Mtwara: Wanaume walalamika kurukishwa kichurachura ili wapewe tendo la ndoa

Mtwara: Wanaume walalamika kurukishwa kichurachura ili wapewe tendo la ndoa

hongera kwa hao wanawake, maana wamejiokotea mazezeta ya bure kabisa..,never call them men
 
Baadhi ya wanaume wa Halmshauri ya mji Nanyamba mkoani hapa wamelalamika kunyanyaswa na wake zao wakati wakitaka unyumba kwa kupewa masharti ikiwemo kurukishwa kichurachura kuzunguka kitanda.

Akizungumza leo Julai 11 katika warsha ya viongozi wa serikali za vijiji katika halmshauri hiyo iliyoandaliwa na shirika lisilo la kiserikali la Smile for Community linalofadhiliwa na Legal Services Facility, Mwenyekiti wa Mtaa wa Namkuku, Andrew Mathew amesema tabia hiyo imechukuliwa ni unyanyasaji wa kingono.

“Unakuta wanaume wengine wakihitaji kupata haki zao za ndoa kuna kuwepo na mambo mengi sana yanafanyika majumbani.

“Wengine wanarukishwa kichura wanaambiwa wazunguke kitanda ili wapate haki ya ndoa, wengine wanaambiwa watoe pesa, wengine wanafulishwa nguo na wengi wanaambiwa waingie jikoni wapike na pia kuna lile kundi la kufungiwa milango na wake zao,” amesema Mathew.

Amesema manyanyaso hayo kwa wanaume yanasababisha kuwepo kwa migogoro ya ndoa, kwani baadhi ya wanaume hulazimika kutafuta wanawake wa nje ya ndoa.

“Ukikaa kuongea nao unawasikia wakielezea hii imewafanya wawe watumwa ndani ya nyumba zao, kwa hiyo wanawake wakilalamika wajue na sisi tutaanza kuvunja ukimya ili jamii ijue nini tunapitia katika ndoa zetu,” amesema.

Kwa upande wake Meneja mradi wa Haki ya Afya Kwa Maendeleo ya Binti kutoka shirika hilo, Aneth Kiyao amesema kuwa, wapo wanaume wanafanyiwa ukatili lakini hawasemi, jambo ambalo linaloifanya jamii iamini kuwa ukatili wa kijinsia ni kwa wanawake pekee.

"Ndani ya ndoa pia wapo wanawake wanabakwa na wengine wamefanywa watumwa wa ngono, ni vema tukapaza sauti kukemea haya yanayoendelea ndni ya ndoa sio sawa.

“Unawezaje kumrukisha kichurachura mumeo ili umpe haki yake ya ndoa?" amehoji Kiyao.

MWANANCHI
 
Hii ililetwa jana, kuna memba akasema rafiki yake huwa analalamika kuwa anaumwa miguu kila siku, so jamaa aka suspect huwa anarukishwa kichura usiku ndio maana miguu inamuuma.... 😁 😁 😁
 
WANAUME WALALAMIKA KURUKISHWA KICHURA CHURA ILI WAPEWE TENDO LA NDOA

Baadhi ya wanaume wamelalamikia kunyanyaswa na wake zao kwa kupewa unyumba kwa masharti ikiwemo kuwataka kuruka kichura-chura kuzunguka kitanda ili kupewa haki Yao hiyo.

Hayo yameelezwa na Mwenyekiti wa Mtaa wa Namkuku halmashauri ya Wilaya ya Nanyamba mkoani Mtwara, Andrew Mathew akichangia mada ya unyanyasaji wa kijinsia katika mafunzo yanayoendelea mjini Nanyanba.

Source Wasafi Digital
Tatizo wanawake wa mtwara viuno feni sana hadi unajikuta unatii kila analosema.
 
Nangu mene nkulukucho... Wamtwara mmetia aibu sana.
 
Acha watutese Ni zamu yao kututesa ila itafika wakati utabiri wa Isaiah 4:1 utatimia bila Shaka wanawake wataona Cha Moto Sana.
 
Na Wake zao hao huwa hawaishii tu hapo bali huwalazimisha pia Waume zao Kuwatongoza upya kabla ya kuwapa Utamu ( Unyumba ) wao Vitandani mwao.

Kwa mengi zaidi juu ya hili litafuteni Gazeti la Nipashe la Leo Jumatano tarehe 12 July, 2023 ujisomee Kiundani zaidi.
 
Back
Top Bottom