Mume amfikisha mahakamani mkewe kwa kupeleka mshahara wake kanisani

Wabeshi siku hizi wameamia makanisani!yaani inshort waganga feki wa zamani now dayz ndo manibii wa mungu..me sio judge but hyo dada hana kosa.
 
Mwanamke akishajiunga na makanisa ya kilokole anakua gaidi.
Kuna mama pale mbezi Luis, alikua anakata eneo anauza hela, anapeka kanisani.
Baadae akawa anatoa dhamani za ndani anapeleka, siku hiyo kapeleka friji.

Mwanamme akachoka akaenda kanisani kudai freji lake, ingawa waliparuana kwa maneno na mchungaji, lakini alirudisha friji, na Mama ikawa mwisho kupeleka vitu kanisani.
 
Uko vizuri mwanamme, lazima uwe na Mamlaka ndani. Ndiyo maana mwanamme, na mwanamme haolewi bali ana owa, hata Mungu amempa mamlaka Mwanamme.

Hakuna aliemuona Mungu, ila vitabu vya dini vinasema, Mungu alimuumba mwanadamu kwa mfano wake, je ukivuta taswira unaona Mungu ana Umbo la kike, je kwanini Wengine Wakiomba, hutumie neno Baba yetu uliembinguni, na siyo Mama yetu.
 
Sahihi
Naona wanawake mnakomaa,lakini undani wa maisha yao hamuufahamu. Kama mwanamke hataki fedha zake zihudumie familia aache kazi. Lakini kutoka asubuhi kwenda kupoteza muda huna unachochangia ni upimbi. Aache kazi ili pesa yake isitumike.
 
Huna point zaidi ni inaonekana wewe ndo mchungaji unayepoke hizo pesa
 

Akili umeacha wapi?
Hao watoto nani atawalisha kuwasomesha na kuwavisha?
Nani atalipa matumizi mengine kama hela zote anapewa baba mchungaji?
 
Dah....muda sio mrefu...Kuna mwanaume atakuja kulalamika humu .....mkewe hamuachii pesa ya matumizi 🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣👏🏼
 
Ni aibu dume Zima kung'ang'ania fedha za mkeo. Sio kazi yake kuhudumia familia. Kidume ng'ang'ana !!! Akikunyima chini ya kitovu hapo nenda mahakamani... Lakini sio kadi yake ya benki.!!!

Sent from my TECNO BA2 using JamiiForums mobile app
Basi akae nyumbani, mimi nipoteze haki zangu za kuhudumiwa kama mume, kuna muda nahitaji huduma yake, naikosa sababu yupo kazini.
 
Kweli kuna wanaume viazi yani wewe na Mke mfanye kazi halafu useme hela ya Mkeo atumie anavyotaka huku wote MNA watoto wana wategemea.
Ndio maana Wazungu wanatuzidi.
Umeona mkuu, kuna wanaume hawaelewiki maana ya mke kufanya kazi nini sasa, kama hela yake haingezi kipato cha familia, haya hanafanya kazi ya kuajiliwa je wanawake walioko kwenye biashara.
 
Issue hapo sio mwanamke kutoa fedha kwa familia ni yeye kupeleka fedha kwa mwanaume mwingine
Kutoa sadaka na kumpa pesa mchungaji ni vitu tofauti

Hakuna muumini hutoa pesa kwa mchungaji ila hutoa sadaka kanisani.Na mchungaji hawezi jua nani katoa nini sababu sadaka huwekwa kwenye chombo cha sadaka kwenye makanisa yote yawe.ya kilokole au la

Huyo mwanaume ana hasira tu na ulokole ni fanatic.tu wa kikatoliki. Hawezi thibitisha popote kuwa pesa huyo mwanamke huwa anazipeleka kwa mchungaji

Hata wewe aliyeandika uko kwenye kundi hilo hilo.Sadaka hazipewi mkononi ikifika kipindi cha kutoa sadaka kila.mtoa sadaka huwekwa kwenye chombo cha sadaka mwisho huenda kuhesabiwa sasa pale huwezi sema hii sadaka ya fulani
Huyo mwanaume Mzushi
 
Mkuu ni majanga, unashangaa ghafla mwanamke ana chale za kutosha mwilini na hakuwa nazo. Unapata habari baadaye kuwa alikuja mganga kuzindika nyumba na biashara kalipwa laki tano na hela ya usafiri. Unawaangalia watoto wako na kufikiria hatima yao, kama ukitoweka ghafla unachoka, unaamua kuendelea kuwepo uwasogeze sogeze huku ukimfungia wife mirija ya pesa taratibu ili awe na adabu, wakati mwingine inakuwa too late.
 
Wanaume tafuteni pesa, pesa ya mwanamke ni yake, ila ya mume ni yenu.
Huo muda unaotumia huko kazini huoni kwamba ni wa kuhudumia ndoa? Muda huo ungekuwa labda unaogesha mtoto, unaunga mboga, unafanya usafi ndani, unafua etc.. Sasa uutmie muda wa ndoa kutafuta fedha and then unachokipata ndani ya muda huo kiwe chako binafsi..!! UBINAFSI HUO
 
Tatizo kubwa si kuhama tu dhehebu bali namna mwanamke anavyotoa hela yote kwa mchungaji badala ya kufanya angalau matumizi ya kifamilia
 
Nyie ndiyo mnaongopea wa Mama wa Watu kua sadaka zao zinaenda mbinguni,kumbe nyie ndiyo mnajifanya mbingu wenyewe na kubunya sadaka za akina Mama masikini,msijione wajanja sana,Malipo hapa hapa Duniani mtalipa tu,karma haijawai kukosea address ya mteja wake, is just a matter of time tu!!

Sent from my TECNO KC8 using JamiiForums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…