Muda wowote kuanzia sasa huenda kikanuka, jaza mahitaji muhimu sasa usisubiri mpaka tarehe 8 December

Muda wowote kuanzia sasa huenda kikanuka, jaza mahitaji muhimu sasa usisubiri mpaka tarehe 8 December

Sasa na nyie si mumshauri ndugu yenu akiwashe Baada ya siku za vitubio ijuumaa/J2

Wabeba zege kwa wachina na wahindi hawajalipwa mafekeche yao ya wiki.!

Mamantilie hajadai madeni yake pia ataishije.!? , awe mpole kwa upolepole ndio mwendo

Michezo bila ushabiki hainogi ukitelekeza mashabiki utapoatea peke yako kibudu
 
Tahadhari ni muhimu,

Huenda mambo yakawa tofauti zaidi kuliko ilivyokuwa hapo awali.

Huenda hata hiyo tarehe tajwa isifike watu wakashtukiza hivyo kama ulikuwa hujajiandaa kimahitaji kikamilifu utakufa njaa.

Nunua umeme wa kutosha angalau wa miezi miwili,

Jaza jaza mavyakula hayo maana kuna wauzaji wana tamaa soon wataanza kuuza kwa bei ya juu kabla hata hiyo lockdown haijafika.

Kama ni gesi nunua ya kutosha,

Acha kupiga stori barabarani na watu usio wajua ,na hata pia unaowajua ila sio kivile chuja maongezi yako usioneshe interest yako kwamba upo upande gani.


Kama wewe ni mpenda starehe nunua vinywaji vyako pendwa vya kutosha angalau kreti 30 weka ndani.

Kama mvuta shisha nunua fleva ya kutosha angalau box 5 kubwa .

Mambo yamebadilika jiandae sasa usingoje mpaka kinuke ,

Huenda jambo likaanza hata kabla ya mwezi wa 12 haujafika.

Jichunge na uchunge unaowapenda .
Uko sahihi
 
Ukweli kuna tension kubwa sana. Ni kama vile kila mtu anasubiri bomu lipasuke tu. Na kwa akili hizi za akina Mwigulu sijui kama wana strategies za ku-deffuse hii tension maana wakishika vipaza sauti wanazidi tu kuchochea moto. Labda wanasubiri tena kuja kuua watu. Inahuzunisha sana kuona kwamba nchi inapitia madhila haya ili tu mtu mmoja form 4 failure asiye na maono yo yote mbali na kuiba na kujitajirisha yeye na marafiki zake na familia aendelee kutawala....
 
Back
Top Bottom