Rais wetu alisema hayo wakati korona ikiingia na kuwahamasisha watu wafanye kazi bila uoga, waendelee na bunge bila uoga, na mmoja wao au zaidi wameambukizwa nayo.
Alisema hayo wakati wachina na wazungu Ulaya na Marekani, waarabu uarabuni na Afrika kaskazini wanakufa na Korona.
Baada ya kusema hayo muda si mrefu akakimbilia Chato kujificha na kutudharirishia alikimbia Dar na Dodoma baada ya kusema Dar kuna visa vingi zaidi na kujiuliza kwa nini wakati ni yeye alieacha mipaka wazi hasa kwa abiria toka nchi zenye Korona.
Hii imeonyesha Rais wetu ana fikra duni hasa baada ya kuweka uchumi mbele kabla ya Afya bila kujua bila wananchi wenye Afya hakuna uchumi. Rais we tu kaonyesha kuchanganyikiwa toka mwanzo aliposema eti Korona ni mafua tu na hayaui, hajui kuwa ugonjwa huu ni wa kupambana nao kama Ebola la sivyo unaweza kumaliza nchi nzima ikiwamo na yeye mwenyewe.
Nampongeza kwa ugunduzi wake wa ulakini wa mashine za kupima korona, ila sikubaliani na njia alizochukua za kuwasimamisha kazi wakuu wa maabara badala ya kuwataka kufanya uchunguzi kwa nini papai limekuwa na Korona.
Ingawaje anafanya uchunguzi, si sahihi kuhukumu kabla ya uchunguzi, kuwasimamisha kazi ina maana anaona wana itilafu na ulakini katika kazi yao, japokuwa ni yeye aliyefanya juhudi zote za kuwadanganya ni sampuli za watu, hivyo walipima hizo sampuli kama Rais alivyotaka.