Mwalimu atelekeza kazi baada ya malipo ya mshahara wa Tsh 34,000 kwa mwezi

Unafungua sana code mkuu, huwezi kukuta mwl wa kijijini anafundisha twisheni eti kuongeza kipato walimu mlioko town pigeni tuition sana tena muwafuta watoto majumbani kwao
 
Jibu kwanza swali langu mkuu ni system gani inaweza kukulipa nusu mshahara afu useme imekuondoa?
Ooh!

Kumbe hatukuelewana mkuu!

Nilichokuwa nakijadili mimi ni kwenye huu utoro mpya alioufanya baada ya kulipwa elf34 na kukimbia kazi, sio ule wa zamani alioenda na akarejea kazini kisha kuadhibiwa kwa kukatwa mshahara!

Sasa hivi kaondoka kiutoro kwa mara nyingine tena bila ruhusa ya mwajiri wake.

Baada ya muda flani kupita asiporejea, bodi ya uchunguzi itakaa na kumfuta katika daftari la ajira, ndicho nilichokuwa nakijadili mimi kwa kusema kuwa, anakokimbilia hata akitafuta kazi kuajiriwa itakuwa si rahisi kwa sababu sasa hivi "data base" ya daftari la ajira kwa watumishi wa umma ni moja tofauti na zamani.
 
Kwa taarifa yako nikipata cheki namba kama sina cheti feki nikitaka kurudi kazini narudi tu muda wowote,kama una ndugu au rafiki anae hiyo shida nipm tusaidiane
 
Unafungua sana code mkuu, huwezi kukuta mwl wa kijijini anafundisha twisheni eti kuongeza kipato walimu mlioko town pigeni tuition sana tena muwafuta watoto majumbani kwao
Kuwafungulia code wanaodharau Kazi ya ualimu, walimu wengi wamejenga nyumba za kisasa nzuri tu.True pia fursa nyingi mjini.
Maisha ni akili
 
Walimu wanapata pesa ndefu tu,sema ni matumizi yako ndo yataamua sasa...
 
Degree 716000/=
 
Alikuwa hana wito wa ualimu
 
Hakuna mshahara wa elfu 34 serikalini katika mfumo rasmi wa ajira hii taarifa ni ya uongo.
 
Walimu wanasomesha watoto shule za mamilion. Watoto wanamaliza vyuo vikuu. Unatokea mmbwa mmoja unawazaririsha wengine.

Na auze bar na auze na K na bado atalaaniwa
 
Labda kama huko bagamoyo wana mfumo wao wa ulipaji wa mshahara kwa watumishi wa umma
 
Huyu inaonekana madeni mengine hayajapita kwenye mfumo wa mshahara na ndio maana anabaki na fedha hiyo, na kama ameadhibiwa kwa mujibu wa sheria hakuna kosa hapo aendelee kupambana.
 
Waache waisome namba. Huenda akili zao zitakaa sawa.
 
Haiwezekani maana kwenye mfumo wa ulipaji mishahara moja ya tatu hairuhusu.
Ukiwa umekopa benk umebakiwa na 1/3, halafu ukapata kosa la kukatwa mshahara na serikali, makato yanapenya tu bila shida. Labda itakuwa huyo Mwl pia alikuwa amekopa zile sehemu za kuacha ATM ndio maana alibakiwa na wlfu 34.

Halafu hiyo 1/3 naona huwa wameiweka kwa ajili ya mabenki, na siyo kwa ajili ya makato ya serikali. Kwa mfano, hata bodi ya mikopo haiangalii 1/3, inapenya tu.

Kama jambo hulijui, penda kutulia halafu utajifunza kwa watu!

Sent from my TECNO F1 using JamiiForums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…