Wasalaam. mosi sio vema Sana kuficha taarifa kama mfanyavyo Ila naamini kua mnazo sababu za msingi na mnamini zinatusaidia Kwa namna moja kupambana na COVID 19, pili ningependa nishauri yafatayo ili kuongeza ufanisi WA kupambana na COVID 19.
1. KUSISITISHA MIKUSANYIKO
Mikusanyiko mingi inayoendelea sio ya lazima mfano ya Bar. Sawa MTU mmoja mmoja anaweza Acha kwenda bar Kwa sasa Ila wote sio wenye utashi Sawa,,hivyo itolewe amri ya kupiga stop Bar..
Pia mikusanyiko ya Ibaada misikiti na MAKANISA isitishwe,,angalia Italy na Saudia ambako ndio HQ ya dini zetu.
Mwisho mikusanyiko masokoni na sehemu za biashara. Hapa hatuwezi kufunga moja Kwa moja shughuli hizi Ila pia hatuwezi kuendelea kuzifanya kana kwamba hakuna athari yoyote ,,basi tuboreshe yafatayo
(a) Tuweke umbali maalumu Kati ya biashara moja na nyingine Kwa biashara zinazo hamishika Kwa urahisi,,mfano magenge ya mboga mboga na natafaka,,,wamachinga wanaopanga bidhaa chini,, hili ni dharura so tunaweza kiuka baadhi ya taratibu kama kuongeza ukubwa WA eneo la biashara,,nazani umbali WA Mita 5 ,Kati ya biashara unatosha.
(b) Kwa biashara zilizo KATIKA wigo maalumu yaan fremu,ipangwe idadi maalumu ya wateja kuingia ndani Kwa wakati mmoja kulingana na ukubwa WA eneo ili iruhusu 1M distance,..IWE ni wajibu WA muhusika na wateja kuzingatia hili ,wateja wanaweza kupanga foleni,,Kwan hata hapo enzi za ujamaa tulipanga foleni kwenye duka la kijiji kupata huduma.
2. KUHUSU kupima wananchi. iwekwe program maalumu ya kupima wakazi wote hasa Kwa mikoa yenye visa vingi ili tujue ukubwa WA tatizo hii itasaidia kuandaa mikakati madhubuti ya kupambana hapo baadae,,tupime Kila mkazi awe na dalili au asiwe na dalili,,na amini wataalamu wapo Sua kila mwaka wanazalisha watu WA biotechnology ni swala la kutangaza nafasi za KAZI na kuwapa semina elekezi KAZI inaanza.
3. CARANTEEN. hivi majuzi ziliibuka tetesi za kuogofya za baadhi ya watu kutiroka CARANTEEN,,,naomba tufanye hivi ili swala la CARANTEEN lisiwe kama adhabu,,
(a) Gharama zote zinazohusika na CARANTEEN hasa chakula igharamiwe na SERIKALI,weka menyu nzuri hapa watu watakaa hata miaka 6 mkitaka,,
(b) KUHUSU watoa huduma za AFYA sehemu za CARANTEEN,,hapa wateuliwe wahudumu maalumu , manesi na madaktari na WATALAMU wengine kadri itakavyo FAA,, wapewe semina elekezi,,,wandaliwe posho maalumu,,na wandaliwe vifaa vya kujikinga,,( hapa mtawapata wengi Hadi wengine watataka kuhonga ili wapate nafasi Natania tu watumish wetu ni waaminifu)
(c) viongezwe vifaa vinavyo hitaji na kuwekwe miundombinu mizuri ili wagonjwa wasiwe bored ,,
NATANGULIZA SHUKRANI NAAMINI YATAFANYIWA KAZI
NB.UMMY MWALIMU Aione kwenye jalada ,na Mniwie radhi Kwa mwandiko mbaya, na makosa ya kisarufi