Pre GE2025 Mtangazaji wa ITV na Tundu Lissu hakika mmetutendea haki sisi watanzania kwenye kipindi cha dakika 45

Pre GE2025 Mtangazaji wa ITV na Tundu Lissu hakika mmetutendea haki sisi watanzania kwenye kipindi cha dakika 45

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Ukiendelea hivi, hakika tutajadili haya maswala ya nchi yetu vizuri.
Kumbe wakati mwingine akili inakurudia na kuwa sawasawa?
Basi nakuomba tafadhali baki hivyo hivyo, tutajadili kwa utulivu kabisa hatma ya nchi yetu hii.

Lakini ukweli unabaki pale pale. Samia ndiye atakuwa kiongozi wa mwisho wa CCM kama tunavyo ijuwa.
Tutaacha kumulaumu yeye, kwani amekuja kumalizia kazi tu iliyo anzishwa na watangulizi wenzake, ukiondoa waasisi wake.

"Nini kifanyike"? Unadhani hilo ni swali tena wakati huu. Mbona utakuwa umechelewa sana kuuliza swali hilo.
Nini kimetokea Appositle?
 
Tundu Lisu anatakiwa kwasasa akiwa na media tour waandishi waulize maswali mengi yanayohusu maswala ya sheria sheria kuliko ya chama chake

Huyu ni mtu muhimu sana anayeweza kufikisha ujumbe kwa wananchi wa kawaida na kuweza kuwafungua wajitambue na kutambua haki zao

Nimsaada mkubwa sana kwenye elimu ya uraia na sheria, maswali yakilenga "engo" hiyo yatawasaidia wengi halafu hayo ya chama chake atayaeleza kwenye majukwaa ya kisiasa
Media ya kufanya hayo ipo wapi! Watu wanapenda vijambo kama tamasha la Kizimkazi!
 
Tundu Lisu anatakiwa kwasasa akiwa na media tour waandishi waulize maswali mengi yanayohusu maswala ya sheria sheria kuliko ya chama chake

Huyu ni mtu muhimu sana anayeweza kufikisha ujumbe kwa wananchi wa kawaida na kuweza kuwafungua wajitambue na kutambua haki zao

Nimsaada mkubwa sana kwenye elimu ya uraia na sheria, maswali yakilenga "engo" hiyo yatawasaidia wengi halafu hayo ya chama chake atayaeleza kwenye majukwaa ya kisiasa
Well said
 
Wengi wetu tunasahau haraka sana....

Mh.Rais alishawahi kupata kusema "nikosoeni mtakavyo" ila MSITUKANE...kwani kwa waafrika matusi si uungwana na heshima ni jambo la kiutu na la lazima[emoji7]

#Nchi Kwanza[emoji7]

#Mh.Rais SSH raia nambari moja[emoji7]

..sasa mbona yeye kaanza kuita wanaomkosoa UMBWA?
 
Ushauri kwa Tundu Lissu, Kama yupo serious anataka urais, asisubirie kuzunguka kwenye majukwaa na vyombo vya habari. Na yeye awe updated kwenye mitandao ya kijamii awe anatoa clip fupi za dakika 1 mpaka 2 anapost mitandao yote ili kuwafikia vijana. Hasa Instagram (Instagram reels, instalive), Whatsapp channel, Telegram Channel, Youtube Channel, YouTube shorts, Facebook, TikTok, TikTok video, TikTok live. Awalenge zaidi vijana hasa hali ngumu ya kiuchumi na ukosefu wa ajira. Awe anapost kila siku consistently bila kuchoka.
Duh!

Huu kweli ni "ushauri" mkuu 'Akilindogosana'. Kwa mwonekano wa harakaharaka, mtu anaweza kusema ni ushauri mahsusi; lakini ukichuka muda na kufikiri kwa kina, hiyo nikazi kubwa, siyo kazi ya kufanywa namtu mmoja. Hiyo ni 'programme' pana sana inayo hitaji maandalizi na mali katika utekelezaji wake.

Lakini ni rahisi kushauri. Kazi kama hii inahitaji utafiti kwanza, na kuwafikia walengwa kupata 'feedback' toka huko kabla ya utekelezaji wake. Huwezi kuingia tu hivi hivi bila kuwa na msingi wapi uanzie. Itakuwa sawa na kuanzisha tu biashara yoyote na popote, mradi tu unao mtaji, bila ya kujuwa kama soko la bidhaa yako lipo.

Hasa hilo kundi unalo shauri lilengwe, ni kundi moja gumu sana; kwa sababu mablimbali; kuna mmoja humu kisha sema "attention" ya wengi katika kundi hilo kwa jambo lolote inadumu kwa masaa tu!
Elewa pia kuwa kundi hili hili ndilo huwa halipigi kura kabisa!

Hata hivyo, nakupongeza sana kwa kuwa na ushauri ambao kwa hali ya kawaida mtu ange dhani hiyo ndiyo njia nzuri ya kuwatia hamasa hawa watu.
 
Sawa aanze hata sasa hivi kupost clip ya dakika 1 mpaka 2. Inatosha kupeleka moto 🤣🤣. Na wasanii wakitoa challenge za nyimbo mpya na yeye acheze, na masuala ya mpira na yeye ashiriki hata kutoa comment mtandaoni.
Ninakubaliana na ushauri wako, lakini hiyo iwe ni kazi ya chama, siyo kazi ya Tundu Lissu.
 
bila michango kwanza sijui kama inawezekana 🐒
LOOooooh!
Naona wewe mwenyewe umelainika kabisa mkuu 'Tlaatlaah' jinsi ulivyo kogwa na mahojiano haya aliyo fanya Tundu Lissu kiasi kwamba ingewezekana ungeungana naye katika mapambano ya kuwaondoa madarakani CCM, au siyo!

Usihangaike kujibu, mezea tu hayo mawazo moyoni mwako.
 
Mimi namkubali sana Odemba wa Star TV mwamba anajua kuhoji maswali yenye mashiko hakupi mda wa kudanganya akikuona unaokoteza majibu anakuchapa lingine.
Hana skills na he is impatient , hana reasoning wala listening skills . Most of his interviews are boring
 
Wengi wetu tunasahau haraka sana....

Mh.Rais alishawahi kupata kusema "nikosoeni mtakavyo" ila MSITUKANE...kwani kwa waafrika matusi si uungwana na heshima ni jambo la kiutu na la lazima[emoji7]

#Nchi Kwanza[emoji7]

#Mh.Rais SSH raia nambari moja[emoji7]
Na katika pumzi hiyo hiyo, udanganyifu na ulaghai ndio yawe halali au siyo?
 
Hamna hoja hapo
20240822_070230.jpg

Unapenda habari za kukufuraisha tu
 
Back
Top Bottom