Ningependa kujikita katika hutaba yake ya 22/4/2020 pale chato kuhusiana na mapambano dhidi ya corona...
Ukiangalia vizr katika hutuba yake ile ilijengeka katika taswila kubwa ya ukosoaji wa juhudi au hatua zilizofanywa na wateule wake..
1. Ukiangalia alimkosoa vikali makonda kuhusu swala la kupulizia dawa katika mji wa dar....
2. Alimkosoa vikali naibu waziri wa afya katika swala la kufukiza ( naibu waziri alitahadhalisha mapema kufukiza hakuwezi kumfanya mtu apone corona)
3. Alimkosoa vikali waziri wa afya katika suala la utoaji takwimu (waziri anasema waliopona 11 wakati walio pona n 100)
Rais alilenga nn katika ukosoaji huo?
Ni kweli hayo waliyoyafanya wateule wa raisi hayoko sahihi?
Katika undelezaji wa waziri UMMY MWALIM wa utoaji wa taarifa ataendelea kuaminika na taarifa zake kwa uma kuhusu mwelekeo wa corona?
Makonda muda huu anakuja na mkakati gani tena baada juhudi za kupambana na coronazake kupingwa kwa nguvu na mteule wake?? Au itabidi atulie tu ajifanye haoni kinachoendelea?
Note. Moyo unamengi ya kusema ila ulimi hauna uwezo wa kunyosha sentensi vzr. Tuvumiliane kwa mwandiko huo!
Sent using
Jamii Forums mobile app