Mume amfikisha mahakamani mkewe kwa kupeleka mshahara wake kanisani

Mume amfikisha mahakamani mkewe kwa kupeleka mshahara wake kanisani

Wabeshi siku hizi wameamia makanisani!yaani inshort waganga feki wa zamani now dayz ndo manibii wa mungu..me sio judge but hyo dada hana kosa.
 
Mwanamke akishajiunga na makanisa ya kilokole anakua gaidi.
Kuna mama pale mbezi Luis, alikua anakata eneo anauza hela, anapeka kanisani.
Baadae akawa anatoa dhamani za ndani anapeleka, siku hiyo kapeleka friji.

Mwanamme akachoka akaenda kanisani kudai freji lake, ingawa waliparuana kwa maneno na mchungaji, lakini alirudisha friji, na Mama ikawa mwisho kupeleka vitu kanisani.
 
Jamani msicheke na wanawake ndoa nyingi zimevunjika kwa wanaume kutowafuatilia wanawake,mimi mke wangu anafanya kazi kila mwezi nahitaji (Lazima)anipe orodha ya matumizi ya mshahara wake kuna wakati ananunua viatu pear 3 kwa wakati mmoja ndani kuna pear zaid ya 40 ujinga huu siuruhusu hapo ni ban ya kununua viatu miezi 3,kuna wakati kwa makusudi akiniambia sukari imekwisha namwambia kanunue na pesa yako na nikute mfuko upo ndani ni amri sio ombi.mshahara wa house girl ni jukumu lake na ninachotaka kujua kalipwa ni lazima sio ombi ,na nimemwambia kama hataki nifuatilie matumizi ya mshahara wake akae nyumbani hakuna tatizo .
Uko vizuri mwanamme, lazima uwe na Mamlaka ndani. Ndiyo maana mwanamme, na mwanamme haolewi bali ana owa, hata Mungu amempa mamlaka Mwanamme.

Hakuna aliemuona Mungu, ila vitabu vya dini vinasema, Mungu alimuumba mwanadamu kwa mfano wake, je ukivuta taswira unaona Mungu ana Umbo la kike, je kwanini Wengine Wakiomba, hutumie neno Baba yetu uliembinguni, na siyo Mama yetu.
 
Sahihi
Naona wanawake mnakomaa,lakini undani wa maisha yao hamuufahamu. Kama mwanamke hataki fedha zake zihudumie familia aache kazi. Lakini kutoka asubuhi kwenda kupoteza muda huna unachochangia ni upimbi. Aache kazi ili pesa yake isitumike.
 
Tatizo liko kwa wanaume oeni wanawake Saizi yenu !wewe lofa kidume kwenu kunguni tupu nyumba za majani umeme hata hakuna mnatumia vibatari unapata kikazi magereza uaskari unaenda mfano kuoa binti mtoto wa Bakheresa. Unaanza kuleta vi theory vya ajabu vya porini huko

Oa kwenu porini huko huyo mwelewa wa vimila vyenu vya kipuuzi na kichwa kwa kidume ndio chenyewe hata kiwe lofa

Kaoe kwenu kwa maskini wenzio
Wazazi matajiri hawaombi ATM za watoto wao wewe kidume lofa ndie ujitie kudai
Vidume wenye msimamo kama wako wakaoe wanawake vijijini kwao wale wasiojua hata kuoga wala kwenda saluni
Huna point zaidi ni inaonekana wewe ndo mchungaji unayepoke hizo pesa
 
Hayamhusu huyo kidume kiofisa koko cha magereza kilinda wafungwa wakinya wasije kutoroka

Mwanamke akipata pesa yake kwa nini utake kudhibiti pesa yake matumizi? Mkataba wa ndoa unatamka kuwa ukioa utadhibiti matumizi ya pesa za mkeo? Mbona wewe hakuombi ATM yako?

Hii kesi tamu hukumu yake itakuwa landmark kuonyesha kama mke ana haki ya chake akipatacho kwa jasho lake kuwa lazima kidhibitiwe na mwanaume aliyemuoa kuwa mwanamke hana uhuru wa kutumia pesa yake hata kununua pedi bila ruksa ya mume aliyeshikilia ATM kisa alilipa mahari.Kuwa hata akitaka pedi ambembeleze mwanaume kuwa naomba ike ATM niliyokupa Katoe pesa nikanunue pedi navuja siku zangu mume wangu niko chini ya miguu yako katoe

Akili umeacha wapi?
Hao watoto nani atawalisha kuwasomesha na kuwavisha?
Nani atalipa matumizi mengine kama hela zote anapewa baba mchungaji?
 
Dah....muda sio mrefu...Kuna mwanaume atakuja kulalamika humu .....mkewe hamuachii pesa ya matumizi 🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣👏🏼
 
Ni aibu dume Zima kung'ang'ania fedha za mkeo. Sio kazi yake kuhudumia familia. Kidume ng'ang'ana !!! Akikunyima chini ya kitovu hapo nenda mahakamani... Lakini sio kadi yake ya benki.!!!

Sent from my TECNO BA2 using JamiiForums mobile app
Basi akae nyumbani, mimi nipoteze haki zangu za kuhudumiwa kama mume, kuna muda nahitaji huduma yake, naikosa sababu yupo kazini.
 
Kweli kuna wanaume viazi yani wewe na Mke mfanye kazi halafu useme hela ya Mkeo atumie anavyotaka huku wote MNA watoto wana wategemea.
Ndio maana Wazungu wanatuzidi.
Umeona mkuu, kuna wanaume hawaelewiki maana ya mke kufanya kazi nini sasa, kama hela yake haingezi kipato cha familia, haya hanafanya kazi ya kuajiliwa je wanawake walioko kwenye biashara.
 
Issue hapo sio mwanamke kutoa fedha kwa familia ni yeye kupeleka fedha kwa mwanaume mwingine
Kutoa sadaka na kumpa pesa mchungaji ni vitu tofauti

Hakuna muumini hutoa pesa kwa mchungaji ila hutoa sadaka kanisani.Na mchungaji hawezi jua nani katoa nini sababu sadaka huwekwa kwenye chombo cha sadaka kwenye makanisa yote yawe.ya kilokole au la

Huyo mwanaume ana hasira tu na ulokole ni fanatic.tu wa kikatoliki. Hawezi thibitisha popote kuwa pesa huyo mwanamke huwa anazipeleka kwa mchungaji

Hata wewe aliyeandika uko kwenye kundi hilo hilo.Sadaka hazipewi mkononi ikifika kipindi cha kutoa sadaka kila.mtoa sadaka huwekwa kwenye chombo cha sadaka mwisho huenda kuhesabiwa sasa pale huwezi sema hii sadaka ya fulani
Huyo mwanaume Mzushi
 
Wengi wa humu ni Watoto hata kuonja k hawajawahi! Comments zinaonesha ukurupukaji. Hii ilitokea kwa Marehemu Dr Likwelile ambaye alimuacha mkewe wa kwanza kwa kupeleka gari na kulitoa kanisani ati ameokoka! Ukiona mwanamke anafanya kitu kama hicho bila kushauriana na mumewe, jua anachepuka
Mkuu ni majanga, unashangaa ghafla mwanamke ana chale za kutosha mwilini na hakuwa nazo. Unapata habari baadaye kuwa alikuja mganga kuzindika nyumba na biashara kalipwa laki tano na hela ya usafiri. Unawaangalia watoto wako na kufikiria hatima yao, kama ukitoweka ghafla unachoka, unaamua kuendelea kuwepo uwasogeze sogeze huku ukimfungia wife mirija ya pesa taratibu ili awe na adabu, wakati mwingine inakuwa too late.
 
Wanaume tafuteni pesa, pesa ya mwanamke ni yake, ila ya mume ni yenu.
Huo muda unaotumia huko kazini huoni kwamba ni wa kuhudumia ndoa? Muda huo ungekuwa labda unaogesha mtoto, unaunga mboga, unafanya usafi ndani, unafua etc.. Sasa uutmie muda wa ndoa kutafuta fedha and then unachokipata ndani ya muda huo kiwe chako binafsi..!! UBINAFSI HUO
 
Hapa wote wawili ni fanatics
Mke fanatic wa ulokole Mume naye ni fanatic mkubwa wa ukatoliki.Kwake mke kuhama ukatoliki kesi!!.wakati katiba ya nchi inaruhusu mtu kuwa ana uhuru hadi wa kubadili dini!!

Ukiangalia cause hapo kubwa ni catholic fanaticism ya mwanaume!! Yuko so fanatical kiasi kuwa akili imemuhama hadi ataka ATM lakini Nadhani main reason anataka kuforce mkewe arudi katoliki kwa kutumia coercive force.

Anyway maparoko wakae na mtu wao huyo kidume mdai ATM apewe na mkewe kumpa ushauri nasaha kwenye issue za difference za kiimani zikitokea baada ya ndoa kufungwa kikatoliki how to manage marriage peacefully in such a situation badala ya kutumia nguvu kuforce mtu arudi kwenye dini kwa kufanya vurugu nk
Tatizo kubwa si kuhama tu dhehebu bali namna mwanamke anavyotoa hela yote kwa mchungaji badala ya kufanya angalau matumizi ya kifamilia
 
Kutoa sadaka na kumpa pesa mchungaji ni vitu tofauti

Hakuna muumini hutoa pesa kwa mchungaji ila hutoa sadaka kanisani.Na mchungaji hawezi jua nani katoa nini sababu sadaka huwekwa kwenye chombo cha sadaka kwenye makanisa yote yawe.ya kilokole au la

Huyo mwanaume ana hasira tu na ulokole ni fanatic.tu wa kikatoliki. Hawezi thibitisha popote kuwa pesa huyo mwanamke huwa anazipeleka kwa mchungaji

Hata wewe aliyeandika uko kwenye kundi hilo hilo.Sadaka hazipewi mkononi ikifika kipindi cha kutoa sadaka kila.mtoa sadaka huwekwa kwenye chombo cha sadaka mwisho huenda kuhesabiwa sasa pale huwezi sema hii sadaka ya fulani
Huyo mwanaume Mzushi
Nyie ndiyo mnaongopea wa Mama wa Watu kua sadaka zao zinaenda mbinguni,kumbe nyie ndiyo mnajifanya mbingu wenyewe na kubunya sadaka za akina Mama masikini,msijione wajanja sana,Malipo hapa hapa Duniani mtalipa tu,karma haijawai kukosea address ya mteja wake, is just a matter of time tu!!

Sent from my TECNO KC8 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom