Mr. Zero,
Nadhani sasa ni wakati wa rais kusimama kama rais wa nchi katika mambo nyeti kama haya, iweje tetesi za uzushi tunazozisikia kutoka viiweni yawe ndo mawazo ya raisi ? kumekua na uvumi kua oh wazungu wanaleta chanjo yakumaliza waafrika, barakoa zina virusi n.k, kwanini rais wa nchi alalamike ka ma sisi! kama kuna uwezekano wa kuingiza barakoa zenye virusi je tuko salama kama nchi?

ni nani mwenye jukumu la kulinda wananchi na mambo kama hayo!?
Kiukweli raisi ni taasisi kubwa yenye vyombo vya kutosha kupata majibu na kuchukua hatua zinazohitajika, mkemia mkuu wa serikali yupo kwanini tusizipime na kujiridhisha badala ya kujenga hofu kwa wananchi? kama tulizipima kwanini tunaendelea kupokea msaada?
KIUFUPI hotuba nzima ilikua n i raisi kuilaumu serikali, serikali yake mwenyewe..........sijui mwananchi afanye nini
 
Angalia na watu wa kuwaamini mkuu.......huyu haaminiki hata kidogo. Miaka mitano ametupotezea muda na kuharibu nchi ni muda wa kuchukua hatua za kumuondoa sio kumsikiliza na kufuata anachosema
 
Walikuwa na sura zenye huzuni na unyonge sana. Kama si njaa na kuogopa kutekwa wangejiuzuru.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwahiyo makosa ni ya TBS, wamepokea mizigo kutoka nje bila kuipima?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Jana mkuu wetu katutoa kwenye Giza kabisa...Apo ndiyo utaona kua Mh. Acha kupotosha wewe....Kwahiyo yakipata moto 100cc basi unayapoza kwanza alafu ndiyo unajifunika?
 
Lucas philipo,
Hujui kuwa hata maprofesa na madokta hapa nchini, wajinga, washirikina, na washamba wapo?

Kwani huko nje madokta na maprofesa wenye imani kama hizo umewasikia?

Acha u mbechile kudhani wengine ni imbeciles wakati imbecile ni wewe mwenyewe.
 
Kutokana na maelekezo ya jana, nahisi kuna umuhimu tukapata watumishi wa afya wa kutosha hata kwa mkataba ili kukabili upungufu wa watumishi hiki kipindi ambacho tunahangaika kujenga nchi na tukiwa tuna hili janga.

Wahitimu wa kada za afya waliopo akiba waingize kwenye mapambano ili kujiimalisha tusisubiri kujiuliza
 
Kwa kuwa sasa ni rasmi tumetambua kujifukiza kama sehemu ya tiba ya corona, nashauri Wizara ya afya iandae video clip fupifupi kuonyesha miti na mimea ambayo inatumika kujifukiza, na pia je tunajifukiza njia panda au ndani ya Nyumba, pia aina ya kaniki ya kuvaa, nyeusi au nyekundu.

Video clip zirushwe na TV zote nchini na ikibidi ziwepo audio kwa ajili ya redio
 
Hao waliopo wachache kwanza wahakikishiwe usalama wao wawapo kazini.

Vifaa kinga hakuna. Matokeo yake watumishi waliopo na hata hao watakaoajiriwa wote tutawapoteza kwa kuambukizwa Corona.
 
Wazo zuri lakini sidhani kama mzee wa kikombe anasikiliza mtu saa hizi amejichimbia kwao, anaamini katika social distancing lakini haruhusu ifanyike.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…