Vp kuhusu mama Maria kusema alilazimishwa kwenda kwenye mkutano wa Jiwe kuongeza vichwa?Tusijilishe upepo jamani ngoma kama ni hivi basi bado imebana, kwa msio fahamu Mwitongo kwa Baba wa Taifa kama jina linavyojiita kwa sasa pamekuwa ni Miuziumsi kwa kizungu na kwa kiswahili ni sehemu ya makumbusho. Hivyo pana hotel na kila kitu ndiyo maana serikali inawahimiza watu wafike pale kwani unakuwa unakumbuka historia ya Tanganyika mpaka Tanzania na mengine pia unaichangia familia ya Mwalimu Nyerere na serikali.
Hivyo mtu yoyote ndani ya Tanzania na nje ya Tanzania anakaribishwa Mwitongo kama mtalii wa ndani au wanje, na aliyeteuliwa pale ni Madaraka Nyerere yeye anapokea wageni wowote kwa upendo wote, sisi tulikuwepo pale mwezi wa 5 alitupokelewa na Madaraka mwenyewe hanashida. Hivyo hilo kufanya kama mtaji wa kisiasa au kiki naona ni la kilofa kwani kura kama hazikutosha mtasema tumeibiwa, mbona tulipokelewa hata na Madaraka Nyerere nyumbani kwa baba wa taifa.
Namimi nachukuwa fursa hii kuwaambia watanzania kuwa waende Mwitongo pana mambo mazuri ya kujifunza pia pana huduma zote za chakula, kulala na mapumziko kwa mtu binafsi hata familia na hata taasisi pia, ni mahala pazuri sana jitokezeni kama Lisu na wengine ni kwa watanzania wote. Ndiyo maana Lisu alimtukana Nyerere lakini Madaraka anampokea hilo ndilo jukumu alilopewa na familia. Ndiyo maana Lisu amekuwa pale na waandamizi wa chama pamoja na yule Askofu wote wamelala pale kwa ghalama zao Madaraka kaingiza na hili ni zuri kuchangia kwani pia panalipa kodi kwa serikali.
Sent from my Infinix X680 using JamiiForums mobile app