Muda wowote kuanzia sasa huenda kikanuka, jaza mahitaji muhimu sasa usisubiri mpaka tarehe 8 December

Muda wowote kuanzia sasa huenda kikanuka, jaza mahitaji muhimu sasa usisubiri mpaka tarehe 8 December

Mithali 22:3
"Mwenye busara huyaona mabaya na kujificha; Bali wajinga huendelea mbele wakaumia."
Mhubiri 9:11-18
Balaa huja ghafla
11Tena, nimeona kitu kimoja hapa duniani, kwamba wenye mbio hawafaulu katika riadha, wala wenye nguvu hawashindi vita; wenye busara hawapati chakula, wenye akili hawatajiriki, wala wenye ujuzi hawapandi vyeo; lakini wakati wa bahati huwapata wote pamoja. 12Mtu hajui saa yake itafika lini. Kama vile samaki wanavyonaswa katika wavu kwa bahati mbaya, na kama vile ndege wanavyonaswa katika mtego kwa ghafla, ndivyo wanadamu wanavyonaswa na balaa inapowaangukia bila ya kutazamia.
13Pia hapa duniani nimeona mfano wa hekima, na ulionekana kwangu kuwa wenye maana sana. 14Palikuwa na mji mmoja mdogo wenye wakazi wachache. Mfalme mmoja mwenye nguvu akafika, akauzingira na kujiandaa kuushambulia. 15Katika mji huo, alikuwapo maskini mmoja mwenye hekima, ambaye, kwa hekima yake aliuokoa mji huo. Lakini hakuna mtu aliyemkumbuka huyo maskini baadaye. 16Basi, mimi nasema, hekima ni bora kuliko nguvu, ingawa hekima ya maskini haithaminiwi, na maneno yake hayasikilizwi.
 
Tahadhari ni muhimu,

Huenda mambo yakawa tofauti zaidi kuliko ilivyokuwa hapo awali.

Huenda hata hiyo tarehe tajwa isifike watu wakashtukiza ,hivyo kama ulikuwa hujajiandaa kimahitaji kikamilifu utakufa njaa.

Nunua umeme wa kutosha angalau wa miezi miwili,

Jaza jaza mavyakula hayo maana kuna wauzaji wana tamaa soon wataanza kuuza kwa bei ya juu kabla hata hiyo lockdown haijafika.

Kama ni gesi nunua ya kutosha,

Acha kupiga stori barabarani na watu usio wajua ,na hata pia unaowajua ila sio kivile chuja maongezi yako usioneshe interest yako kwamba upo upande gani.


Kama wewe ni mpenda starehe nunua vinywaji vyako pendwa vya kutosha angalau kreti 30 weka ndani.

Kama mvuta shisha nunua fleva ya kutosha angalau box 5 kubwa .

Mambo yamebadilika jiandae sasa usingoje mpaka kinuke ,

Huenda jambo likaanza hata kabla ya mwezi wa 12 haujafika.

Jichunge na uchunge unaowapenda .
Mkuu ni aina gani ya watu unaowashauri wafanye hayo?

D9 inahitaji 'movement' ya kitaifa na siyo watu kujifungia ndani kama mijusi.

Wadhani ukijifungia ndani itasaidia na hautafuatwa?

Utafuatwa, tena Polisi akiwa na mjumbe wa nyumba 10 kama sheria inavyotaka, akishakukukamata hautakuja kurejea kwako milele, kaa ukijidanganya sasa!

Hali iliyopo hivi sasa inamhusu kila mmoja wetu na si kwa kundi fulani tu katika jamii, hapana.
 
Back
Top Bottom