Mtaji wa Milioni 5-10 (TZS): Biashara gani unaweza kufanya?

Amen!
No worries..

Yas mimi mzee wang alikufa.. so aliacha nyumba nne.. Watoto tuko watatu; tukagawana kila mmoja akapata yake ile moja tukauza. Sasa kila mmoja alipata mil 16 hiv. Mimi nikaenda Kibaha nikanunua kiwanja nikajenga vyumba 8.

Wezangu wakaanzisha biashara... Ni mwaka wa tatu sasa wenye biashara zishakufa na wapo kwenye msoto... Mmoja kauza nyumba tuliogawana.. So nina experience mkuu.. Wewe wekeza tu kwenye ujenzi itakusaidia baadae..
 
umsimdanganye.....
Hii biashara ni kichaa....
Ki uhalisia iko tofauti...
Na ulivyo changa nua.
 
wekeza kwenye ujenzi/nyumba.
 
Tafuta Kibali cha kuuza mkaa. Uwe unanunua Mkaa kutoka vijijini kwa bei poa kabisa. Ukiondoa yote baada ya kuuza mkaa unaweza pata faida hata 50%. Changamoto ni eneo la biashara.
 

bodaboda ni pasua kichwa na hasa zikiwa mabali na eneo unaloishi. Baada ya muda utasikia kuwa imeibiwa! Fikiria kuhusu biashara ya mazao kwa msimu unaokuja
 
You will never go wrong investing in real estate and if you are also patient try investing in stocks.

I do not know how the market in Tz is but if I were you, I would invest as follows
1.50% in real estate(land and buildings)
2.40% in stocks
3.10% in cash( for emergencies).

Considering that you are employed, you should consider topping up these investments periodically(monthly for stocks and cash and Quarterly for real estate)
 
zuuth

Naona unajifunza kwa walioshindwa. Je nyumba yako ingeezuliwa na kubomolewa na mafuriko ungesemaje? We si ungekuwa umefulia. kweli biashara ni mipango na utekelezaji.
 
Last edited by a moderator:
Vipi kama hizo pesa zilipatikana kwa biashara ya bia? Ila nimegundua watu mna imani za ajabu ajabu sana kuhusu pesa za urithi. Ukweli ni kwamba pesa yeyote ya kupewa bure bure kuitumia kuzalisha ni kazi sana sio suala la kuonwa na marehemu wala nini.
 
Wewe ndio umeongea hawa boda boda, bajaj na daladala ili mwende sawa inabidi wewe uwe muhuni zaidi yao. Ukiwasikiliza lazima uishie na hadithi za bwana Elli.

Mi nilishawahi kufanya bajaj na nilikuwa nafanya hivyo hivyo. Kuna kipindi nilibadili dereva wa bajaj kama mara 6 hivi ndani ya miezi miwili. Akileta longo longo nahakikisha analipa deni na bajaj naichukua na kuweka mwingine. Wapo vijana wana malengo mnaweza kufanya kazi vizuri tu ili kuwapata si kazi rahisi.
 
Last edited by a moderator:

Ya! Mim nakushauri kama unamtu wa karibu ambaye unamwamin anaweza kusimamia mradi wa kuku wa mayai hiyo inatosha kabisa kukuza seti ya kuku elfu moja wa mayai na baada ya miezi sita utakuwa unatengeneza hela nzuri, habari zaidi kuhusu hili watafute wanaofuga watakushauri zaidi.
Jambo la pili ukiona unashindwa kabisa tafuta kiwanja sehemu ambayo ukiikadiria unaona thamani yake inakuwa kwa kasi nunua kwa bei sawa na hiyo hela au chini yake kama inawezekana baadae unaweza kujenga au kuuza ukiamua.
 
naona unajifunza kwa walioshindwa je nyumba yako ingeezuliwa na kubomolewa na mafuliko ungesemaje we si ungekuwa umefulia kweli biashara ni mipango na utekelezaji
Mi nimeshangaa hasa eti ndugu zake wamechemsha ndio anahitimisha hela ya urithi haifanyiwi biashara!! Ingekuwa hivyo hizi kampuni zenye miaka zaidi ya 200 si zingekuwa hazipo zote!
 
Wekeza Fanya biashara hiyo pesa izalishe usiifungie baada ya muda haitakuwa na thamani hiyo but ukiwekeza utaiongeza.
 
Vizur saana mkuu...nenda Kibaha nunua kiwanja for 3m inayobakia anza ujenzi.
Mkuu Kibaha ipi? Maana maeneo mengi bei ipo juu kwelikweli. We tutupie vieneo hivyo tukatembelee.
 

Njoo Buyuni hapa Vigwaza kata pori la eka 10 kwa Tsh 4.3m, kisha zinazobaki weka akiba benki, huku ukipambanua na kuchanganua miradi kadhaa itakayojitokeza. Au njoo hapa Mkuranga, nunua shamba kando ya mto eka kumi kwa milioni saba, kisha tulia, bei inapanda sana mitaa hii ya Mkuranga. Deal nyingi zinahitaji usimamizi wa karibu sana na saa nyingine inabidi kuwa mnoko sana ili hela irudi.

Kwa real estate, inabidi mtaji uwe mzuri, japo hiyo pesa waweza anzia kwa kununua kiwanja.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…