Pia unaweza jifukizia kwa kuchanganya yaani unachemsha tangawizi, limao na Vitunguu saumu kimoja una kata nusu aisee kama una vimafua sijui kwisha habari yakeHili jambo la kujifukizia linaweza likatutoa kwenye hili janga ambalo halina kinga.
Nimejaribu kutafiti kuna watu wanakubali na kuna wengine wanakataa.. lakini wengi wanaopinga ni wale wenye viwanda vya madawa.
Ila ukweli ni kwamba ukijifukizia kikohozi na mafua vinapona kabisa..
Kwa wale wanaopenda kujisomea naomba usome kuhusu
1. EUCALYPTUS OIL STEAM
2. EUCALYPTUS LEAVES STEAM
Huu mti ambao unapatikana kwa wingi Tanzania na ni bure , umefanyiwa tafiti nyingi za kisayansi na unatumika kama source ya madawa mengi sana.
Lakini baadhi ya nchi wamekua wakitumia kutibu baadhi ya homa kama za mafua.
Naamini pendekezo la mheshimiwa Rais likipata mwongozo wa watalaam linaweza leta matokeo mazuri.
Tungeomba waziri atangaze kila mtanzania kujifukizia asubuhi na jioni kila siku kwa kuchanganya na huu mti eucalyptus.
Wenye phamarcy mtatuwia radhi kidogo, tupo vitani.View attachment 1427392
Sent using Jamii Forums mobile app
Pia unaweza jifukizia kwa kuchanganya yaani unachemsha tangawizi, limao na Vitunguu saumu kimoja una kata nusu aisee kama una vimafua sijui kwisha habari yake
Asiyejivukiza asitoke nje ya nyumba yake.
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] Acha nikalale mie..
Upo sahihi, tamaa mbaya, hata hivyo utakuja kipindi watu hawataenda kufanya shopping,Utaratibu uendelee kwa kuchukua tahadhari ipi?
Wangefunga mipaka wangezuia muingiliano ya wageni kutoka mataifa ambayo yameathirika kulikua na uwezekano mkubwa kutopata hili janga
Tamaa ya pesa, ndio sababu mpaka sasa inatutesa
Ka Corona haka tunaambiwa tusikaogope, lakini tunaambiwa tuchukue tahadhali. Tunaambiwa tuvae mask, lakini pia tutumie njia za asili. Tuliambiwa tuache ubishi tuwasikilize wataalam na viongozi wetu, lakini leo tumeambiwa takwimu zingine ni za uongo, yani alizo nazo yeye ndio za kweli waliokufa/kufariki ni 10 tu. Tumeambiwa tusikaogope lakini wamefunga vyuo na mashule yote kwa muda usiojulikana. Tunapambana na nani hasa viongozi wetu au Corona?
Tunapambana na Corona, kalipoanza ndio kalikuwa ka Corona sasa ni Corona, tuwasikilize viongozi wetu kwa kutekeleza kila maelekezo tunayopewa.Ka Corona haka tunaambiwa tusikaogope, lakini tunaambiwa tuchukue tahadhali. Tunaambiwa tuvae mask, lakini pia tutumie njia za asili. Tuliambiwa tuache ubishi tuwasikilize wataalam na viongozi wetu, lakini leo tumeambiwa takwimu zingine ni za uongo, yani alizo nazo yeye ndio za kweli waliokufa/kufariki ni 10 tu. Tumeambiwa tusikaogope lakini wamefunga vyuo na mashule yote kwa muda usiojulikana. Tunapambana na nani hasa viongozi wetu au Corona?