Mtaji wa Milioni 5-10 (TZS): Biashara gani unaweza kufanya?

Mtaji wa Milioni 5-10 (TZS): Biashara gani unaweza kufanya?

......umeona ee?

....hahhaha, halafu jamaa wana hoji kwa hasira kweli badala ya kuchukua business ideas mbali mbali zilizomo humu.
Anyway, hamadi kibindoni, tunasonga mbele.
Heshima mbele mkuu Malila, umetufungua akili kwa mengi uliyotufunza humu.

Nataka kujaribu "kwa fujo" kilimo cha zao la ufuta kijijini Mkenge, (Between Kimazichana na Mkuranga.)

Lima bila hofu,ile mitaa mizuri udongo wake uko vizuri. Mimi naingiza kuku wa kienyeji wa kutosha,nimefanya pilot imenipa moyo sana. Pembeni ni kambale kwa kwenda mbele.
 
  • Thanks
Reactions: Mbu
Kwani kiongoz wangu huna kipaj? Kama unacho wekeza huko, kama huna basi jiulize unapenda biznec gan? Hiyo unayoipenda watafute walio fanikiwa uwaulize na watakushauri vzur., ni hayo tu kiongoz. kumbuka fedha ni uwekezekaji, bila uwekezaji itaisha tu. Na vile unafamilia teh teh.
 
Wana JF wenzangu nawashukuru kwa mawazo mazuri,hiyo ni ishara kuwa Vijana tukiamua tunaweza kabisa kujitegemea.
 
Unaweza kuifanya biashara hii hata kama unakaribia kwenda mbinguni, kule vijijini watu wanauza misitu yenye miti inayokaribia kuvunwa kwa bei ya kutupwa kabisa, unanunua kamsitu kako, na wewe unatafuta mnunuzi tena unauza au unavuna mwenyewe na unapata faida kubwa,na ukaachana na taabu za tra na ndugu zao. Na kama una vijana/wadogo zangu wafundishe kazi hii, kwa sababu haihitaji usimamizi wa kila siku, kwa mwaka mara moja tu basi. Sehemu kubwa ya mwaka miti inapogoma yenyewe huko shambani.

mkuu bei ya msitu iko vipi?
 
Nitafute inbox ili nikuunganishe kwenye biashara ya mpunga yaani. Unanunua mazao kipindi cha mavuno kwa bei ya chini...then unayahifadhi. Alafu unayauza kipind cha njaa kwa Bei ya zaidi ya Mara mbili mpaka Tatu ya ile ulionunulia...
 
wajameni eeh, nimebahatika "kupata" mahala ka-Mtaji. Ni kiasi cha shs. milioni kumi tu, (10,000,000/=) za Kitanzania. Nipeni mapendekezo nizi invest wapi, kivipi na matarajio ya faida.
(i.e biashara gani inalipa (plus location), kwa muda gani, na SWOT analysis zake)

10m/= inatakiwa kwa siku iwe inazalisha sio chini ya 55,000/=, kwa wiki 385,000/=.

Biashara gani? Hapo naona ya chakula ndio poa, nafaka, lete toka mikoani, uza jumla, pia kuuza nyama buchani (bucha 2) zitatosha kabisa..

Location? Tafuta frame penye watu walio na kipato, upanga, oysterbay, msasani, mikocheni, ada estate, kilongawima, mbezi beach etc...

Mtaji utarudi baada ya mwaka plus faida (roughly + 20m/=)...

Kila la heri..
 
Safi mkuu nimependa ushauri wako
 
Mm nakushauri ufungue biashara ya pub,unaweza pata faida baada ya muda mfupi sana
 
Nikiwa napita pita hpa,najionea jambo kubwa sana ambalo nilikuwa nalifikilia,
Mii binafsi ina taji wa milion tatu,nataka nikiwekeze kiasi hiki kwenye biashara,je wadau mwanishauri vip
 
Nikiwa napita pita hpa,najionea jambo kubwa sana ambalo nilikuwa nalifikilia,
Mii binafsi ina taji wa milion tatu,nataka nikiwekeze kiasi hiki kwenye biashara,je wadau mwanishauri vip

Tembelea kwanza wenye biashara zenye makazi na wafanyabiashara wenyewe wawe wenye makazi. Hapo ndipo utapata pa kuanzia. Na usikurupuke kwenye hili na tafuta q\wataalamu wenye kutambulika sio wavaa suit kubwa utajuta. Achana na washauri wa mitaani. Kama utakuwa na kuhitaji maelekezo nitafute
 
wajameni eeh, nimebahatika "kupata" mahala ka-Mtaji. Ni kiasi cha shs. milioni kumi tu, (10,000,000/=) za Kitanzania.

Nipeni mapendekezo nizi invest wapi, kivipi na matarajio ya faida.
(i.e biashara gani inalipa (plus location), kwa muda gani, na SWOT analysis zake)

Tembelea kwanza wenye biashara zenye makazi na wafanyabiashara wenyewe wawe wenye makazi. Hapo ndipo utapata pa kuanzia. Na usikurupuke kwenye hili na tafuta q\wataalamu wenye kutambulika sio wavaa suit kubwa utajuta. Achana na washauri wa mitaani. Kama utakuwa na kuhitaji maelekezo nitafute
 
huo ushauri wa ngombe unafaa kweli.. ila sas kuna gharama za wafanyakazi
 
Wadau mimi ni Mwajiriwa,

Katika mambo ya urithi leo hii nimepewa mgao wangu wa 10mil cash. Nimeweka kwenye Account yangu nafikiria kitu cha kuifanyia.

Kwa nyie wazoefu, nipeni ushauri kibiashara ila mkizingatia mie ni mwajiriwa.

Nitashukuru kwa kila wazo chanya
 
Kwa mfano ninunue boda boda 8 kwa bei ya jumla.. nifungue account say BOA bank. Kila nikipewa cash nadeposit huko.. Then cash inflow niwe nanunua boda boda moja kila mwezi. After six months si naweza kukopa na kununua boda boda nyiingi zaidi au!???
Dahh kaz kweli kweli!!!
Nahitaji kutulia
 
Back
Top Bottom