Mtaji wa Milioni 5-10 (TZS): Biashara gani unaweza kufanya?

Mtaji wa Milioni 5-10 (TZS): Biashara gani unaweza kufanya?

je unataka investment ya muda mfupi au mrefu, specify,pili biashara hiyo utasimamia mwenyewe au unataka uweke mtu wa kuisimamia? Je unataka biashara hiyo ndo uitegemee kwa maisha ya kila siku? Uko tayari kwenda kinyume cha imani yako(kama una imani/dini) ?
Mkuu kwenda vipi kinyume na imani ya dini naomba unifafanulie hapa
 
Nenda kaanzishe mwalo wa kuoshea mchanga wa dhahabu

Unalipa sana
 
Ng`ombe kweli wanalipa ( maziwa sio nyama),lakini jamaa yuko nje ya nchi. Mziki wa kutunza ng`ombe ukiwa mbali,tena ng`ombe wa maziwa si mchezo. Angekuwa Bongo ningemsaidia kumwonyesha kiwanja safi cha kufugia ng`ombe hao.
Nipo Bongo, napenda kujua zaid kiwanja cha kufugia hawa ng'ombe.
 
Salaam Wanabodi.

Naomba kufahamishwa biashara ya kufanya kwa mtaji wa Shilingi Milioni Saba (TZS 7,000,000.00) Sehemu yeyote ndani ya Tanzania ikizingatiwa fedha zenyewe ni mkopo kutoka CRDB Bank wa kurudisha ndani ya Miaka Mitatu (3).

Mkopo huu niliopata kutoka CRDB ilikuwa ni kwa ajili ya kununulia gari, lakini machale yamenicheza nimeona ni bora nijiongezee kwa kuamua kutumia katika kufanya kazi za biashara na ujasiriamali,

Naomba kupatiwa wazo la biashara au ujasiriamali nitakaloweza kufanya ndani ya miaka mitatu niweze kurudisha mkopo wa benki niliyokopa kutoka CRDB Bank.

Nawasilisha
 
mkuu wewe ni biashara gani ulikua unapenda sana kuifanya?

biashara ambayo unahisi utaifanya vizuri kuliko watu wengine wanavyoifanya?

biashara zote zina faida. tatizo sio biashara, tatizo ni wewe una advantage ya kufanya biashara gani kwa mafanikio?

angalia uzoefu wako, taaluma yako, ujuzi wako na vipaji vyako kisha tengeneza wazo la biashara linalo endana na navyo.

kila biashara ina faida, la sivyo watu wasingekua wanazifanya.
 
cha muhimu jitambue na ujue ujuzi ulilonao la kufanya biashara uitakayo, uwe na taaluma ya kitu unachotaka kufanya na uthubutu kufanya kila kitu kina ugumu wake mwanzoni hivyo tia bidii
 
mtaji mkubwa wa biashara ni akili yako.. hela hizo zitulize kwanza fixed.. huku unachekecha akili yako vizuri...

epuka matapeli
 
Habarini wana JF,

Baada ya kupambana kwa kipindi kirefu nimeweza kusave fedha kiasi mpaka kufikisha tsh million nane.Lengo la uzi huu ni kutaka kuwashirikisheni ndugu zangu hapa. Nina mawazo kadhaa ya kibiashara kulingana na eneo nililopo.

Lengo langu sasa ni angalau nipate ushauri which one is the best kati ya hayo mawazo niliyo nayo.

Mawazo hayo ni:
1. Stationery
2. Duka la vyakula/mangi
3. Mgahawa wa chakula
4. Maabara ndogo ya kupima afya
5. Kibanda cha miamala ya kifedha.

NB. Biashara zote nilizotaja hapo juu ninatamani kuongeza thamani kwa kuweka M- Pesa isipokua tu hiyo ya maabara.

KARIBUNI WAKUU.
 
Habarin wana jf. Baada ya kupambana kwa kipindi kirefu nimeweza kusave fedha kias mpka kufikisha tsh million nane.
Lengo la uzi huu ni kutaka kuwashirikishen ndugu zangu kweli. Nina mawazo kadhaa ya kibiashara kulingana na eneo nililopo. Lengo langu sasa ni angalau nipate ushaur which one is the best kati ya hayo mawazo nilio nayo.
Mawazo hayo ni:
1. Stationery
2. Duka la vyakula/mangi
3. Mgahawa wa chakula
4. Maabara ndogo ya kupima afya
5. Kibanda cha miamala ya kifedha.
NB. Biashara zote nilizotaja hapo juu ninataman kuongeza thaman kwa kuweka m pesa isipokua tu hiyo ya maabara.

KARIBUN WAKUU.

Wekeza kwenye saluni unafungua ya kike na kiume sehemu moja zinakuwa ni classic saloon zenye wadhifa ..mgahawa wa chakula unalipa pia it just depend eneo na ulivobuni eneo lako watu siku hizi wanapenda kula maeneo hata kama sehemu padogo lakini pavutie hata kwenye kiselfie
 
Back
Top Bottom