Evelyn Salt
JF-Expert Member
- Jan 5, 2012
- 70,916
- 141,437
Twende nae jacana au carribean..... Au ushahama mpwapwaBora atutafte tumsaidie matumizi
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Twende nae jacana au carribean..... Au ushahama mpwapwaBora atutafte tumsaidie matumizi
Nihame niende wapi, mweke sawa tu tukamsaidie kupanga bajetiTwende nae jacana au carribean..... Au ushahama mpwapwa
Msaad ndugu kuhusiana na HII TAASISI ya uwekezaji. kama uta jali nilikua nahitaji maleezo kidogo... plss pm or whatsup 0659666123kwa ushauri wangu hiyo hela wekeza katika taasisi za kifedha za kukuza mtaji kama vile utt pesa yako itakuwa kuna mifuko mbalimbali ya kununua hisa kadri bei ya vipande inavyvo panda ndio unapata faida na kuna mfuko ambao unatoa gawio kila baada ya miezi mitatu kama utawekeza kuanzia milioni mbili na kuna gawio kila baada ya mwaka mmoja kama utawekeza tsh milioni moja kumbuka hela yako ukiamua kuichukua unaweza ukaichukua ukitaka vilevile kuna mfuko wa umoja unaweza kuanzia elfu kumi na utawekeza kadri kulingana na uwezo wako na unapata faida bei jinsi inavyopanda na vilevile unaweza ukakopa hizo hisa ndio dhamana yako.
plss your numberIelekeze katika Biashara ya mtandao wa masoko (Multi Level Marketing). Ni pm kwa Maelezo zaidi.
Dah haya. Dah..kazi kwelkwelSikilizeni hiki kipindi kilichorushwa hewani na Channel 10 na Rifaro Africa Ltd kuelezea biashara yao ya mda wa maongezi na jinsi ambavyo unaweza kutengeneza mamilioni ya pesa kila mwezi kwa mtaji mdogo tu wa TZS 128,500
Kwa nini utumie mda wako wa maongezi kihasara hasara?
Wajameni eeh,
Nimebahatika "kupata" mahala ka mtaji. Ni kiasi cha Shs. milioni kumi tu, (10,000,000/=) za Kitanzania.
Nipeni mapendekezo nizi invest wapi, kivipi na matarajio ya faida (i.e biashara gani inalipa (plus location), kwa muda gani, na SWOT analysis zake).
=======
Wadau huu uzi umenivutia ... Nina nia ya kuanzisha kiwanda kidogo cha mafuta ya alizeti ... naomba anayejua hili anipe ufahamu ..faida na hasara zake
Habarini wakuu, mimi pia ni kiri ya kwamba huu uzi humekuwa ukinivutia zaidi,ninafarijika na mawazo yanayotolewa, mimi pia nimeanza kilimo cha mazao kama hoho, kitunguu, karoti na nina shamba lenye ekari 2.5 na pia lina vyanzo vya maji vizuri tu, nimeamua kuchimbia mipira chini kwa chini toka kwenye chanzo mpaka kwenye kisima nilichochimba,kwa maana hiyo sasa kilomo changu hakitategemea mvua sana,, sasa basi naombeni ushauri kwa aliyewahi kufanya kilimo cha naamna hii, uzoefu, faida, upandaji uzingatie nini hasa, aina ya mbolea ya kutumia kwenye mazao husika hapo juu,na mengineo
Mkuu, sorry niliahidi kukushauri ukikanusha kuwa kukukwapua hizo pesa na umefafanua vizuri. Kaka so far watu wengi wametoa ushauri. Wewe pia umetoa wazo lako la tender, etc. Miaka ya nyuma nikiwa Bongo nilifungua company na kazi zangu kubwa zilikuwa supplies. Ni kweli kazi hii inalipa sana lakini upataji kazi wake ni nimgumu sana. Unatakiwa kuwa na network ya uhakika. Pia kwa supplies hiyo pesa ni ndogo kwani unaweza pata kazi ya kwanza ukatakiwa utumie say 15m na malipo yakaje say 3 weeks after say 3 weeks. Kwa namna hiyo kama huna 'rescue plane' yaani mtu wakukupa pesa kiasi chochote unachotaka muda wowote itakushinda. Ninauzoefu nayo mkuu nilifanya japo kwangu tatizo ilikuwa kupata kazi kwani nilikuwa na rescue plane anytime nikitaka pesa nikaonyesha LPO jamaa fasta ananiwezesha.
Kwakuongezea ushauri wawakuu, mi nakushauri kama unaweza kakodi ha kadhaa Dodoma ulime Zabibu soko guaranteed na Breweries mkuu
Thanks msanii,
Wazo la kuwekeza ktk ardhi hasa miti (mitiki,milingoti,pines) ambayo growth rate yake ni kubwa na ina good future ni bomba sana. Hizo hela ni nyingi sana kwa shughuli za kuwekeza ktk miti ie mitiki kwa kuanzia. Siku ukipata hela kidogo kama milioni moja hivi nitafute,nitakupa mchanganuo kwa vitendo bure ushindwe mwenyewe.
Kwa sasa,tujitahidi kukamata ardhi ndugu zangu,tuendako kubovu sana.
Katika biashara ni hatari sana kuwekeza kwenye mradi mmoja (Concentration Risk) kwani ukipata hasara basi umepoteza kila kitu. Ni muhimu sana kupanga kuyaweka mayai yako kwenye makapu tofauti ili kapu moja likioza kwa sababu yai moja limeoza ndani ya kapu hilo basi makapu mengine yasalimike na hivyo kukuwezesha kuendelea na biashara yako (Diversification).
Ili kufanya diversification yenye tija basi hakikisha miradi unayotaka kuifanya in risk profiles ambazo hazishabihiani kabisa kwa maana kwamba kama vyanzo vya hasara vikitokea kwenye biashara moja basi vyanzo hivyo ni vyanzo vya faida kwenye biashara nyingine. Kwa mfano kama unataka kufanya biashara ya kuuza mablanketi basi fikiria kufanya na biashara ya kuuza barafu pia kwa sababu kama hakuna baridi basi mablanketi hayatauzika lakini barafu zitauzika kutokana na watu kutumia sana vitu vya baridi wakati wa joto hivyo hasara utakayoipata kwenye uuzaji duni wa mablanketi itafidiwa na faida utakayoipata kwenye uuzaji mwingi wa barafu.
Kama unafikiria diversification basi ushauri wangu ni kufikiria mradi wa Rifaro kwani vyanzo vyake vya hasara (Risk Profile) vinatofautiana sana na biashara za kawaida tulizozizoea na hivyo itakusaidia ku diversify risk ya kuwekeza kwenye miradi ambayo ina risks zinazoshabihiana.
Toa TZS 128,500 tu kwenye hizo hela zako uwekeze kwenye mradi wa Rifaro zilizobaki wekeza kwenye mradi utakaoamua kuufanya.
Kwa maelezo ya kina kwa nini uwekeze kwenye mradi wa Rifaro soma thread hii hapa
Kwa nini utumie simu yako ya mkononi bila kulipwa wakati kuna Rifaro?
Hata mimi nilitambua kuwa kadanganya. Hesabu ya carry ni alfu 15 kwa siku.Mkuu,usimpoteze mwenzio,hakuna Suzuki Carry inaleta hesabu ya 50,000 kwa siku.Ninauzoefu wa Biashara hiyo na ninaifanya.