila siku? Uko tayari kwenda kinyume cha imani yako(kama una imani/dini) ?
hizi kauli ufanya watu kuogopa biashara, unapotaka kumtenga mtu na Mungu wake inakuwaje???
 
hizi kauli ufanya watu kuogopa biashara, unapotaka kumtenga mtu na Mungu wake inakuwaje???

Hapa unakwepa ukweli ulio dhahiri ktk maisha ya kila siku.

Wenye dini zao hawafanyi biashara zinazokinzana na dini zao mkuu,wewe uko wapi ambako huyaoni hayo? Pombe zinauzwa hadharani kabisa, na wenye dini zao hawafanyi biashara hiyo. Nguruwe wanafugwa, wanauzwa na kuliwa peupe lakini kuna wenye dini zao wanakaa kando.

Wasio na dini wanabeba sembe, wanakula swine,wanapika pombe, wanalima bange na kufanya mengine yanayofanana na hayo mkuu ndani ya bongo hii hii. Halali yako ni haramu ya mwenzio na ndio maana sheria zikawekwa.Nchi yetu haina dini ili tusio na dini tupate nafasi ya kufanya tuwezavyo bila kumkanyaga mtu mguu wake.

Mkuu, huku ni biashara, jukwaa la dini lipo. Nimemshauri huyo ndugu ili achague moja kt ya kumfuata muumba wake au biashara ambayo inakinzana na imani yake, nikamuuliza je uko tayari. Kwa sababu ningeweza kumwambia afungue bar kumbe imani yake inamkataa. Hapo ubaya uko wapi?
 
Mkuu wangu haya mambo ya hz DINI zakuletewa na watu weupe ni unafki2! Manake hao wanaosema kitu flan ni dhambi kutumia au kuuza tunakutana kwenye vikorido kimya kimya! Kwenye dunia hii akili kichwani mwako!
 
Hapa unakwepa ukweli ulio dhahiri ktk maisha ya kila siku.

Wenye dini zao hawafanyi biashara zinazokinzana na dini zao mkuu,wewe uko wapi ambako huyaoni hayo? Pombe zinauzwa hadharani kabisa, na wenye dini zao hawafanyi biashara hiyo. Nguruwe wanafugwa, wanauzwa na kuliwa peupe lakini kuna wenye dini zao wanakaa kando.

Wasio na dini wanabeba sembe, wanakula swine,wanapika pombe, wanalima bange na kufanya mengine yanayofanana na hayo mkuu ndani ya bongo hii hii. Halali yako ni haramu ya mwenzio na ndio maana sheria zikawekwa.Nchi yetu haina dini ili tusio na dini tupate nafasi ya kufanya tuwezavyo bila kumkanyaga mtu mguu wake.

Mkuu, huku ni biashara, jukwaa la dini lipo. Nimemshauri huyo ndugu ili achague moja kt ya kumfuata muumba wake au biashara ambayo inakinzana na imani yake, nikamuuliza je uko tayari. Kwa sababu ningeweza kumwambia afungue bar kumbe imani yake inamkataa. Hapo ubaya uko wapi?
Mkuu, wewe ni mtu muhimu sana katika kuelimisha jamii ila napata shida kwa jinsi ambavyo umejibu swali langu, kuna baadhi ya kauli zako hapa zimekuwa za jazba. Maana yangu ni kuwa kwani haiwezekani mtu akafanya biashara isiyokinzana na imani yake ya dini na bado akafanikiwa? Mimi binafsi nimejiajiri na ushauri mwingi nimesoma hapa na kuufanyia kazi lakini kujiajiri kwangu hakukinzani na imani yangu na ninaona mafanikio................
 
Wewe ndio umekuja na neno lililojificha nyuma ya pazia. Naomba turudi kwenye topic husika. Dini ina jukwaa lake. Huku tukate mabizinezi. Nimefafanua kwa nini nilimshauri mtu yule achague.
 
Wewe ndio umekuja na neno lililojificha nyuma ya pazia. Naomba turudi kwenye topic husika. Dini ina jukwaa lake. Huku tukate mabizinezi. Nimefafanua kwa nini nilimshauri mtu yule achague.

Malila

I salute you...pia niongeze jambo, kama mtu amechukua mawazo ndani ya huu uzi na akayatekeleza, basi ni vyema akaja kutoa ushuhuda wa changamoto na mafanikio aliyokutana nayo kwenye biashara husika.
 
Last edited by a moderator:
quote_icon.png
By Mgombezi

Mimi ni mfugaji, nitakushauri kufuga ngombe kwa mchakato ufuatao:

Ujenzi wa banda = Ths 500,000/=
Manunuzi ya Ngombe 5 x Tsh 900,000 = Tsh 4,500,000/=
(Ngombe utawanunua wakiwa na mimba ya miezi 6)
Kuwahudumia ng'ombe kwa miezi mitatu kabla ya production = Tsh 1,500,000/=
(inahusisha mshahara kwa wafanyakazi wawil + chakula + madawa)

Jumla = Tsh 6,500,000/=

Baada ya Miezi 3;

UZALISHAJI:

Ngombe hawa watakuwa wakitoa maziwa si pungufu ya lita 5 kwa asubuhi na jioni kwa kila ng'ombe. Hivyo uzalishaji kwa siku utakuwa lita 10 kwa siku kwa ng'ombe.

MAPATO

Lita 10 x Ng'ombe 5 = lita 50 kwa siku x Tsh 1000 (bei ninayouza mimi hapa) = Tsh 50,000 kwa siku
Mapato kwa mwezi = Tsh 50,000 x 30 = 1,500,000/=

Gharama za uendeshaji kwa mwezi = Tsh 600,000/=

Faida = Tsh 900,000/= kwa mwezi

BAADA YA MIAKA 5:

Kumbuka ng'ombe huzaa kila mwaka hivyo basi baada ya miaka mitano utakuwa na ng'ombe wasiopungua 25. Kipato chako kwa mwezi unaweza kufikia si pungufu Tsh 18,000,000 endapo utakuwa na ngombe jike 20 kati ya hao 25.

****sijaelewa hiyo hesabu ya hapo pekundu inakujaje*******
 
  • Thanks
Reactions: Mbu
Wanajamvi nina Tsh 10,000,000 (shilingi milioni kumi) nisaidieni ushauri wa aina ya biashara nitakayofungua niweze kuishi mjini Dodoma pamoja na familia yangu kwa kufanya biashara

Karibuni mnipe ushauri na elimu ya ujasiriamali
 
Kanunue kiwanja pale cda cha kama square mita 500 hivi kisha wakikupa offer utaombea mkopo, of course utahitaji kuwa na ramani ya nyumba unayotaka kujenga, building permit. ukijenga hostel itakuwa safi maana dodoma demand ya hostels ni kubwa.
 
Dodoma biashara nzuri kwa pesa yako ni ya mazao. Fanyia utafiti, tumbukize 3M kwa majaribio.
 
......mwendo mdundo.......na kazi inaendelea.......hii mada mali sana
 
  • Thanks
Reactions: Mbu
Samahani mkuu malila, hayo mashamba ya laki nne kuna vyanzo vya maji? Mimi kiu yangu kubwa ni kufanya hotculture, na nikipata shamba karibu na dar naona ndiyo haswaa nitakuwa karibu na soko.
 
......wakati tunamsubiri Malila, fikiria upatikanaji wa maji kwa kuchimbisha visima.

'Wataalamu' wapo wengi tu waliofanya uwekezaji katika sector hiyo.
 
Last edited by a moderator:
Mkuu mbu nashukuru kwa ushauri mzuri,siyo vibaya hata wewe kama unafahamu maeneo ya karibu na dar ambapo naweza pata walau ekari tano za kuanzia ukanipm mkuu. Natanguliza shikirani.
 
  • Thanks
Reactions: Mbu
......wakati tunamsubiri Malila, fikiria upatikanaji wa maji kwa kuchimbisha visima.

'Wataalamu' wapo wengi tu waliofanya uwekezaji katika sector hiyo.[/QUOTE

Yapo mashamba Mkuranga ambayo yapo kando ya mito. Ni km 60 toka Tazara pale kwenye mataa. Hivi vijito havikauki. Yapo karibu na barabara na usafiri public kwa maana ya daladala upo. Kazi kwako.
 
  • Thanks
Reactions: Mbu
Samahani mkuu malila, hayo mashamba ya laki nne kuna vyanzo vya maji? Mimi kiu yangu kubwa ni kufanya hotculture, na nikipata shamba karibu na dar naona ndiyo haswaa nitakuwa karibu na soko.

Kuna vijito viwili visivyokauka mwaka mzima.
 
  • Thanks
Reactions: Mbu
Back
Top Bottom