Mtu huyu akisimama na mgombea wa CCM mwaka 2025, ni lazima CCM tuangukie pua

Mtu huyu akisimama na mgombea wa CCM mwaka 2025, ni lazima CCM tuangukie pua

Mleta mada angekuwa ni mtu makini angekusoma kwa uangalifu zaidi ya kukupa 'like' kama alivyofanya hapa.

Kama kuna mtu aliyejitoa kikwelikweli (hata kama hilo halikuwa lengo na tegemeo mwanzoni mwa harakati zake), mtu huyu anayesemwa hapa kajitoa hasa. Lakini pamoja na kujitoa huko, watu aliotegemea wataelewa maana ya kujitoa kwake ikawa kama hawana habari naye. Hili linakatisha tamaa mtu yeyote yule, hata kwenye siasa.

Kuna kitu/jambo ambalo CHADEMA hawajalitambua vizuri kuhusu waTanzania, na kwa nini CCM inaonekana kuendelea kuwashikilia kama wapo jela.
CHADEMA inawapasa kudadisi na kuelewa ni jambo gani hilo.
Pamoja na ubovu wooote ilioufikia CCM, lakini waTanzania ni kama wameshikwa na sumaku wasiweze kujinasua. Jibu la CHADEMA na vyama vingine vya upinzani lipo hapo.
Wajiulize wenyewe, na wakilijua, CCM inakwisha.

Ukweli ni kwamba CCM imebaki kama mzoga tu, unaosubiri kufukiwa.
Hapana mkuu, sikumpa Like tu peke ake kama ulivyoandika hapa. Nimemjibu hoja yake vizuri, na bila shaka kaelewa ndo maana hakurudi tena. Soma post namb #31 utaona nlichoandika. Na ikiwa utairuhusu akili yako kuwa huru kuchanganua kile nlichoandika basi utaelewa nlichomaanisha. Ila kama utasoma huku umebeba hisia ya uchama ndan ya akili na moyo wako, basi itakuwa ngumu kukubaliana na kile nlichoandika. Just go back to the post number #31, read afu uje na mtizamo wako.
 
Ni yapi hasa "haya mengine"?
Soma thread yangu kwa kutulia bila kubebwa na hisia kali ya uchama. Nina imani hayo mengine utayaona nimeyaandika.

Thread yang imegawa vipengele kwa misingi ya namba.
Kwahiyo swali lako nimeshalijibu kwenye namb 2 hapo chini ya thread.

"Kumpata mtu sahihi"? Huyo mtu yukoje? Usahihi wake utakuwa upi?
Sasa mkuu Kalamu , thread imeshamzungumzia huyo mtu anatakiwa awe yuko vipi. Afu wewe unauliza swali ambalo limeshajibiwa kupitia thread yenyewe!

Anyway kama hautojali soma tena thread yang kuanzia namba 1 na namb 2, nina imani utaliona jibu la swali lako.

CCM wana "mtu sahihi"?
Mkuu Kalamu , Kama CCM ingekuwa na mtu sahihi, mimi ningetoa ushauri huu wa kazi gani?
 
Ila Halima Mdee alistahili kuwa hata M/kiti wa CDM kuliko huyu aliyepo sasa! Yule dada anajua, anajiamini na ni mchapakazi. Hayumbishwi na walioshikilia rungu iwe ndani ya chama au nje ya chama. Yuko imara kusimama na kile kilicho sahihi, siyo huyu wa mbingu na Ardhi. 😂😂 ukisema mbingu na ardhi tafsiri yake ni kuwa umeridhika na utendaji kazi wa mtu huyo 100% hivyo hauna haja ya kuweka upinzani ni halali yake aendelee bila hata kupingwa. (Mbingu na Ardhi = pepo na jehanamu) sa uko peponi sa hv nini unahitaji tena?
Halima Mdee ni nondo imara ya upinzani. Ila hawezi kupewa uenyekiti kwa sababu ya ukapuku wake.
Mwenyekiti wa sasa anakishikilia chama kwa sababu ya pesa zake.

Amekuwa akitumia pesa zake kuwahonga chawa mbali mbali mitandaoni, na chamani ili waendelee kumpigania kubaki katika nafasi aliyopo leo.
So sio easy kwa mtu kapuku kama Halima awe na ubavu wa kumshusha mwenye pesa zake. Waswahili wanasema mkono mtupu haulambwi.
 
Sawa. Mimi muaminifu mno. Yaani sitadokoa nitakua na maadili yote kwa maslahi mapana ya chama chetu
Basi tukianzisha chama nitakupigania usimame kwenye hazina ya chama chetu mkuu. I'm sure, you deserve to be the one.
 
Habari zenu wana JF wenzangu, ama baada ya salam ningependa sasa nijielekeze kwenye mada husika.

Ndugu wana JF wenzangu na watanzania wenzangu, ili chama cha CCM kiweze kushindwa katika uchaguzi mkuu wa 2025 au 2030, yanahitajika mambo matatu.

1) Kwanza: kinahitajika chama imara cha upinzani chenye sera nzuri, zinazoeleweka na kutekelezeka. Chama hicho kiwe na sura ya kitaifa, kiwe na viongozi wakweli, wenye maono na misimamo thabiti ya kuikomboa nchi. Kiwe na mifano hai ya utekelezaji wa sera zake kupitia chama husika ili kiweze kuaminika machoni mwa watanzania wengi.
a) Sio mtu useme chama chetu kina misingi ya demokrasia wakati mwenyekiti wa chama ambacho kingekuwa mfano wa demokrasia hiyo ana miaka 20 madarakani.​

b) Sio mtu useme chama chetu ni cha maendeleo, wakati wanaoendelea katika chama ni mwenyekiti wa chama taifa na genge lake, huku chama chenyewe kikiwa hakina hata ofisi ya kufanyika mkutano wa ndani.​

c) Sio mtu useme chama chetu kitasimamia utawala bora na haki, huku ndani ya chama chenyewe hakuna anaeweza kuongelea lolote mbele ya mwenyekiti wa chama au makamu wake.​

2) Pili: Anahitajika kuchaguliwa mgombea ambae hana makandokando ya uongo, uoga, unafiki na mwenye uwezo wa kweli wa kusimamia sera za chama chake bila kuyumbishwa na mtu yoyote iwe ndani ya chama au nje ya chama.

a) Sio kiongozi anakuwa na kauli za kilaghailaghai kwa maslahi yake binafsi ya kisiasa, na kiuongozi (kama tunavyoona hapo chini pichani) bila kujali madhara yatokanayo na ulaghai huo. Mtu wa aina hii ni ngumu kuchaguliwa maana watanzania wa sasa sio wale wa 2001, kule Zanzibar ambapo watu walikufa, kujeruhiwa na kufungwa, huku muhusika aliepiganiwa (aliekuwa katibu mkuu wa chama, na mgombea wa upinzani) akiwa Saudia Arabia kula tende na maswaiba zake. Mgombea akiwa hana msimamo thabiti wa kusimamia sera au hoja zake mwenye, basi hata Tume ya Taifa ya Uchaguzi ya Marekani ikija kusimamia uchaguzi bado ataangukia pua tu.​

3) Tatu: Tume huru isiyoegemea upande wowote wa kisiasa. Tume iwe na viongozi kutoka vyama mbali mbali vya kisiasa na kiraia ili kujenga sura ya utaifa katika tume hiyo.

Ni hayo tu ninayoyaona mimi, katika kuijenga Tanzania bora zaidi ya kesho.

Asanteni sana.

View attachment 2319901View attachment 2319903View attachment 2319904View attachment 2319911View attachment 2319912
Punguani mkubwa. Umemeliza bando langu bure
 
Kwa upinzani 2025 goli liko wazi kabisa ni wao waamue kufunga au kubutua.
Wakifuata ushauri niliowapa hapo juu watafunga goli kiulaini.
Wakipuuza na kurudisha wagombea wale wale wenye makando kando ya uongo, unafiki na uchumia tumbo, basi watajikuta wanaendelea kubutua juu hata kama golini hamna kipa.
Wabongo wengi siku hizi hawataki porojo katika mambo ya msingi.
 
Mnapataga wapi akili za kuandika nyuzi za kijinga hivi...
Kwa kweli JF kuna watu wameigeuza choo cha stand ana kun.. yeyote.
Hoja za hovyo sasa zimekuwa kama fasheni mpaka zinatia kinyaa.
Nadhani sasa tuanzishe uzi wa kuwataja wenye hadhi ya kuwapa Tuzo ya umbulula kwa kutujazia ujinga humu
 
Mkuu @Kalamu , Kama CCM ingekuwa na mtu sahihi, mimi ningetoa ushauri huu wa kazi gani?
Hivi unajisikia kuwa "umetoa ushauri" katika mada yako hii. Seriously?

USHAURI. Umempa nani?

Nitakwenda kusoma ile #31, uliyonielekeza nikaisome hapo juu; lakini sidhsni kwamba unajisikia kuwa umetoa ushauri katika mada yako iliyopo hapa.

Na ili unielewe vizuri, basi juwa kwamba sisukumwi na mambo ya "uchama" ninapochangia humu. Sina maslahi na chama chochote, ila ninayo maslahi na Tanzania tu, basi.
 
Hivi unajisikia kuwa "umetoa ushauri" katika mada yako hii. Seriously?

USHAURI. Umempa nani?

Nitakwenda kusoma ile #31, uliyonielekeza nikaisome hapo juu; lakini sidhsni kwamba unajisikia kuwa umetoa ushauri katika mada yako iliyopo hapa.
Kwani ushauri hutolewa kwa namna gani mkuu?
 
Back
Top Bottom