Hapa unakwepa ukweli ulio dhahiri ktk maisha ya kila siku.
Wenye dini zao hawafanyi biashara zinazokinzana na dini zao mkuu,wewe uko wapi ambako huyaoni hayo? Pombe zinauzwa hadharani kabisa, na wenye dini zao hawafanyi biashara hiyo. Nguruwe wanafugwa, wanauzwa na kuliwa peupe lakini kuna wenye dini zao wanakaa kando.
Wasio na dini wanabeba sembe, wanakula swine,wanapika pombe, wanalima bange na kufanya mengine yanayofanana na hayo mkuu ndani ya bongo hii hii. Halali yako ni haramu ya mwenzio na ndio maana sheria zikawekwa.Nchi yetu haina dini ili tusio na dini tupate nafasi ya kufanya tuwezavyo bila kumkanyaga mtu mguu wake.
Mkuu, huku ni biashara, jukwaa la dini lipo. Nimemshauri huyo ndugu ili achague moja kt ya kumfuata muumba wake au biashara ambayo inakinzana na imani yake, nikamuuliza je uko tayari. Kwa sababu ningeweza kumwambia afungue bar kumbe imani yake inamkataa. Hapo ubaya uko wapi?