Punguza Bp ...mkuu Hii Corona inaweza kukupata. Hata kama afya yako ni Imara na ukafa vilevile.
Tupe mfano imempata nani ambaye sio ngonjwa akaahindwa kujipigania haya kwa kujifukiza, sasa wewe unaishi na ugonjwa Wa presha hatari ukijifukiza si unaweza ondoka na maji
 
Tupe mfano imempata nani ambaye sio ngonjwa akaahindwa kujipigania haya kwa kujifukiza, sasa wewe unaishi na ugonjwa Wa presha hatari ukijifukiza si unaweza ondoka na maji




Watu mbona mnajipa sana matumaini / hata mama Lwakatare alikuwaga anasema hivyo km ww
 
Corona ni ugonjwa usio na dawa, Kuna wanaopona kwa kinga za mwili. Cha muhimu ni kupigana na dalili za mwanzo kama joto kali na homa unakunywa paracetamol. Hali ya hatari ni kushindwa kupumua hapa unahitaji msaada wa daktari.
 
Corona ni ugonjwa usio na dawa, Kuna wanaopona kwa kinga za mwili. Cha muhimu ni kupigana na dalili za mwanzo kama moto kali na homa unakunywa paracetamol. Hali ya hatari ni kushindwa kupumua hapa unahitaji msaada wa daktari.
Kweli kabisa, lakini na sala za toba zisiachwe kwani ugonjwa unakuja kama mwizi Hujui siku wala saa
 
Corona ni ugonjwa usio na dawa, Kuna wanaopona kwa kinga za mwili. Cha muhimu ni kupigana na dalili za mwanzo kama joto kali na homa unakunywa paracetamol. Hali ya hatari ni kushindwa kupumua hapa unahitaji msaada wa daktari.
Leo ulikoamkia...
 
Inawezekana maana watu wanaogopa hospital balaa ndio maana wanapokufa kigogo uanza zake eti hawana takwimu sasa kama MTU alijificha utajuaje
Kila mtu apambane kujenge kinga ya mwili kabla ya kuzidiwa na kuacha mapombe!!
Hospital ni kwenda kumchungulia mtoa roho kama kalala!
 
1.Kutema mate hovyo kila mahali.
Kwa wale watu ambao hamuwezi kupitisha muda wa dakika mbili bila kutema basi wakati huu wa Corona jaribuni kupunguza hiyo tabia.Sina uhakika kama hiyo ni hulka au ugonjwa lakini vyovyote iwavyo badilikeni angalau kwa kipindi hiki cha janga la Corona ila jaribu kufikiria umepata Corona na unatema mate hovyo kwenye ua ambao watoto wanacheza ni watu wangapi utawaambukiza.

2.Kushikashika na kuchezea pua.
Kuna gari nimepanda kutoka Mwanjelwa hadi Uyole kuna mtu anachezea lipua lake tangu nimepanda hadi nashuka imenifanya kumpa konda elfu kumi na kumuachia chenji kwa sababu yake.Wale wote ambao hamuwezi kuondoa mikono yenu kwenye mapua yenu wakati huu wa Corona pumzikeni kwa muda,mtaandelea baada ya hali kutulia na mtaweza kuweka mikono yenu popote mnapotaka katika miili yenu.
 
Jifunze njia za kufanya ukipata korona..usiwe mchoyo share kwa wenzako...

kwanza usipaniki, jiweke kando then jitibu kwa style hii.
 
Kuna nchi za afrika magharibi zilichelewa kuchukua hatua ila wanatoa taarifa zao na cases zao zipo juu pia...Hata nchi za ulaya zilichelewa mbona...Ni kheri utoe takwimu hata kwa kuzibalance kuliko usitoe kabisa;watu wanabweteka.
 
Wasalaam. mosi sio vema Sana kuficha taarifa kama mfanyavyo Ila naamini kua mnazo sababu za msingi na mnamini zinatusaidia Kwa namna moja kupambana na COVID 19, pili ningependa nishauri yafatayo ili kuongeza ufanisi WA kupambana na COVID 19.

1. KUSISITISHA MIKUSANYIKO
Mikusanyiko mingi inayoendelea sio ya lazima mfano ya Bar. Sawa MTU mmoja mmoja anaweza Acha kwenda bar Kwa sasa Ila wote sio wenye utashi Sawa,,hivyo itolewe amri ya kupiga stop Bar..

Pia mikusanyiko ya Ibaada misikiti na MAKANISA isitishwe,,angalia Italy na Saudia ambako ndio HQ ya dini zetu.
Mwisho mikusanyiko masokoni na sehemu za biashara. Hapa hatuwezi kufunga moja Kwa moja shughuli hizi Ila pia hatuwezi kuendelea kuzifanya kana kwamba hakuna athari yoyote ,,basi tuboreshe yafatayo

(a) Tuweke umbali maalumu Kati ya biashara moja na nyingine Kwa biashara zinazo hamishika Kwa urahisi,,mfano magenge ya mboga mboga na natafaka,,,wamachinga wanaopanga bidhaa chini,, hili ni dharura so tunaweza kiuka baadhi ya taratibu kama kuongeza ukubwa WA eneo la biashara,,nazani umbali WA Mita 5 ,Kati ya biashara unatosha.

(b) Kwa biashara zilizo KATIKA wigo maalumu yaan fremu,ipangwe idadi maalumu ya wateja kuingia ndani Kwa wakati mmoja kulingana na ukubwa WA eneo ili iruhusu 1M distance,..IWE ni wajibu WA muhusika na wateja kuzingatia hili ,wateja wanaweza kupanga foleni,,Kwan hata hapo enzi za ujamaa tulipanga foleni kwenye duka la kijiji kupata huduma.

2. KUHUSU kupima wananchi. iwekwe program maalumu ya kupima wakazi wote hasa Kwa mikoa yenye visa vingi ili tujue ukubwa WA tatizo hii itasaidia kuandaa mikakati madhubuti ya kupambana hapo baadae,,tupime Kila mkazi awe na dalili au asiwe na dalili,,na amini wataalamu wapo Sua kila mwaka wanazalisha watu WA biotechnology ni swala la kutangaza nafasi za KAZI na kuwapa semina elekezi KAZI inaanza.

3. CARANTEEN. hivi majuzi ziliibuka tetesi za kuogofya za baadhi ya watu kutiroka CARANTEEN,,,naomba tufanye hivi ili swala la CARANTEEN lisiwe kama adhabu,,

(a) Gharama zote zinazohusika na CARANTEEN hasa chakula igharamiwe na SERIKALI,weka menyu nzuri hapa watu watakaa hata miaka 6 mkitaka,,
(b) KUHUSU watoa huduma za AFYA sehemu za CARANTEEN,,hapa wateuliwe wahudumu maalumu , manesi na madaktari na WATALAMU wengine kadri itakavyo FAA,, wapewe semina elekezi,,,wandaliwe posho maalumu,,na wandaliwe vifaa vya kujikinga,,( hapa mtawapata wengi Hadi wengine watataka kuhonga ili wapate nafasi Natania tu watumish wetu ni waaminifu)

(c) viongezwe vifaa vinavyo hitaji na kuwekwe miundombinu mizuri ili wagonjwa wasiwe bored ,,
NATANGULIZA SHUKRANI NAAMINI YATAFANYIWA KAZI

NB.UMMY MWALIMU Aione kwenye jalada ,na Mniwie radhi Kwa mwandiko mbaya, na makosa ya kisarufi
 
Bora hata huo ushauri ungeutoa kwa Wananchi wenzako, badala ya hiyo Serikali ambayo yote kimsingi imekimbilia mafichoni.
 
Wanao ugua mtaani na kupona ni wengi kuliko wanafika hospital! Kikubwa watu wasigara na waogelea kwenye pombe wana hatari kubwa!
kabisa halafu mtu mmoja hapo.juu anasema kwamba hata uwe na afya isiyo na mgogoro unaenda..yani wewe unywe na kuvuta halaaf utegemee corona itakuacha haulindi afya yako korona ijenge urafiki na wewe?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mapendekezo yenu yote down the drain, shimoni yaani.
Ndio hivyo sasa msubiri kufa na mafua na kuzikwa kwa siri usiku.
Watakaobaki watakuwa wamepata somo la kutosha kwenye aina ya uongozi watakaoutaka.
 
Mkuu unasemaje sasa kuhusu kinga ya mtu mweusi baada ya gonjwa kushika kasi miongoni mwa jamii ya watu weusi huko Marekani na hapa Afrika?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…