#COVID19 Mtazamo, Maoni, Ushauri na Mapendekezo kwa Serikali na Wananchi kuhusu Ugonjwa wa Corona - COVID-19
Habari wakuu!!, covid-19 ni hatari kwa afya zetu, tujitahidi kuzingatia kanuni za afya.
Moja kwa moja kwenye Mada.

Kwa wanachuo tulio kuwa tunategemea boom na tumepanga magetoni (chumba), nakodi zimekata, mtaani hakusomeki (sio wote).

Tuombe Mungu corona iishe turudi chuo maisha yaendelee. Wenye Nyumba hebu kuweni na subira corona ikiisha tutawapa pesa zenu.
 
Hamna cha kusoma hapo, be serious
Nani sasa awe serious kati yangu na ww usietaka kusoma wakati huohuo hujui na unajifanya unajua!

Magu sio wa kubishana naye kwa akili za aina yako! Anajua anachosema na kufanya! Ni msomi mzuri!
 
Za kuambiwa changanya na zako, Hilo suala kihalisia haliwezekani, kimsingi mzee baba kachemsha kashauri pumba.
Hapana, linawezekana! Mvuke unapotoka unskuwa na nyuzi joto 100 lakini unapopanda juu mpaka kukufikia, nyuzi joto zinakuwa zimepungua na hivyo hautaungua!
 
Habari za midaa hii washika dau?

Lengo la uzi huu ni kwa wale waliowahi kuugua corona.Watupe mbinu walizotumia kupambana na janga hili.Ni vyema kujifunza kwa kupitia waliofanikiwa.

Jana nimekua na hofu.Nikiwa kwenye mizunguko yangu.Nikahisi koo linawasha(nikashtuka).Niliporudi home baada ya kula nikachemsha maji ya mchaichai na tangawizi nikanywa nikalala.

Asubuh muwasho siusikii tena ila ni chafya nyingi na mafua.Nimegonga chai ya tangawizi ila nasikia maumivu ya kichwa kwa mbali.

Sijui ni hofu ama lah!Lakini imebidi nitulie home nisitoke isijekuwa teyar nimeshapata.

Kama uliwahi kuugua njoo tupe mrejesho ulipambanaje mkuu.Asante

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wakuu kuna msemo usemao aliyeshiba hamujui mwenye njaa, lakini Rais Magufuli ameonesha kuitupilia mbali msemo huo kwa kusimama na watanzania ambao wengi wao ni masikini kwa kukataa maoni ya baadhi ya wanasiasa wabinafsi kama Zito ambao walitaka raia wafugiwe ndani ilihali wakijua fika maisha Yao ni yakupata leo na kula leo. uzi tahari.
 
Yeye kakimbia kujificha Chato!Halafu anasema si mnaona nimewaita watu kutoka Dar,hivyo msitishike na Corona😅😅😅!Nilitamani kuzimia niliposikia hayo!
Hapa naona alikuwa anajitetea kuwa hajaikimbia Dar kwasababu ya Corona ndio maana akawaalika watu wa Dar!Hivyo tusiwaogope watu wanaotoka Dar kuja mikoani teh teh teh!
 
[emoji848]
IMG-20200423-WA0000.jpeg
 
Matumizi ya masks yamepanda sana,mahitaji ni makubwa mno.Kwa wastani wa kutumia barakoa mbili kwa siku tunahitaji wastani wa barakoa milioni 100 kila siku kwenye nchi yetu yenye wakazi zaidi ya milioni 50.

Viwanda vya "Mwijage" elfu nne vyenye wastani wa cherehani nne vinaweza kutengeneza barakoa 20 kila cherehani mara nne ni barakoa 80 kwa kiwanda kimmoja kwa siku.

Viwanda 4000 vya Mzee sound vitazalisha barakoa milioni 3 na laki mbili kwa siku.
Wakati kiwanda cha CCM kimejikita kutengeneza bendera za chama na masharti ya chama,viwanda vya Mh.Mwijage vinaweza kuleta mchango mkubwa.
 
Ningependa kujikita katika hutaba yake ya 22/4/2020 pale chato kuhusiana na mapambano dhidi ya corona...

Ukiangalia vizr katika hutuba yake ile ilijengeka katika taswila kubwa ya ukosoaji wa juhudi au hatua zilizofanywa na wateule wake..

1. Ukiangalia alimkosoa vikali makonda kuhusu swala la kupulizia dawa katika mji wa dar....

2. Alimkosoa vikali naibu waziri wa afya katika swala la kufukiza ( naibu waziri alitahadhalisha mapema kufukiza hakuwezi kumfanya mtu apone corona)

3. Alimkosoa vikali waziri wa afya katika suala la utoaji takwimu (waziri anasema waliopona 11 wakati walio pona n 100)


Rais alilenga nn katika ukosoaji huo?

Ni kweli hayo waliyoyafanya wateule wa raisi hayoko sahihi?

Katika undelezaji wa waziri UMMY MWALIM wa utoaji wa taarifa ataendelea kuaminika na taarifa zake kwa uma kuhusu mwelekeo wa corona?

Makonda muda huu anakuja na mkakati gani tena baada juhudi za kupambana na coronazake kupingwa kwa nguvu na mteule wake?? Au itabidi atulie tu ajifanye haoni kinachoendelea?

Note. Moyo unamengi ya kusema ila ulimi hauna uwezo wa kunyosha sentensi vzr. Tuvumiliane kwa mwandiko huo!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hili sio kweli, na unajua hivyo. Sayansi haiwezi ikawa ya nchi moja na isiwe na matumizi sehemu nyingine.

Jamii zinatofautiana kutoka nchi moja hadi nyingine, asilimia 99% ya wagonjwa wa COVID-19 kwa Africa ni vijana wa mikoa kuania 15 mpaka 45. Tofauti na wenzetu wa Ulaya na Asia ambao ni 95% ni wazee kuanzia umri wa 65 mpaka 100.

Matibabu yanaweza kuwa tofauti maana vijana wengi wanapona huu ugonjwa bila dawa au matibabu ya aina yoyote.
 
Habari zenu wadau!

Jamani maisha ni magumu sana! Sijui kwa vile wengine tulikuwa tumezoea kukaa tu nakuvuta mshahara mwisho wa mwezi. Sema kweli nilikuwa nafanya kazi kwenye company moja hivi pale Arusha inahusiana utalii lkn kwa sasa hakuna kazi. Nikaamua niwe mjasilia mali aisee ujasilia mali ni mgumu asikwambie mtu. Yaani kwa siku faida unapata 5k au 10k tu.

Naombeni mnipe mbinu mliotumia mpaka mkatoboa kupitia kujiajiri. Sema kweli maiaha siyo shwari huku
 
Kama unapata buku 5 au 10 kipindi hiki cha corona basi hiyo biashara ngumu. Corona ikiisha utameki mpaka laki. Mie nina saloon ya kisasa jumapili nikasema nikae nione biashara maana nilikuwa siwaamini wafanyakazi kuhusu kushuka kwa mapato.

Nimekaa asubuhi mpaka saa 12 jioni wamekuja watu wanne tu kunyoa na mmoja alinyoa ndevu tu. Ilibidi nipunguze vinyozi awe anakuja mmoja tu badala ya watatu

HALI NI MBAYAAA nimeandika kwa herufi kubwa ili kuweka msisitizo
 
Back
Top Bottom