Mtaji wa Milioni 5-10 (TZS): Biashara gani unaweza kufanya?

Mtaji wa Milioni 5-10 (TZS): Biashara gani unaweza kufanya?

Tulia kwanza usiweweseke. Inaonekana 10m hukuwahi kufikiri kuipata. Mimi nashauri kwanza usiwe na papara. Tulia kwa zaidi ya miezi 6. Nilishawahi kamata hela ndefu sana miaka michache iliyopita, papara niliyokua nayo ya kufungua biashara kedekede ili eti kuzidisha hela ilinimaliza tu.

This time around niko much wiser. Hata idondoke 500m sasa hivi, yani natulia kama mwaka tu hivi bila kuwa na kimbelembele labda itokea opportunity ya wazi wazi kabisa.
 
Mkuu pesa ya urith haifanyiwi biashara....ujui mzee kapataje..nenda tafuta kiwanja jenga then pangisha itakusaidia maisha yako yoote

m10 tu anunue kiwanja na kujenga mbona kanma haitoshi kabisa, labbda afanyie finishing kama nyumba alikuwa nayo
 
wakati bado unashangaa usiidoke doke ipeleke UTT, wekeza huko pesa yako itaendelea kukua pale utakapo pata cha kufanya ichukue
 
Fungua biashara ndogo isiyozidi nusu ya hela uliyonayo then isimamie mwenyewe... Utaona returns nzuri tuu....biashara zote in nzuri kikubwa ni usimamizi.
 
Kama huna wazo la biashara, chukua robo tatu ya fedha hiyo nunua kiwanja hata kule Kibaha Pwani, nyingine rekebisha matatizo madogo madogo ya home na kama una mtoto anasoma mlipie ada ya mwaka kabisa, then tulia. Kile Kiwanja kitapanda thamani kila siku kinaweza kukusaidia baadae.
 
uuuuuuuuwi kwa mfano tu awe ni mwanaume kapata 20ml hajui chakufanya jaman hivi mtoa mada uko serious au unawaza endapo utapata
 
Futa kabisa wazo hilo.
Kwanza kwa pesa hiyo huwezi kununua bodaboda nane.
Halafu usiwekeze kwenye Biashara moja.
Ushauri wa bure:
10m,unaiona ni pesa kubwa,lakini kiukweli ni pesa ndogo sana.Ila inaweza kuzalisha pesa kubwa kama ukituliza kichwa chako.
Na hali ilivyo ni kwamba bado unapapara,nakushauri iweke Bank kama miezi mitatu kisha ndio uifanyie mradi wako unaotaka kufanya.La sivyo utajuta.

Kwanza nakushauri toa kama 700,000 umtolee sadaka Marehem ili upate Baraka zake,maana bila yeye usingezipata.
na tabia ya pesa za Urithi,yaani kama ulitoa hata elfu moja katika hizo ukaenda kunywea bia basi hata ufanye nini umaskini ni wa kwako hadi unaingingia kaburini.Maana wafu wanaona matendo yetu
sumtymz maendeleo/mafanikio tunayachelewesha si wenyewe kwa imani zisizo kuwa na msingi..hiyo sadaka akaitoe wapi???
 
Kwanza nakushauri toa kama 700,000 umtolee sadaka Marehem ili upate Baraka zake,maana bila yeye usingezipata.
na tabia ya pesa za Urithi,yaani kama ulitoa hata elfu moja katika hizo ukaenda kunywea bia basi hata ufanye nini umaskini ni wa kwako hadi unaingingia kaburini.Maana wafu wanaona matendo yetu

Acha kudanganya watu wewe, wafu wanaona wapi matendo yetu? Wakiona enhee wanafanyeje? Hii imani itakua yako tu lakini sio universal
 
Wadau mimi ni Mwajiriwa,

Katika mambo ya urithi leo hii nimepewa mgao wangu wa 10mil cash. Nimeweka kwenye Account yangu nafikiria kitu cha kuifanyia.
Mdau,
Umebobea kwenye shughuli gani? Umeajiriwa kwenye shughuli gani? Unaishi wapi? Umeoa/olewa? Kama umeoa "partner" wako anajishughulisha na nini?
 
Inaelekea huna idea ya biashara hadi ujue ufanyie nini. Nenda kanunue hisa ndo biashara isioumiza kichwa
 
Nami nataka kufuga sasa naomba unielekeze hapo kwenye kiwanja safi cha kufanyia mifugo hiyo ya ngombe mkuu nahitaji

Unataka kufuga kwa ajili ya nyama au maziwa, kama ni nyama itakuwa rahisi zaidi. unaanza na wa kienyeji, na msimu mzuri wa kukusanya ndama kwa bei nzuri unakaribia.
 
Wakati huu yapaswa kutulia ikizingatiwa una ajira inayokuwezesha kwa mambo mengine .. Ukiweza fanya utafiti kujua ni benki gani inatoa rate kubwa kwa fixed deposit fungua account tupia hela umo then kaa fikiri kwa miezi 6 nini cha kufanya kwa kuuliza wadau humu na kuoanisha na mazingira uliyopo na kuangalia wengine wanaofanya kitu hicho eneo hilo kwa kifupi upate muda wa kutosha kufanya utafiti wa uwekezaji huku hela ikiongezeka benki kidogo
 
Kama unahitaji nitakupa mtu ambaye mtafanya naye biashara ya BOX(Kuagiza mizigo ya maduka ya jumla) ni biashara safi. utatengeneza pesa nzuri tu.
 
I have made up my mind.
Nina kiwanja 40 by 40 maeneo ya chekereni Arusha.
Nataka nifuge kuku tu, wa kienyeji na wa kisasa. Tatizo umeme haujafika.
Nahitaji mtaalam wa solar pia naweza kupata incubator hapa Arusha??
Nianze project fasta. Kila jioni badala ya kwenda bar. Naenda kwenye mradi.
 
Jipange.... Ukihitaji incubator hapo Arusha itakufikia kutoka Nairobi within three days ex China, full automatic at a very reasonable price.
 
USHAURI WANGU:

Hiyo hela ni nyingi sana kama utakuwa na akili lakini kama kichwa chako ni zero itaonekana ndogo. Mie nakushauri utafute eneo uonyeshe mipira ya Ulaya na ya hapa Bongo utapata faida kubwa sana tena mtaji wake hauzidi milioni 3. Halafu hizo 7 zinazobaki utajiongeza mwenyewe.
 
Wadau mimi ni Mwajiriwa,

Katika mambo ya urithi leo hii nimepewa mgao wangu wa 10mil cash. Nimeweka kwenye Account yangu nafikiria kitu cha kuifanyia.

Kwa nyie wazoefu, nipeni ushauri kibiashara ila mkizingatia mie ni mwajiriwa.

Nitashukuru kwa kila wazo chanya

Nunua shares za Swissport, NMB Na CRDB au TBL Na TCC.
 
Mkuu pesa ya urith haifanyiwi biashara....ujui mzee kapataje..nenda tafuta kiwanja jenga then pangisha itakusaidia maisha yako yoote

Sawa mkuu..
But which location..what kind of house with that amount?
I'm just thinking aloud...
 
Back
Top Bottom