#COVID19 Mtazamo, Maoni, Ushauri na Mapendekezo kwa Serikali na Wananchi kuhusu Ugonjwa wa Corona - COVID-19
Huu ni wito mahususi kwa NHIF.

Tunaona dunia nzima serikali na taasisi binafsi zinatenga ruzuku kupambana na corona katika kila hali.

Sisi wanachama wenu ambao tunachangia kwenye mishahara na namna zingine mnatuachaje? Kwanini msifikirie kutuwezesha vifaa vya kujikinga na corona kama vile sanitaiza na barakoa?

Kiwekwe kiwango cha kuwezesha na aina ya wawezeshwaji. Kwa mfano mnaweza kuwawezesha wanachama wachangiaji ili kumudu gharama. Mnaweza kuweka kiwango cha kupata lita 5 ya sanitaiza na barakoa kadhaa ambazo ni non-disposable.

Wakingeni sasa wanachama badala ya kusubiri aumwe na kulazwa ambapo mtalipa gharama kubwa zaidi.
 
Kuna kuchanganyikiwa hapa na sikama watakavyo, tuwaombee hekima kwa Mungu maana huu ni mwanzo tu, tutarajie magumu zaidi.
Ni kama mmeamua kutuaacha wananchi kila mtu ajihangaikie kivyake, kama chama tu tuna uwezo wa kugawa Tshirt, kofia, khanga, vipeperushi, mabango na posho nchi nzima kipindi cha kampeni.. Serikali inashindwa ku-waorganize wafanyabiashara wakubwa na wadau wengine wa afya kushirikiana na serikali tukapata Barakoa bure kabisa kwa kila mwananchi? kama mmeshindwa kwa nini msitoe msamaha wa kodi kwa hizi bidhaa ili zipatikane kirahisi kipindi hiki na kwa bei nafuu angalau ya tsh 500? Angalia sasa watu wanakimbilia kusafiri kurudi kijijini bila kupimwa nyie serikali ni kama hampo, siku si nyingi huko vijijini nako ugonjwa unaenda kutapakaa.. Jamani hivi nini kazi yenu?

Hao migambo na polisi mnaoweka kukamata wasiovaa Barakoa ni wa nini wakati upatikanaji wake bado ni kizungumkuti? Gawa kwa watu halafu wakamate wasipovaa, sio kama mnavyotaka kufanya hivi sasa..,Katibu mkuu wangu bashiru saidia kuwashauri hawa watu maana mpaka sasa raia hawajui wafuate lipi,ummy alishawahi kusema wanaotakiwa kuvaa barakoa ni wale waliopatwa na maambukizi tu juzi makonda kasema watu wavae barakoa hata za vitambaa vya khanga, naibu waziri wa afya akatoa kauli bungeni kwamba kuna barakoa maalum kwa ajili ya kuzuia maambukizi ya corona sio kuvaa yoyote watu hawajui washike lipi?

Kuna video na picha zinatrend mitandaoni zikionesha watu wasio na nia njema wamekusanya barakoa zilizotupwa wanazifua, wanazipiga pasi halafu wanaziuza tena kwa watu jambo ambalo ni hatari kwa afya, wapo wanaovaa barakoa zilizotengenezwa kwa material ya sidiria za mitumba ambapo pia kiafya sio rafiki..Mko wapi serikali MKO KIMYA😎, mnawezaje kukaa siku mbili hadi tatu bila kutoa maelekezo yoyote kipindi hiki,taarifa hazitolewi, tetesi zinaachwa zisambae na kuleta taharuki🙃🙃

Mmetuacha tujiiendee kama meli isiyokuwa na nahodha, mnajua kwa nini tunawahudumia kila kitu bure na familia zenu kwa malipo ya kodi zetu? Hapa mnacheza sandakarawena maisha yetu

viongozi wetu kuweni serious na maisha yetu, ni kama mmewatelekeza watanzania na sasa kila mmoja anapambana kivyake..., angalieni hapo kenya tu serikali inagawa hivi vifaa vyote bure, kwa nini sisi? Jamani 😭😭
 
Serikali ipunguze Kodi ,pia itoe msaada kwa Kila Kaya ili kunusulu athari kubwa sambamba na kupunguza Bei ya bidhaa muhimu
 
Kuwashauri ni kupoteza muda hata hao praise team wa ccm ni kwa ajili ya kutafuta madaraka tu....kwani kuna kiongozi wa ccm anashaulika awamu hii?
 
Ni kama mmeamua kutuaacha wananchi kila mtu ajihangaikie kivyake, kama chama tu tuna uwezo wa kugawa Tshirt, kofia, khanga, vipeperushi, mabango na posho nchi nzima kipindi cha kampeni. Serikali inashindwa ku-waorganize wafanyabiashara wakubwa na wadau wengine wa afya kushirikiana na serikali tukapata Barakoa bure kabisa kwa kila mwananchi?

Kama mmeshindwa kwa nini msitoe msamaha wa kodi kwa hizi bidhaa ili zipatikane kirahisi kipindi hiki na kwa bei nafuu angalau ya tsh 500? Angalia sasa watu wanakimbilia kusafiri kurudi kijijini bila kupimwa nyie serikali ni kama hampo, siku si nyingi huko vijijini nako ugonjwa unaenda kutapakaa.. Jamani hivi nini kazi yenu?

Hao migambo na polisi mnaoweka kukamata wasiovaa Barakoa ni wa nini wakati upatikanaji wake bado ni kizungumkuti? Gawa kwa watu halafu wakamate wasipovaa, sio kama mnavyotaka kufanya hivi sasa.

Katibu mkuu wangu bashiru saidia kuwashauri hawa watu maana mpaka sasa raia hawajui wafuate lipi Ummy alishawahi kusema wanaotakiwa kuvaa barakoa ni wale waliopatwa na maambukizi tu juzi makonda kasema watu wavae barakoa hata za vitambaa vya khanga, naibu waziri wa afya akatoa kauli bungeni kwamba kuna barakoa maalum kwa ajili ya kuzuia maambukizi ya corona sio kuvaa yoyote watu hawajui washike lipi?

Kuna video na picha zinatrend mitandaoni zikionesha watu wasio na nia njema wamekusanya barakoa zilizotupwa wanazifua, wanazipiga pasi halafu wanaziuza tena kwa watu jambo ambalo ni hatari kwa afya, wapo wanaovaa barakoa zilizotengenezwa kwa material ya sidiria za mitumba ambapo pia kiafya sio rafiki.

Mko wapi serikali MKO KIMYA😎, mnawezaje kukaa siku mbili hadi tatu bila kutoa maelekezo yoyote kipindi hiki,taarifa hazitolewi, tetesi zinaachwa zisambae na kuleta taharuki[emoji854][emoji854]

Mmetuacha tujiiendee kama meli isiyokuwa na nahodha, mnajua kwa nini tunawahudumia kila kitu bure na familia zenu kwa malipo ya kodi zetu? Hapa mnacheza sandakarawena maisha yetu.

Viongozi wetu kuweni serious na maisha yetu, ni kama mmewatelekeza watanzania na sasa kila mmoja anapambana kivyake..., angalieni hapo kenya tu serikali inagawa hivi vifaa vyote bure, kwa nini sisi? Jamani [emoji24][emoji24]
Amekimbia kwenda kujificha akadhani kuwa corona inapita anashangaaa tu inapaa ikimtafuta huko aliko, mwambieni atoke mafichoni huko

Sent using Jamii Forums mobile app
 
IMG_5243.JPG
 
Raisi Magufuli, Wakati hauko upande wako yafuatayo ni mapendekezo ya Kizalendo kabisa natoa, kama nilivyotoa mwanzoni kabisa mwa janga hili lilipoanza, Nilipendekeza Tuzuie watu kutoka nje wasiingie nchini, kwa maana mipaka yote ya nchi ifungwe (isipokuwa kwa situation maalum za. mizigo kuingia na kutoka)

hatuna jinsi sasa ni muda wa maamuzi magumu.

Situation tuliyo nayo ni ngumu kuliko hata wakati wa vita ya Kagera, ni mgumu kuliko hata harakati za kudai uhuru, WAKATI HUU TULIO NAO NI TISHIO LA, UWEPO WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA NA WATU WAKE

1. Kama unaweza kuilisha dar, Arusha, Mwanza na Miji yetu mikubwa piga lockdown yote nyumba kwa nyumba, Kama huwezi basi Piga Lockdowndown miji hiyo kwa level ya kata, siyo nyumba kwa nyumba, aliyeko Mwenge asiende kinondoni, aliyeko Kinondoni asiende Posta, masoko ya chakula yawe wazi, Hospitali ziwe wazi, Pharmacy ziwe wazi na watu watoke mmoja mmoja kwa ajili ya essential goods kama vile kununua chakula na dawa. Hakikisha unaplan vizuri watu hawafi kwa njaa, Au let say kw mfano wenye malaria, wenye kuhitaji dawa pharmacy, au wajawazito wenye kuhitaji kujifungua wakajikuta wanazuiwa kutembea. Mtihani upo kwenye watu kula Hapa umiza kichwa sana

2. Kopa watumishi wa umma kwa muda wa miezi miwili, Kata mishahara Ya watumishi wa Umma wenye kipato cha milioni moja kwenda juu kata 50%, wenye kipato cha laki tano kuja chini kata 10%. Hizi pesa ziwe deni la ndani ambalo serikali itakuja kulipa siku moja. Hizi pesa zitumike kununulia Chakula na Kukigawa bure kwa wananchi.

5. Ndani ya mikoa, kwenye mikoa ambayo haijaathiriwa sana, Funga nchi kwa level ya wilaya, mtu asitoke wilaya moja kwenda wilaya myingine.

6. Funga nchi yote kwa level ya mkoa, Safari zote za mikoa zife

8. Chagua nyumba kadhaa kila kata za miji ya Dar, Arusha, Mwanza na ile ambayo inaonyesha dalili za kuwa hardly hit ziwe supply point (maghala) kwenye kata hizo

7. Rasilimali za Jeshi la wananchi kama vile magari ya kijeshi zitumike kusambaza bidhaa muhimu nchi nzima, kwenye masoko na kwenye supply point katika kila kata, na kila Mwenye usafiri wa gari katika kila kata awe identified ili awe distributor wa essential goods katika kata yake, awezeshwe kwa mafuta

8. Tumia mtandao ulionao, Matawi ya CCM, Viongozi wa nyumba kumikumi, Misikiti ya maeneo, Makanisa, Vituo vya polisi, ofisi za serikali za mitaa, watendaji wa kata etc Hapa pia uwe makini isije ikaonekana misaada inakuja kwa misingi ya udini, uchama n. k

9. Challenge kubwa ni wale watu wasio na makazi maalum, ambao hula magengeni, ambao hawajui kupika, ambao hawana nyenzo za kupika, Hapa inabidi uumize kichwa kwelikweli maana ukikosea hapa watu watavamia nyumba nyingine kupora chakula. Hapa unaweza kutumia shule za msingi na sekondari zilizofungwa kuwaweka hawa na kuwasaidia kwa chakula.

10. Tulipeleka vijana wetu JKT siyo wakapige kwata, bali kwenye wakati kama huu tuwaite on duty watekeleze duty kama za kusimamia order kwenye kipindi kama hiki, kwa hiyo hawa ambao ni reserve army waitwe wasaidie kuimplement lockdown hizo nilizopendekeza, miongoni mwa vijana hawa na wanajeshi na volunteers wawe assigned duty ya kupita katika nyumba za mitaa waliyopangiwa kuchukua data za watu kama vile temperature, kujua kama kuna wagonjwa, hali ya chakula cha wananchi, vifo ndani ya majumba, kuchukua data zao na kuziwasilisha panapohusika kwa haraka sana

11. Wale watakaosimamia lockdown waelimishwe sana wawe na commonsense, kwa mfano kuna watu watataka kwenda hospitali, kuna wajawazito wanataka kujifungua n. k, wasije wakaanza kutumia nguvu dhidi yao badala ya kutambua kuwa huduma maalum kwa watu hao haziepukiki

12. Usizuie teksi, bodaboda wala bajaji zitakazokuwa zinabeba watu kwa ajili ya huduma za msingi kama kupeleka watu hospitali

13. Kila atakayetoka mtaani kwa ajili ya kupata essential goods na service ya dharura lazima awe na barakoa.

14. Maduka yetu yale ya kawaida mitaani yenye kuuza bidhaa za chakula na mahitaji mengine ya msingi kama mafuta ya taa, kupikia kwenye kila kata iliyo kwenye lockdown yasifungwe, yale mengine yanayouza bidhaa zisizo za chakula kama vile nguo, vipodozi, vilevi etc yafungwe

15. Challenge nyingine ni vifo vitakavyotokea majumbani, vifo vya Corona au visivyo vya Corona, Mazishi yataendeshwaje?, Kuchelewa kuwa na muongozo katika suala hili kunaweza kusababisha mrundikano wa miili majumbani kama huko Ecuodor na hali ikawa mbaya miili ikichelewa kuzikwa. Yachimbwe makabuli makubwa ya halaiki sehemu zitakazochaguliwa ambapo serikali itazika, Kama logistic zitakuwa ngumu kwa serikali kufika kila sehemu kwa wakati basi kila kata itenge eneo lake la mazishi ya watu wengi kwa wakati mmoja

Mzee, lengo la lockdown, ni kulocalize cases zilipo kirahisi na kuziidentify maana baada ya muda fulani wataonyesha dalili, inalenga kuzuia maambukizi kusambaa na pia kusaidia mfumo wa afya usicollapse kwa kuzidiwa na new cases za kiwango kikubwa

Mzee Ulikosea kutofunga mipaka hapo awali kwa kuhofia uchumi(Kama alivyosema Polepole), Sasa Uliacha kuuanika, leo tunautwanga mbichi.
Wahenga hawakuwa Wajinga kusema heri kinga kuliko tiba!
 
Habari watanzania wenzangu tuendelee kumuomga mungu atuepushie mbali janga hili la corona.......
.
.
Mimi kama Mtanzania naomba niishauri serikali yangu pendwa nikiwa na nia njema kabisa ya kutusaidia watanzania wote kiujumla naamini serikali ikiamua itaweza,,,,
.
.
Mawazo yangu serikali ingeongeza usambazaji wa vifaaa na vipimo katika vituo vya afya yani nikimaanisha iwe rahisi upimaji wa corona km mgonjwa wa HIV anavyopimwa ...yaani upimaji uwe katika vituo vyetu vya afya likiwezekana hilo serikali itengeneze mfumo huu

.
.
serikali ifanye lockdown kwa wananchi wote then itoe wataalamu au wahitimu wa masuala ya afya wapewe semina then wapite kila kaya kama ilivyokuwa kwenye sensa ya watu na makazi pia muda ambao watu wakiwa majumbani kwao halmashauri na serikali za mitaaa zinapuliza dawa mitaani maofisini na kwenye usafiri na sehemu nyeti zote...

Baada ya vipimo majibu yakitolewa watu waliosafe wapatiwe kadi maalumu kama zile za kura, au vile vya wamachinga au ile kadi ya manjano baada ya wananchi kupewa hizo kadi ina maana wapo salama waruhusiwe waendelee na shughuli za kila siku wakiwa na kadi zao hizo zinazowakilisha usalama wa raia na yule yoyote ambaye ataingia mtaani bila ya kuwa na kadi hyo ina maana amevunja sheria itabidi ashughulikiwe ipasavyo pia ulinzi uboreshwe tuna askari wa kutosha hakuna kinachoshindikana

Naamini serikali inaweza sana kwa sababu ikipigwa lockdownrahabu kama nchi nyingine gharama na uchumi wetu utayumba kwa kiasi kikubwa sana

TUJIANGALIE

NI MAWAZO YANGU TU KWA SERIKALI IF MTU UKIONA NI USEFUL UNAWEZA KUPELEKA USHAURI HUU MBELE ZAIDI ILI UWEZE KUFIKIA WIZARA HUSIKA
 
Raisi Magufuli, Wakati hauko upande wako yafuatayo ni mapendekezo ya Kizalendo kabisa natoa, kama nilivyotoa mwanzoni kabisa mwa janga hili lilipoanza, Nilipendekeza Tuzuie watu kutoka nje wasiingie nchini, kwa maana mipaka yote ya nchi ifungwe (isipokuwa kwa situation maalum za. mizigo kuingia na kutoka)

hatuna jinsi sasa ni muda wa maamuzi magumu.

Situation tuliyo nayo ni ngumu kuliko hata wakati wa vita ya Kagera, ni mgumu kuliko hata harakati za kudai uhuru, WAKATI HUU TULIO NAO NI TISHIO LA, UWEPO WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA NA WATU WAKE

1. Kama unaweza kuilisha dar, Arusha, Mwanza na Miji yetu mikubwa piga lockdown yote nyumba kwa nyumba, Kama huwezi basi Piga Lockdowndown miji hiyo kwa level ya kata, siyo nyumba kwa nyumba, aliyeko Mwenge asiende kinondoni, aliyeko Kinondoni asiende Posta, masoko ya chakula yawe wazi, Hospitali ziwe wazi, watu watoke mmoja mmoja kwa ajili ya essential goods. Hakikisha unaplan vizuri watu hawafi kwa njaa, Mtihani upo kwenye watu kula Hapa umiza kichwa sana

2. Kopa watumishi wa umma kwa muda wa miezi miwili, Kata mishahara Ya watumishi wa Umma wenye kipato cha milioni moja kwenda juu kata 50%, wenye kipato cha laki tano kuja chini kata 10%. Hizi pesa ziwe deni la ndani ambalo serikali itakuja kulipa siku moja. Hizi pesa zitumike kununulia Chakula na Kukigawa bure kwa wananchi.

5. Ndani ya mikoa, kwenye mikoa ambayo haijaathiriwa sana, Funga nchi kwa level ya wilaya, mtu asitoke wilaya moja kwenda wilaya myingine.

6. Funga nchi yote kwa level ya mkoa, Safari zote za mikoa zife

8. Chagua nyumba kadhaa kila kata za miji ya Dar, Arusha, Mwanza na ile ambayo inaonyesha dalili za kuwa hardly hit

7. Rasilimali za Jeshi la wananchi kama vile magari ya kijeshi zitumike kusambaza bidhaa muhimu nchi nzima, kwenye masoko na kwenye supply point katika kila kata, na kila Mwenye usafiri wa gari katika kila kata awe identified ili awe supplier wa essential goods katika kata yake, awezeshwe kwa mafuta

9. Tumia mtandao ulionao, Matawi ya CCM, Viongozi wa nyumba kumikumi, Misikiti ya maeneo, Makanisa, Vituo vya polisi, Hapa pia uwe makini isije ikaonekana misaada inakuja kwa misingi ya udini, uchama n. k

9. Challenge kubwa ni wale watu wasio na makazi maalum, ambao hula magengeni, ambao hawajui kupika, ambao hawana nyenzo za kupika, Hapa inabidi uumize kichwa kwelikweli maana ukikosea hapa watu watavamia nyumba nyingine kupora chakula. Hapa unaweza kutumia shule za msingi na sekondari zilizofungwa kuwaweka hawa na kuwasaidia kwa chakula.

10. Tulipeleka vijana wetu JKT siyo wakapige kwata, bali kwenye wakati kama huu tuwaite on duty watekeleze duty kama za kusimamia order kwenye kipindi kama hiki, kwa hiyo hawa ambao ni reserve army waitwe wasaidie kuimplement lockdown hizo nilizopendekeza

Mzee Ulikosea kutofunga mipaka hapo awali kwa kuhofia uchumi(Kama alivyosema Polepole), Sasa Uliacha kuuanika, leo tunautwanga mbichi.
Wahenga hawakuwa Wajinga kusema heri kinga kuliko tiba!
Mimi ukinishauri ndo umepoteza kabisa,yaani unataka niweke lockdown usifanye kazi eee? Hiiiiii nasema sipangiwi,watanzania chapeni kazi
 
Back
Top Bottom