Mwalimu Nyerere: Mafanikio, mapungufu na misingi ya taifa letu.

Hatimae umeunga mkono hoja
 
Sawa
 
Wewe sijui hujaelewa hoja
Yanayotokea leo ndio kwa namna moja au nyingine anapokea lawama

Kwa sababu wao ndio walikosea mfumo bora tangu mwanzo
Mf: katiba na muungano
Hoja nimeelewa vizur sana hapa,labda huenda nyie ndio hamtaki kukubali kwamba sio kila kosa ni la Nyerere

Kuna mambo ya moja kwa moja unaweza kumlaumu Nyerere kama katiba au swala la Muungano,lakini sio kila jambo anapaswa kupewa lawama

Kuna mengine watangalizi wake wangepaswa kuyabadilisha,ndio maana hata yeye alisema Kuna mambo ya kijinga alifanya lakini kibaya zaidi bado watangulizi wake wanayaiga, je hapa wajinga ni yeye au watangulizi wake?
 
Nyerere ana mengi mazuri ila hakuwa mchumi mzuri na pia alijuhusisha na mambo mengi sana ambayo hayakuwa na faida kwa Tanganyika kama nchi. Alikuwa idealist sana pia.
Kosa lake kubwa ni kutokuacha Tanganyika ipatikane mwaka 1994 au kuto kuiunganisha Zanzibar kuwa nchi moja mwaka 1984 alipomtoa Jumbe madarakani.
Ni nafasi ambazo hazirudi tena. Pia aliamini CCM itawajali wananchi akasahau alimfanya Mwenyekiti wa Chama akawa ni Raisi wa nchi.
Mwenyekiti alivyoingizwa na wafanyabiasha chama kikawa cha wafanya biashara kikaachana na wakulima na wafanyakazi.
Muundo halisi wa CCM ni ule wa nchi kuwa na katiba ya chama kimoja. Wafanyakazi kama wanachama wa chama walikua na jukumu la kukitetea chama. Baada ya kuletwa vyama vingi, kikaondolewa mikononi mwa wafanyakazi na kuwekwa mikononi mwa Wafanyabiashara.
Madhara yake ni tabaka la Wafanya biashara kuamua namna ya kuendesha nchi. Macho yao ya kwanza ni faida kwanza kabla ya kuangalia mkulima na mfanyakazi wanataka nini.
 
Urithi mbaya wa Nyerere ni pamoja na Katiba hii mbovu tuliyonayo.
Nyerere hakuamini kwenye Demokrasia ya matendo zaidi alikuwa na maneno tu.

Kwa Nguvu na ushawishi alikokuwa nao angeweza kushawishi kuundwa kwa Katiba inayoruhusu utawala WA Kidemokrasia badala yake alitengeneza mazingira mpaka sasa Katiba ya yetu ni ya mfumo wa Chama kimoja.
Kwa Katiba yetu ni kichaa peke yake anaweza kuamini CCM itaondoka Madarakani.
Naomba mniruhusu niseme Nyererea amechangia mauaji ya oktoba 29.
 
Kwani Nyerere kalaumiwa kwa kila kitu mkuu?
 
Miongoni mwa vitu alivyofanikiwa Nyerere ni kuweza na kuikuza na kuiendeleza lugha ya kiswahili na kuifanya iwe lugha mama na inayozungumzwa na kueleweka na watu wengi na makabila mbalimbali, kujenga taifa lisilokuwa na udini na ukabila kwa kiasi kikubwa

Mapungufu yake ni kuingia haraka na bila kutafakari kwa kina kwenye siasa za ujamaa, muungano wa 1964, kutengeneza katiba ya mwaka 1977 ambayo imeifanya ccm kuwa chama dola kuliko chama Cha kisiasa..

Yote kwa yote anabaki kuwa muasisi wa taifa letu regardless ya disaster aliyotengeneza either kwa kujua au kutokujua
 
Mimi hua si comment humu mara kwa mara ila leo wacha ni comment. Asee huyu ShesRise_1 ni mtu mmoja mwenye akili sana. Hua napitia maada zake kmya kmya na most of mada zake ni za kujenga. Nakupongeza sana ShesRise_1 kwa kua ww ni moja kati ya Great thinker wa Jamii Forums. Moderator napendekeza huyu member apewe uplatnum member
 
Hapa nawahitaji wafuatao... Kiranga (pundit) Mkandara @udadisi Susuviri Nyani Ngabu Jasusi if you know what I mean
 
Hakika hakika alifanya kazi nzuri sana

Mapungufu yake ni kuingia haraka na bila kutafakari kwa kina kwenye siasa za ujamaa, muungano wa 1964, kutengeneza katiba ya mwaka 1977 ambayo imeifanya ccm kuwa chama dola kuliko chama Cha kisiasa..
Chama dola hapa alikosea timing aisee alituingiza chaka
Lakini si tunaweza kufanya kitu?
Yote kwa yote anabaki kuwa muasisi wa taifa letu regardless ya disaster aliyotengeneza either kwa kujua au kutokujua
Nyerere ni Baba wa Taifa
 
Shukran sana mkuu 🙏🙏
Lakini kusifiwa hivi mbele ya hadhara sio rahisi kwangu hata kidogo

Shukran mnoo 🤝
Moderator napendekeza huyu member apewe uplatnum member
Muda ukifika nitapewa
Asante sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…