Kimsingi Kauli kama hizi hutokewa na watu wajinga na ambao wanaishi kwenye mawazo ya kale na kusikiliza stori za vijiweni zilizojaa uongo na mihemko.
Mwambukusi Toka anazaliwa Hadi anazeeka yeye Kila kitu anapinga Hadi Sasa Anatukana kwao,huu ni ugonjwa sio kawaida.
Mwambukusi anatakiwa kuelewa kwamba Yuko out of date na hana takwimu Wala data za kusema Mbeya ambayo ni kitovu Cha Uchumi wa Nyanda za Juu Kusini na Mkoa namba 3 Kwa Uchumi Mkubwa Tanzania nzima eti hauna mzunguko.
Mzunguko upi anaouzungumzia Mwambukusi? Mbeya ni kati ya Mikoa 4 ambayo wakazi wake Wana stable income Kwa mujibu wa takwimu Rasmi.
Aisha Mbeya ni kati ya Mikoa 10 inayoingiza mapato mengi TRA.Mbeya Ina Uchumi mkubwa wa dhahabu ambapo soko lake kule Chunya linaongoza Tanzania Kwa mauzo na Mapato.
Suala la miundombinu ni Changamoto ya miji yote Tanzania ikiwemo huko huko Dar anakoshinda ,lakini pia ujenzi unaendelea na mwingine umesgafanyika wa Barabara za mitaani ila Mwambukusi hafahamu zaidi ya kuponda.
View: https://www.instagram.com/p/Dbqs4ZWlow0/?igsh=MTZxcHlzazM3ZDhwdQ==
My Take
Mwambukusi anatakiwa kuelewa kwamba takribani Kila business entity iliyoko Dar pia Ina Tawi Mbeya ,kungekuwa hakuna huo mzunguko hakuna matawi ya biashara yangefunguliwa Mbeya.
View attachment 3644013