Muda sahihi wa kuiweka Dar es Salaam kwenye “lockdown” ni sasa

Mpka sasa nashishindwa kuelewa namna serikali inavyowalinda raia wake dhidi ya maambukizi.
 
Mkuu unaweza ukatuambia nchi gani imefanikiwa kuudhibiti ugonjwa huu kwa hiyo LOCKDOWN mnayoipigia chapuo?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Je kuhusu wafanya biashara wa hizo bidhaa km dereva, utingo, sokoni, nk kama wanaweza kujikinga na maambukizi, ni wazi kuwa hata wateja wao wanaweza. Hoja hii ina maana kuwa iwapo hao hawatachukua tahadhari za maambukizi watasambaza Dar na Mikoani walikotoa au kupeleka bidhaa.

Nasisitiza, jukumu la kujikinga na maambukizi ni wajibu wa mtu mwenyewe kwa usalama wake na mwingine. Kwa mfano, mimi sikubali kuguswa wala kumgusa mtu na sijumiki kwenye mikusanyiko ya watu. Ikibidi kufanya hivyo km kanisani nakaa umbali salama au navaa barakoa.
 
Serikali imekwisha kutoa ushauri wa jinsi ya kujikinga kwa maambukizi na inaendelea kusimamia utekelezaji wake. Ni jukumu la kila mwananchi kuzingatia ushauri huo kwa hiari.
 

hakuna kauli ya kishenzi kama hii. wagonjwa wakifikia buku hospital zote zikijaaa nisisikie mbuzi yoyote inaniambia mambo ya lockdown.
Hamjui madhara ya magonjwa haya. kama serikali haina uwezo wa kuwalisha maskini wake hata kwa siku 21 iseme.


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tunawaomba viongozi wetu mtusikie. Japo nyie ndiyo kama wazazi wetu kwa sasa katika kupambana na hili Janga la Covid 19, mwajua zaidi yetu na kinachotufaa.

Natoa wito na ombi mfunge Mipaka ya Jiji la DSM, magari ya mizigo ya lazima na vyakula tu yaruhusiwe. Wazee wetu huko mikoani wapo kwenye risk kubwa sana. Msisubiri ugonjwa usambae zaidi.

Msishupaze shingo jamani, hata nyie mna ndugu na jamaa wa ambao mnaweza kuwapoteza vile vile. Ukizingatia kuwa tuna upungufu wa vifaa na nguvu kazi.

Tafadhali jamani, walau muwe na huruma japo kidogo tu; hayo mapato mnayotatafuta mnaweza mkayapata na mkashindwa kuyatumia vile vile!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Umeshachelewa sn mkuu......tayari mikoa 19 imeshaambukizwa kwa hiyo hakuna Stori ya Dar hapo ni nchi nzima umeshasambaa....
Viongozi wetu wanazidi kutuangamiza kwa kukosa maarifa wanatutaka tuchape kazi huku wao wamejichimbia kusikojulikana...
TUMECHELEWA MARA MBILI...
1. JIWE ALIKATAA KWA KIBURI CHA KISHAMBA KUFUNGA MIPAKA YA NCHI ETI TUSIKOSE WATALII
2.JIWE AMEENDELEA KUKATAA KUIFUNGIA DAR PAMOJA NA USHAURI WA MH MBOWE MARA MBILI ETI TU KWA SABABU NI KAULI YA MBUMGE KUTOKA UPINZANI
 
Wamekimbilia chato kujificha huko wao wasubiri mlipuko utakapolipuka watatafutwa huko huko walikojificha

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Itapata huko alikoenda kujificha anajiita jiwe Wakati muoga amekimbia na makamu wake wamekimbia wote sijui wamejificha wapi na mwisho waziri Mkuu nae atakimbia tutapaki wenyewe sasa kila mtu atapaki akijichukulia hatua mwenyewe pasipo muongozo wa wowote wa nchi

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Samahani mkuu, huyo kwa Avatar ndo Wewe??
 
Hakuna maana ya kufunga mipaka ugonjwa ushasambaa
 
Tuendelee kuvumilia labda watajitokeza wakiguswa na upepo wa kisulisuli
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…