Mtaji wa Milioni 5-10 (TZS): Biashara gani unaweza kufanya?

Mtaji wa Milioni 5-10 (TZS): Biashara gani unaweza kufanya?

kwa ushauri wangu hiyo hela wekeza katika taasisi za kifedha za kukuza mtaji kama vile utt pesa yako itakuwa kuna mifuko mbalimbali ya kununua hisa kadri bei ya vipande inavyvo panda ndio unapata faida na kuna mfuko ambao unatoa gawio kila baada ya miezi mitatu kama utawekeza kuanzia milioni mbili na kuna gawio kila baada ya mwaka mmoja kama utawekeza tsh milioni moja kumbuka hela yako ukiamua kuichukua unaweza ukaichukua ukitaka vilevile kuna mfuko wa umoja unaweza kuanzia elfu kumi na utawekeza kadri kulingana na uwezo wako na unapata faida bei jinsi inavyopanda na vilevile unaweza ukakopa hizo hisa ndio dhamana yako.
Msaad ndugu kuhusiana na HII TAASISI ya uwekezaji. kama uta jali nilikua nahitaji maleezo kidogo... plss pm or whatsup 0659666123
 
Wajameni eeh,

Nimebahatika "kupata" mahala ka mtaji. Ni kiasi cha Shs. milioni kumi tu, (10,000,000/=) za Kitanzania.

Nipeni mapendekezo nizi invest wapi, kivipi na matarajio ya faida (i.e biashara gani inalipa (plus location), kwa muda gani, na SWOT analysis zake).

=======

Mradi huu mpya ambao unaweza kuutumia kama njia ya uwekezaji mbadala utakufaa sana.
 
Zitoe sadaka ndugu, kisha fanya kazi kwa bidii Mungu atakupatia mara 70
 
Wadau huu uzi umenivutia ... Nina nia ya kuanzisha kiwanda kidogo cha mafuta ya alizeti ... naomba anayejua hili anipe ufahamu ..faida na hasara zake

Hebu share na mimi hapa kuhusu hiko kiwanda cha mafuta ya alizeti. Na shamba na michikichi yangu karibia 50.
Kwa sasa navuna na kutengeneza mawese kienyeji.
 
Habarini wakuu, mimi pia ni kiri ya kwamba huu uzi humekuwa ukinivutia zaidi,ninafarijika na mawazo yanayotolewa, mimi pia nimeanza kilimo cha mazao kama hoho, kitunguu, karoti na nina shamba lenye ekari 2.5 na pia lina vyanzo vya maji vizuri tu, nimeamua kuchimbia mipira chini kwa chini toka kwenye chanzo mpaka kwenye kisima nilichochimba,kwa maana hiyo sasa kilomo changu hakitategemea mvua sana,, sasa basi naombeni ushauri kwa aliyewahi kufanya kilimo cha naamna hii, uzoefu, faida, upandaji uzingatie nini hasa, aina ya mbolea ya kutumia kwenye mazao husika hapo juu,na mengineo

Unafanya/umejaribu green-house farming?

ImageUploadedByJamiiForums1468383679.354154.jpg

Source; MIRADI KWANZA: Getting Rich through Farming, Amazing findings!!
 
Mkuu, sorry niliahidi kukushauri ukikanusha kuwa kukukwapua hizo pesa na umefafanua vizuri. Kaka so far watu wengi wametoa ushauri. Wewe pia umetoa wazo lako la tender, etc. Miaka ya nyuma nikiwa Bongo nilifungua company na kazi zangu kubwa zilikuwa supplies. Ni kweli kazi hii inalipa sana lakini upataji kazi wake ni nimgumu sana. Unatakiwa kuwa na network ya uhakika. Pia kwa supplies hiyo pesa ni ndogo kwani unaweza pata kazi ya kwanza ukatakiwa utumie say 15m na malipo yakaje say 3 weeks after say 3 weeks. Kwa namna hiyo kama huna 'rescue plane' yaani mtu wakukupa pesa kiasi chochote unachotaka muda wowote itakushinda. Ninauzoefu nayo mkuu nilifanya japo kwangu tatizo ilikuwa kupata kazi kwani nilikuwa na rescue plane anytime nikitaka pesa nikaonyesha LPO jamaa fasta ananiwezesha.

Kwakuongezea ushauri wawakuu, mi nakushauri kama unaweza kakodi ha kadhaa Dodoma ulime Zabibu soko guaranteed na Breweries mkuu

Hili la Zabibu nami nime lipenda, vipi mkuu una weza tupa mtiririko wa kilimo hiki cha zabibu?

1) Kwa maana ni saizi gani ya eneo litafaa kwa kupata faida ya kiasi au kubwa ?

2) ni eneo gani Dodoma lina stawi zaidi hasa kwa sisi ambao hatujawahi fika?

3) Ukodishaji wa shamba una kuaje ( gharama na muda wa Ukodishaji kwa kila heka)?

4) Bei ya zabibu kwa soko la ndani ikoje?

POLE kwa Swali refu Mkuu, tuna tamani kuwekeza, na uwanja huu ndio pa kujifunzia.
 
Thanks msanii,

Wazo la kuwekeza ktk ardhi hasa miti (mitiki,milingoti,pines) ambayo growth rate yake ni kubwa na ina good future ni bomba sana. Hizo hela ni nyingi sana kwa shughuli za kuwekeza ktk miti ie mitiki kwa kuanzia. Siku ukipata hela kidogo kama milioni moja hivi nitafute,nitakupa mchanganuo kwa vitendo bure ushindwe mwenyewe.

Kwa sasa,tujitahidi kukamata ardhi ndugu zangu,tuendako kubovu sana.

Malila , ushauri unapatikana inbox? Hasa ukizingatia nami naitafuta hiyo a Milioni nianze kufuata nyayo zako
 
Kaka upepo wa biashara sasa hivi nchini sio mzuri kabisa. Mie nakushauri ununue eneo lililopimwa na lenye hati kisha utulie baadae unaweza ukajenga hapo au kuuza na kupata faida kubwa maana ardhi kila siku inapanda bei. Kufanya biashara huku unafanya kazi ni ngumu sana maana utakosa usimamizi mzuri na kufaidisha hao utakaowapa ajira tu. Hiyo hela ni ndogo ila unaweza kununua kiwanja au hata viwanja viwili vitakavyokuja kukutoa sana baadae na pia hata na wewe ukaja kuwaachia urithi wanao
 
Katika biashara ni hatari sana kuwekeza kwenye mradi mmoja (Concentration Risk) kwani ukipata hasara basi umepoteza kila kitu. Ni muhimu sana kupanga kuyaweka mayai yako kwenye makapu tofauti ili kapu moja likioza kwa sababu yai moja limeoza ndani ya kapu hilo basi makapu mengine yasalimike na hivyo kukuwezesha kuendelea na biashara yako (Diversification).


Ili kufanya diversification yenye tija basi hakikisha miradi unayotaka kuifanya in risk profiles ambazo hazishabihiani kabisa kwa maana kwamba kama vyanzo vya hasara vikitokea kwenye biashara moja basi vyanzo hivyo ni vyanzo vya faida kwenye biashara nyingine. Kwa mfano kama unataka kufanya biashara ya kuuza mablanketi basi fikiria kufanya na biashara ya kuuza barafu pia kwa sababu kama hakuna baridi basi mablanketi hayatauzika lakini barafu zitauzika kutokana na watu kutumia sana vitu vya baridi wakati wa joto hivyo hasara utakayoipata kwenye uuzaji duni wa mablanketi itafidiwa na faida utakayoipata kwenye uuzaji mwingi wa barafu.

Kama unafikiria diversification basi ushauri wangu ni kufikiria mradi wa Rifaro kwani vyanzo vyake vya hasara (Risk Profile) vinatofautiana sana na biashara za kawaida tulizozizoea na hivyo itakusaidia ku diversify risk ya kuwekeza kwenye miradi ambayo ina risks zinazoshabihiana.

Toa TZS 128,500 tu kwenye hizo hela zako uwekeze kwenye mradi wa Rifaro zilizobaki wekeza kwenye mradi utakaoamua kuufanya.

Kwa maelezo ya kina kwa nini uwekeze kwenye mradi wa Rifaro soma thread hii hapa

Kwa nini utumie simu yako ya mkononi bila kulipwa wakati kuna Rifaro?

Aisee.Umenikumbusha Miaka Iyo Wakati Nasoma Financial Management.Nilisoma Kitu Kinaitwa Portfolio Investment.
"Don't put all Eggs Into One Basket" Adi Mifano Yako Uliyotoa..
Aisee
 
hiyo simpo endi klia. fungua duka la kuuza vifaa/matilio ya maiti maana watu kila siku wanakufa, kwa hakika hutalala njaa hadi unaingia kaburini. uza SANDA, JENEZA, PAFYUMU ZA MAITI, MAJI YA ZAMZAM nk, hapo mwaka wako ni mmoja tu unaanza kutembelea HAMA, CLUZA, PLADO, eksetla. ZINGATIA
 
Back
Top Bottom