Ni pamoja na kumdhibiti Rais, kwani hiyo sheria kuwa reviewed ndiyo mwisho wa maisha?
Wamdhibiti rais kwa katiba hii? Hata hivyo tuko kwenye mchakato wa katiba mpya, kwanini waendelee kutunga sheria nyingine ambazo sio za dharura, kwanini tusisubiri katiba mpya ili sheria nyingi ziwe ndani ya hiyo katiba mpya?
 
Kama kuna watu wanapewa Uhuru wa kujieleza halafu wanautumia vibaya kutukana viongozi hata wakuu wa Nchi kwa kigezo ni wapinzani hii sheria itaenda kuwadhibiti ipite tu kwa nguvu zote ili tuheshimiane
Ingekuwa hao viongozi wanaingia madarakani kwa chaguzi halali, huu utetezi wako ungekuwa na hoja.
 
Mbaya sana hii,kama kelele zetu hazitasikika ni Bora Wapinzani wamlilie beberu Marekani na Washirika wake.
Hatari sana hii.
 
Maana yake wataweza mteka mfanyakazi wa JF na kulazimisha kupata watu wanaowataka.


Hapo mbona itasababisha na wao waanze kuwindwa?
 
Kama kuna watu wanapewa Uhuru wa kujieleza halafu wanautumia vibaya kutukana viongozi hata wakuu wa Nchi kwa kigezo ni wapinzani hii sheria itaenda kuwadhibiti ipite tu kwa nguvu zote ili tuheshimiane
Ni ujinga na wenda wazimu kutunga sheria eti kwa kulenga wanaoitukana serikali, zitungwe sheria kwa kwa kuzingatia taifa kwanza kwa miaka mia ijayo na kwa kizazi kijacho,

Huu ni upuuzi eti unakimbiza limswada kujilinda na wakosoaji na watukanaji ,

Tatizo Afrika kiongozi akisha kuwa pale juu sijui hujiona nani , wakati ni binadam yule yule wala kuwa pale hakujambadilisha kitu chochote nje ya kuwa na kipato cha juu kuliko wengine,

Sasa endeleen mtajua hamjui ,nasema hili kwa confidence kubwa mno maana Mungu wangu yupo up to date sana
 
Naanza kuona dalili za Samia kutaka kubaki/kubakishwa madarakani kwa mda mrefu kwa maslahi ya wanaonufaika, machawa, mafisadi na walamba asali
 
Hongera mkuu for the well informed article.
 
Nchi zote zenye uongozi makini zinaweka mifumo yake ya kiulinzi na kiusalama kwa kuangalia maslahi mapana ya taifa, wala siyo kwa tamaa ama utashi wa kisiasa ama maslahi ya chama tawala kutaka kubakia madarakani kwa gharama yoyote ile.

Katika muswada huu Rais atakuwa anajiaibisha yeye mwenyewe na serikali ya chama chake, inaonyesha ni kwa jinsi gani yeye na chama chake ni wenye mashaka mengi. Wanatambua kuwa wapo katika hofu kubwa kwa kadiri miaka ya chaguzi za 2024 na 2025 zinavyozidi kukaribia. Kwa hiyo basi kilichobaki ni kutumia hila na hadaa ili kuudhibiti upinzani dhidi a chama tawala.

Mambo ni mengi na muda ni mfupi, kuna minyukano ndani ya chama chake kote bara na visiwani, kuna muitikio chanya kwa wananchi kwa vyama vya siasa hasa hasimu wake mkuu CDM, kuna viguvugu la wanaharakati ambalo kwa sasa linapata "attention" kubwa katika makundi yote ya kijamii, kuna hii idara yenyewe ambayo Ina mgawanyiko mkubwa ndani yake kifuatana na kifo cha Mkuu aliyepita.

Ni vyema kama nchi ukasukwa mfumo imara wa taasisi nyeti ya urais kuliko kumfanya Rais kuwa ndiye kila kitu. Rais anapaswa kudhibitiwa hata kama ndiye kiongozi wa juu wa taasisi hii. Kuruhusu taasisi hii kuendeshwa kama chombo cha mtu binafsi, kwa hisia, na mihemuko, kama nchi tunakwenda kuchuma majanga.

Hakuna atakaye baki salama, kila asiyejipendekeza kwa Rais atashughulikiwa. Zitawelwa hila dhidi ya watu tishio kwa watawala, wataumizwa na kuuawa kisa kwa kisingizio tu cha kulinda usalama wa taifa, pasipo wahusika kuwajibishwa kupitia matendo yao. Hii ni aibu kwa watawala kutaka kufanya hila katika masuala nyeti ya taifa letu la Tanzania.
 
Amen
 
Hii nchi ni mali ya Ccm, acha wafanye watakalo.
 
Wasiwasi wa matendo waliyofanya awamu ya Tano... tatizo lakuwa na wabunge ambao wanaona mpaka mwisho wa pua zao, hawaoni mbali!!! Leo tunarais mungwana, Je vp akitokea rais katili kama au kumzidi yulee... Ninini kitamzuia kumwaga damu ya yeyote anayempinga???
 
Ila wajue kuwa what goes around come around
 
Daa nchi yangu:-
1. Huyu analeta sheria mpya ili kulinda baadhi ya watu wake na kumlinda yeye badala ya kutengeneza sheria ya kuwalinda watanzania wote. Mwenzake aligeuza mgambo wa maliasili kuwa jeshi usu na zimamoto kutembea na silaha za moto mwisho wa siku ni mauaji kila siku kwenye mbuga za wanyama, ziwani, kwenye mito, maporini, mistuni. n.k
2. Na wabunge wetu walivyowasahaulifu wataipitisha wakifikiri itawakomesha wapinzani na raia tu kumbe mbele ya safari itawangáta wao na kama sio wao basi ndugu zao.
3. Ni wakumbushe tu Bashe, Nape, Januari na Ndugai wakati mnapitisha hii sheria kumbukeni madhila yaliyowapata wakati wa utawala uliopita Pia Mzee Makamba na Kinana kumbukeni mlivyobatizwa kwa moto.

Kwa ufupi sana hii sheria ni nzuri tu kwa wale walio karibu na kiongozi husika kwa muda fulani. Lakini akija kiongozi mwingine hawa hawa watakaoipitisha sasa watabatizwa kwa moto na sheria hii hii wanayotaka kuipitisha. Kwa kuwa sisi binadamu tuna tabia ya ubinafsi na kujisahau bila shaka hii sheria itapitishwa kwa kishindo lakini Mungu alivyo fundi hawa hawa wanaoipisha wengi wao itakuja kuwanyoosha huko mbele ya safari.

Muda ni mwalimu mzuri.

Ni tizamo tu
 
Usarama wa taifa kupewa uwezo huo si hatari kwa wanainchi wa kawaida Bari mafisadi"

Na Kama mnavyo jua majizi nimajitu yenye mapesa mengi kiasi kwamba Yana mzidi nguvu mpaka raisi kwenye maamzi ya Kima endeleo


Na raisi akiwauliza Usarama wa taifaHawa watu vipi?

Wana mwambia tunaweza kuwadhibiti Hawa majizi lakini nyuma yao Kuna akina nanii na nanii pale bungeni na wizarani na pale mahakamani Sasa tunashindwa


Nafikiri ndiyo maana samia ameamua kuwapa uwezo Usarama wa taifa kufanya kazi automatically pale ambapo panapaswa kushughulikiwa haraka

Nakisha baadae wakatoa maelezo kwa bosi wao ambaye atakuwa ni raisi tu sio waziri frani Tena wakati waziri huyo ndiye aliye nyuma ya mafisadi nama jizi kwataifa letu

Nina imani mm sheria hii ninzuri isipokuwa kuwe na marekebisho madogo madogo sababu

Tanzania panaonekana Kuna serikari ndani ya serikari

Serikali hiyo inaitwa

SERIKALI YA MAFISADI ISIYO FIKIKA ILIYO JIFICHA NDANI YA SERIKALI YA WANAINCHI KIVULI

kwa hiyo Nanjia pekee nikuiwezesha TISS ili ibaki serikari sahihi isiyo weza kumyumbisha raisi.

Haiwezekani raisi anaongea hili waziri anaongea hili.
Raisi anatoa billion 2 wizara husika inapokea Kisha inatoa million 200 nyingine mfukoni

hukunyuma WANAINCHI hawapati huduma kwa MDA wanaanza kumlaum raisi

Amini nawaambieni Usarama wataifa utakuwa unanguvu ya kufanyia kazi hata maoni yenye Tina mnayo yaweka jf na kuya fanyia kazi kwa vitendo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…