Papi Chulo, Unajua ni uzembe wa hali ya juu kiongozi mkuu kutuhumu bila kuchukua hatua haraka?

Kuna amri ya kuvaa barakoa ukiingia ofisi za umma, mabenki na sehemu mbalimbali. Sasa kwa vile yeye ndio anavyombo vyote vya uchunguzi kwa nini asiseme MARUFUKU BARAKOA ZA NJE tuu basi ili uchunguzi uendelee?

Kunyamaza kwake wangapi wanapotea wakitumia huku wakisubiri huo uchunguzi?
Halafu acha tabia ya kudhani kukosoa utendaji ni kumchukia Rais na serikali! Hayo ni mawazo ya hovyo sana

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sisi tumeitikia wito wa Rais Magufuli tumeanza kujifukiza
 
Wazo zuri lakini sidhani kama mzee wa kikombe anasikiliza mtu saa hizi amejichimbia kwao, anaamini katika social distancing lakini haruhusu ifanyike.
ndo hapo tutakwama kama hajajiandaa kuimarisha sekta ya afya kwa kuongeza nguvu jeshi ya watumishi wa afya wa kutosha maana waliopo ni wachache mno
 
Nini kazi ya TBS??? Ina maana mzigo ukitoka nje haupimwi ubora kabla ya matumizi?
Sio chuki mkuu ukweli upo wazi kama serikali imeshindwa kazi basi sio kuwaambia watu wavute mvuke [emoji35]
 
Chakaza, Umepindisha mada kiasi kikubwa mno kwa mtu ambaye hajasikiliza unaondoka naye jumla.

1. Hajasema tusivae ila ameweka angalizo kuwa lazima hata sisi tujiridhishe ubora wake. Tena amepongeza wale wanaotengeneza locally, labda kumuongezea hata hizo local zithibitishwa kufaa kwake

Amesema upuliziaji(fumigation) hakuuwi Corona virus. Usipinge haraka watu niwatafuta fursa na wapigaji, swali ni hili dawa zilizopulizwa zinaua virus?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mie nauliza tu,Mkurugenzi wa TBS na TFDA wametumbuliwa? Hizo mask tunazinunua kwenye maduka yaliyo ndani ya Tanzania
Hii ndio hoja ya maana.
Hivi tunakomea kuamini tu kuwa tuletewa msaada au tumenunua nje basi . Swala la ubora tunategemea uchunguzi wa wenzetu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…