#COVID19 Mtazamo, Maoni, Ushauri na Mapendekezo kwa Serikali na Wananchi kuhusu Ugonjwa wa Corona - COVID-19
Pamoja na kutotangazwa rasmi kwa sababu za kifo cha Mh.Ndasa,maelezo ya watu wake wa karibu ikiwemo Ezekiel Kimwaga yanaonyesha alipatwa na changamoto ya kupumua. Zaidi pia spika amewahi kutangaza kuhusu mbunge kupatwa na maambukizi ya corona.

Kwa sababu hizo ukizingatia kusambaa kwa kasi kwa maambukizi ya corona,hamuoni haja ya kuahirisha bunge na kujipiga karantini? Mbunge Mh.Nkamia ametoa maoni kama haya ili kunusuru afya ya wabunge na kudhibiti maambukizi. Ni vyema mkachukua hatua.

Tumesikia kuwa mwezi May mmepanga kuitisha kamati za bunge kwa kuita idara mbalimbali za serikali kuja kujibu repoti za Mkaguzi Mkuu-CAG. Huu ni wakati wa kutangaza kufutwa kwa vikao hivyo vya kamati.

Maisha ya watu ni muhimu sana kuliko vikao hivyo.


Screenshot_20200430-052204_Chrome.jpg
 
Hali si shwari huku vijijini, raia wanalalamika kusikia ongezeko la visa vya corona. (Kumbe Rais alikuwa sahihi kusema tusitishane). Wanasema ugonjwa huu umeletwa na Rais. Wanauliza mbona haukutokea hapo kabla? (Waelimishwe).

Wanadai Rais kwasababishia maisha magumu kwa kupandisha bei za bidhaa na sasa ameleta corona.

Wanadai kuwa hawatampa kura na wengine hawataenda kupiga kura. Kwa hiyo tutegememee idadi ndogo kabisa ya wapiga kura kuwahi kutokea baada ya mfumo wa vyama vingi.

Tujikinge na Corona, hata Kim Jong Un amejificha Corona (Inasemekana mwanzoni alitoa order kila anaepatikana na corona ale shaba)
Screenshot_20200430-065133.png


Mlioko Dar Jijini, hii taarifa ina ukweli wowote?
94701930_671099903685704_2719308434078957568_n.jpg
 
Kama kupatwa kwa Dunia kule Mwakaleli Mbeya walimshukuru Magufuli na kumwomba awapelekee tena mnashangaa nini hapa?

Kama wengine wasomi kabisa wakipata ajali wanamshukuru Magufuli unategemea wanakijiji hawa wanajua nini?

Korosho zilivyopanda bei CCM walitumia mwanya huo kuwaaminisha wananchi kuwa ni Magufuli kapandisha bei, na hawakuwaambia ukweli kuwa huu ni upepo wa soko la dunia.

Zilipoporomoka bei hizo korosho CCM hawakuwaambia wananchi kuwa huu ni upepo tu wa soko la dunia
 
Madaraka matamu.

Kama bado unang'ang'ania kazi ambayo umesusa huifanyi, kwa nini usishtakiwe kwa uhujumu uchumi? Mtu yeyote anayetaka aeleweke na kuaminika hawezi kufanya mchezo huo mchafu wa kususa wakati wa vita. Ni mpiganaji gani hataki kukosolewa na kuelekezwa pale anapoona amekosea? Huyu si msaliti huyu na hastahili hata kuwa huru uraiani na sembuse kwenye msitari wa mbele?

Hawatufai hawa. wanatakiwa waondolewe na wakae mbali na uwanja maana wataendelea kutusaliti kwa akili zao finyu wakidhani wanamkomoa mkuu wao kumbe wanatuangamiza. wengine nje ya sanduku wapo wengi sana wenye nia na uwezo wa kuenda naye. Pengine hawa wameshakomaa katika mfumo taralila . Sasa hawezi kuwakunja ndiyo sababu wanagangamala.

Anatakiwa aweke watu wapyakabisa ambao hawajafanya kwenye taralila.
 
Tabby kwanini umetoa avatar Picha yako tuliyokuzoea ya yule mwanamama? Halafu ulipoteaga kipindi flani hapa kati

Honestly Kiongozi, nina wasi wasi account yangu ilikuwa hacked.!. Sikumbuki kuweka avatar hapa. Tena ya mwana mama!.Nitaomba mods wanionyeshe hicho picha.

Mkuu nilikwenda retreat mara moja sasa nimerudi! 😁 😁 😁 😁 😁
 
Kama wanazengo wanaelewa hivyo acha waelewe tutafanyaje sasa Ila wambie tu

1.waoshe mikono kwa maji yenye kutiririka na sabuni

2. Kama hawana jambo la msingi wakae nyumbani waepuke misongamano

3.wavae barakoa si lazima wakanunue dukani wanaweza kata hats khanga zao wakakunja Mara mbili wakajifunika pua na mdomo waonyeshe na mfano
4.kama wanaweza jikukiza wambie wajifukize kwa majani ya mpera, mwarobaini, mwembe wajivukize kwa mfumo wa nyungu wanajua

CORONA NOMA TUABARISHANE
 
Mbona hujashauri serikali kusitisha malipo ya mikopo ya nje pamoja na matumizi ya fedha kwenye miradi inayoendelea?

Ushauri wangu ni kuisitisha miradi yote na kujihami kwa kuweka pesa zote za nchi kwenye mfuko wa tahadhari. Mambo yakirejea normal tutaendelea na ujenzi.
Tupe mfano halisia hapo nyumbani kwako umesitisha nini kwa ajili ya kukabiliana janga la COVID-19?
 
Trust None,
Naunga mkono hoja maana jamaa yule amelaaniwa ndo maana tangu 2015-2020 Tanzania imekuwa ikikumbwa na majanga tu.

Sasa naona MUNGU ameikasirikia dunia kwa kushindwa kumuondoa mwanaharamu yule.
Lakini sijamtaja mtu hapo hivyo mboga mboga msihamaki
 
Wakuu mu hali gani?

Hili wazo halijanijia leo wala juzi. Na halijaanza baada ya kuanza kuwapoteza wabunge wetu 2 waliotutoka kwa magonjwa mbalimbali ikiwemo pressure.

Ila sasa baada ya hali kuwa si shwari hapa nchini na ulimwengu kiujumla kuhusu hili janga la COVID 19 naendelea kujiuliza kuendelea kwa vikao vya bunge Tanzania tafsiri yake haswa ni nini?

Kwanini wasisitishe kabisa au kufanya online meetings?
 
Tafsiri yake jiwe hana akili timamu. Anahatarisha cabinet yake na mhimili wote wa bunge.
 
Waache visingizio wapige kazi, kazi ni msingi wa maendeleo.

Tunategemea bunge likamilishe wajibu wake wakupitisha bajeti ya serikali, ku-lockdown bunge NEVER.
Kwanza wamepona zaidi ya watu 100, waliokufa ni 16 tu, kuna magonjwa hatarishi zaidi ya hili.
 
Back
Top Bottom