Hivi sasa watu wengi wameacha kuvaa barakoa, wanashikana miili na wachache wanaweka maji ya kuosha mikono. Harakati za jiji zimerudi kama ilivyokuwa mwaka jana na hii ni baada ya kusikia kauli za viongozi zikiashiria hakuna maambukizi mapya wala vifo. Tanzania tumefanikiwa kuishinda Corona ndani ya muda mfupi sana, hii ni rekodi nzuri na inabidi tuwapongeze viongozi wetu. Nikiangalia mitaani kwangu watu wameisahau Corona ndani ya siku chache na maisha yamerudi kama zamani.
Swali, nani ametangaza kuwa Corona imekwisha?