Binafsi nilidhani ni gharama kubwa kumbe ni hela ambayo hata watu binafsi wanaweza kununua hata 20 lakini serikali inashindwa.

Wamenunua ndege kwa gharama kubwa wameipaki moja pale airport ili kila anayepita awe anaiona
Tuliyoshangaa tupo wengi bhasi!
Millioni 56 ni pesa ndogo sana kwa serikali ajabu tuna upungufu mkubwa sana wa ventilator.

Hatupo serious! Hili janga limetonyesha na limetufunza mengi kwa wenye kuona na kutafakari.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tuliyoshangaa tupo wengi bhasi!
Millioni 56 ni pesa ndogo sana kwa serikali ajabu tuna upungufu mkubwa sana wa ventilator.

Hatupo serious! Hili janga limetonyesha na limetufunza mengi kwa wenye kuona na kutafakari.
maana yake hata sasa ukikata pumzi,hakuna pa kuwekwa unasubiri kifo tu. hapa nimeelewa kwa nini TISS wamemkimbiza Chattle
 
Watanzania wote ghafla wanachukuliwa kama watoto hata na watu kama Makonda, hatuna haki ya hotuba (free speech), wala haki ya kusema ukweli.

Lazima tujipange na wabunge wetu tupiganie haki zetu za kuwa huru kimawazo na kutoa maoni muhimu serikalini.

Bila hivyo tutaona nchi yetu inageuka kuwa ya udikteta kama siyo tayari iko hivyo, na hilo litasababisha machafuko ya kisiasa mwishowe.
 
Unakumbuka ulivyo msaliti dada Mange kwa uwoga wako.
Maybe ungekuwa huru now.
 
Habari za jioni. Nimemsikiliza huyu mama kwa makini, siamini kamaanaweza kutoa clip ya kupotosha. Ninaco amini tiba ni kwamba njia hii inaweza kukusaidia wewe au ndugu yako. #Tusipuuze


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tayari ishapiga honi.........

Isahaanza kuchukua momentum
Mamamae am sure huko Dodoma jioni hii watakuwa wanajamba jamba sana. Umri na yale magonjwa yaisiyo na dawa yalivyojaa mle, utawakula kama simba
 
Ndugu zangu, Ugonjwa ulivyoripotiwa huko Kenya tulisema mengi mno.Nilikuwa Arusha siku hiyo.Nilishuhudia mbwembwe nyingi kwa wakazi wa Arusha.Mask ,sanitiser na groves.
Baadaye akatangazwa mgonjwa wa kwanza katika nchi yetu. Mtu mmoja aliandika katika social network kuwa " kipele kimempata mwenye kucha".
Leo waziri Mkuu katangaza maambukizi kufikia 480. Idadi inakimbia mno, nadhani tuko juu katika East Africa. Sio vizuri kwetu, na kwa majirani zetu pia.Baadae ninahisi tutatengwa sisi.Itakuwa mbaya mno kwetu.
Kuna viongozi wana muono tofauti .Mfano niliona video ikimuonyesha Dc wa Iringa akisema kuwa watengeni watu wa Dar es salaam. Nilimpenda mno.kusema kweli sasa hivi ukienda mikoani, umetoka Dar unatisha.
Sasa tuangalie Dar es salaam, jiji letu lililosheheni watu wa kila namna Wanaojua sana na wajanja mno.Toka Rc wa Dar es salaam atuhimize kuvaa barakoa, kuna vichekesho vingi mno kila mahali.Katika daladala waweza kukuta zaidi wa watu 10 hawajavaa barakoa.Nenda mtaa wa Kongo na masokoni, kwenye masoko/magulio ya wiki, hakuna anayejali. Sio mnunuzi wala muuzaji.Nenda Mbagala kaangalie ule msongamano wa wafanyabiashara na wanunuzi. Ninachokiona mbele kabisa kinatisha.
Raisi , kwa kujua hali zetu, hapendi lock down wala kufunga mikoa. Lakini kwa dharau zetu, kwa kuwa hatuwezi na hatutaki kufikiri tutakwisha.
Tufanyeje?- Askari watumike kukamata watu wanaozagaa mitaani bila barakoa.Wakenya na Wahindi wamepigwa mpaka wameelewa. Magari ya abiria yasimamishwe katika maeneo yoyote , askari waangalie wale wanaopuuza kuvaa barakoa, wawashushe wawatandike, pamoja na kondakta aliyewapakia.
Viongozi wetu hawaendi Kongo Street wala Mbagala. Hivyo basi watume watu kuangalia hali halisi.Hizo sehemu hatarishi zifungwe.Nina mengi ya kushauri , lakini nimshauri nani?
Stay home, stay safe

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ndugu wa JF;
Bila shaka sote tunatambua ukubwa janga hili la COVID-19
Niende kwenye mada niliyokusudia iwafikie Watanzania wenzangu waweze kujiepusha. Tumeelezwa jinsi virus vya Corona vinavyosambaa. Pamoja na njia zote hizo lakini pia kasi ya maambukizi yamekuwa makubwa sana sehemu za maofisi kutokana na matumizi ya AC iwe ndani ya magari au kwenye majengo yetu.
Utafiti huu nimeufanya si kwa kutembelea maofisi hayo la ni kutokana na uzoefu. Mtu mwenye ugonjwa wa kifua kikuu huweza kuambukiza wengine kwa kasi sana ikiwa atakuwa katika ofisi zenye AC kuliko akiwa kwenye ofisi isiyo na AC.
Boss anatoka nyumbani na gari lake full AC anafika ofisini full AC lakini ndani ya muda mfupi Boss anakutwa amefariki ghafla. Lazima watu wajiulize kwanini.
Nahitimisha kwa kusisitiza kuwa AC ni msambazaji mkubwa wa Coronavirus
 

Ni kweli. AC inaweza kufyonza virusi na kuvitawanya jengo zima/gari/kwenye basi iwapo kuna mfanyakazi/abiria muathirika
 
Niliona case kama hii China. Familia ziliambukizwa kupitia AC.But how ?
 
Sema Corona virus- conducive inviroment yake ni hali ya ubaridi kama ilivyo mbu kwa hali ya joto kama Dar, Kyela Mbeya nk. Huwezi kumkuta mbu Lushoto
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…