Mtu huyu akisimama na mgombea wa CCM mwaka 2025, ni lazima CCM tuangukie pua

Hapana mkuu, sikumpa Like tu peke ake kama ulivyoandika hapa. Nimemjibu hoja yake vizuri, na bila shaka kaelewa ndo maana hakurudi tena. Soma post namb #31 utaona nlichoandika. Na ikiwa utairuhusu akili yako kuwa huru kuchanganua kile nlichoandika basi utaelewa nlichomaanisha. Ila kama utasoma huku umebeba hisia ya uchama ndan ya akili na moyo wako, basi itakuwa ngumu kukubaliana na kile nlichoandika. Just go back to the post number #31, read afu uje na mtizamo wako.
 
Ni yapi hasa "haya mengine"?
Soma thread yangu kwa kutulia bila kubebwa na hisia kali ya uchama. Nina imani hayo mengine utayaona nimeyaandika.

Thread yang imegawa vipengele kwa misingi ya namba.
Kwahiyo swali lako nimeshalijibu kwenye namb 2 hapo chini ya thread.

"Kumpata mtu sahihi"? Huyo mtu yukoje? Usahihi wake utakuwa upi?
Sasa mkuu Kalamu , thread imeshamzungumzia huyo mtu anatakiwa awe yuko vipi. Afu wewe unauliza swali ambalo limeshajibiwa kupitia thread yenyewe!

Anyway kama hautojali soma tena thread yang kuanzia namba 1 na namb 2, nina imani utaliona jibu la swali lako.

CCM wana "mtu sahihi"?
Mkuu Kalamu , Kama CCM ingekuwa na mtu sahihi, mimi ningetoa ushauri huu wa kazi gani?
 
Halima Mdee ni nondo imara ya upinzani. Ila hawezi kupewa uenyekiti kwa sababu ya ukapuku wake.
Mwenyekiti wa sasa anakishikilia chama kwa sababu ya pesa zake.

Amekuwa akitumia pesa zake kuwahonga chawa mbali mbali mitandaoni, na chamani ili waendelee kumpigania kubaki katika nafasi aliyopo leo.
So sio easy kwa mtu kapuku kama Halima awe na ubavu wa kumshusha mwenye pesa zake. Waswahili wanasema mkono mtupu haulambwi.
 
Hahaha.. ila utakuwa unatembea na mnyororo mkuu, usije ukatoka nduki na michango ya chama 🤣🤣🤣
Sawa. Mimi muaminifu mno. Yaani sitadokoa nitakua na maadili yote kwa maslahi mapana ya chama chetu
 
Sawa. Mimi muaminifu mno. Yaani sitadokoa nitakua na maadili yote kwa maslahi mapana ya chama chetu
Basi tukianzisha chama nitakupigania usimame kwenye hazina ya chama chetu mkuu. I'm sure, you deserve to be the one.
 
Punguani mkubwa. Umemeliza bando langu bure
 
Kwa upinzani 2025 goli liko wazi kabisa ni wao waamue kufunga au kubutua.
Wakifuata ushauri niliowapa hapo juu watafunga goli kiulaini.
Wakipuuza na kurudisha wagombea wale wale wenye makando kando ya uongo, unafiki na uchumia tumbo, basi watajikuta wanaendelea kubutua juu hata kama golini hamna kipa.
Wabongo wengi siku hizi hawataki porojo katika mambo ya msingi.
 
Mnapataga wapi akili za kuandika nyuzi za kijinga hivi...
Kwa kweli JF kuna watu wameigeuza choo cha stand ana kun.. yeyote.
Hoja za hovyo sasa zimekuwa kama fasheni mpaka zinatia kinyaa.
Nadhani sasa tuanzishe uzi wa kuwataja wenye hadhi ya kuwapa Tuzo ya umbulula kwa kutujazia ujinga humu
 
Mkuu @Kalamu , Kama CCM ingekuwa na mtu sahihi, mimi ningetoa ushauri huu wa kazi gani?
Hivi unajisikia kuwa "umetoa ushauri" katika mada yako hii. Seriously?

USHAURI. Umempa nani?

Nitakwenda kusoma ile #31, uliyonielekeza nikaisome hapo juu; lakini sidhsni kwamba unajisikia kuwa umetoa ushauri katika mada yako iliyopo hapa.

Na ili unielewe vizuri, basi juwa kwamba sisukumwi na mambo ya "uchama" ninapochangia humu. Sina maslahi na chama chochote, ila ninayo maslahi na Tanzania tu, basi.
 
Hivi unajisikia kuwa "umetoa ushauri" katika mada yako hii. Seriously?

USHAURI. Umempa nani?

Nitakwenda kusoma ile #31, uliyonielekeza nikaisome hapo juu; lakini sidhsni kwamba unajisikia kuwa umetoa ushauri katika mada yako iliyopo hapa.
Kwani ushauri hutolewa kwa namna gani mkuu?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…