Kitu moja unachotakiwa kukikumbuka, Wewe na jamaa mmekutana tu Ukubwani ili muanze maisha Kupendana au Lah hii sio issue maana Upendo hufa wakati wowote.
Hautakuja kuwa na hadhi sawa na mama yake, Huwezi break hiyo Bond. Na ukiendelea kujaribu kukaa juu atafanya jambo la ajabu kuliko hilo.
Jua nafasi yako, kuna baadhi ya watu Mama zao huwezi kuwareplace, Ukimpayukia au kumbishia bila staha mama yake ( inaonesha ndio ulichofanya) hilo ni tusi ambalo linahitaji Jibu. Tushukuru jibu limekuwa kumtuma mtoto huku akimwangalia .
Usiporekebisha mtazamo wako juu ya Mama mkwe, ndoa yako itajifia kifo cha kawaida tu.
Kama ambavyo unampenda na kumjali mwanao, hutaki atumwe dukani usiku.
Ndio huyo mama na mwanae wako hivyo, ni wao dhidi ya Dunia nzima.