Salaam Wanabodi.
Naomba kufahamishwa biashara ya kufanya kwa mtaji wa Shilingi Milioni Saba (TZS 7,000,000.00) Sehemu yeyote ndani ya Tanzania ikizingatiwa fedha zenyewe ni mkopo kutoka CRDB Bank wa kurudisha ndani ya Miaka Mitatu (3).
Mkopo huu niliopata kutoka CRDB ilikuwa ni kwa ajili ya kununulia gari, lakini machale yamenicheza nimeona ni bora nijiongezee kwa kuamua kutumia katika kufanya kazi za biashara na ujasiriamali,
Naomba kupatiwa wazo la biashara au ujasiriamali nitakaloweza kufanya ndani ya miaka mitatu niweze kurudisha mkopo wa benki niliyokopa kutoka CRDB Bank.
Nawasilisha