Mwalimu Nyerere: Mafanikio, mapungufu na misingi ya taifa letu.

Chama dola hapa alikosea timing aisee alituingiza chaka
Lakini si tunaweza kufanya kitu?
Kama njia nyepesi itashindikana basi kwa njia ngumu itawezekana, kama itapatikana katiba iliyo bora itakuwa ni mojawapo ya njia nyepesi ya kubadilisha Hali iliyopo, tukawa na tume huru ya uchaguzi itasaidia chaguzi zetu ziwe na mantiki pamoja na uhalisia na maamuzi ya wananchi yataheshimiwa naamini watu wanataka mabadiliko lakini chaguzi zetu zimekaa kitapeli , mabadiliko ni muhimu ikishindikana ndo watu hufikia maamuzi magumh au njia ngumu hapo sasa ndiyo machafuko na uvujaji damu hutokea kama ilivyokuwa oktoba 29 ijapokuwa haikufanikiwa ila ni mwanzo wa mengi yanayoweza kutokea hapo baadae
 
Ahaa basi sawa ngoja tuone
 
Hongera mkuu kwa maada murua kabisa.

Kwa mawazo yangu na ingekua amri yangu bhasi ningetafuta baba wa Taifa mpya. Simvunjii heshima Nyerere lakini huo ndio ukweli na utabaki kuwa ukweli daima. Nasema hivyo kwasababu zifuatazo-

Mosi

- Nyerere alitengenezwa na hao wenye maslahi na hii nchi ili tupate uhuru wa bendera. Nyakati za ukoloni zilikua zimeshakwisha kwasababu watu walikua wanazidi kufunguka kiakili na kutafuta mbinu mbadala za kupambana na ukoloni, hivyo wakoloni walikuja na mbinu mbadala ambayo ndio ukoloni mamboleo.
Nyerere aliiuza Tanganyika kwa Malkia, rejea historia ya safari yake Uingereza. Pia katika mapinduzi 9 ambayo yalijaribu kumtoa Nyerere madarakani, mapinduzi yote hayo yalizimwa kwa usaidizi wa Uingereza.
Pia Uingereza ndio mmiliki wa kisiwa Cha Zanzibar, rejea historia ya vita fupi kabisa duniani ilikua ni kati ya Uingereza na Zanzibar. Je! ulishawahi kujiuliza kwanini Zanzibar alipigana na Uingereza? Je! baada ya hayo mapigano ni Nini kilitokea/kiliendelea?
Baada ya vita fupi kabisa duniani, Zanzibar ilibakia kuwa koloni la Uingereza pia.

Muungano wa Tanganyika na Zanzibar ni kusudio la Uingereza kuunganisha makoloni yake ili uwepo wepesi wa kufanya ukoloni mamboleo. Hivyo Nyerere anapopewa credit ya muungano nafikiri tunashindwa kuelewa alifanya hivyo kwa maslahi ya nani???
Leo tunauona muungano wetu ulivyo wa hovyo, tena afadhali huyo mkoloni yeye muungano wake na Ireland, Scotland na Wales Kuna uhuru kidogo.

Nyerere ndiye aliruhusu Uingereza iwe inaandika/kuipitisha mitaala ya elimu yetu. Sio ajabu elimu yetu ni mboooovu na haizalishi wasomi wenye tija kwa Taifa letu.

2. Nyerere aliua mifumo yetu ya asili(Uchief) ya uongozi akaleta mfumo wa kitaifa. Nyerere aliingia mikataba ya kuua mifumo ya kichifu na kuleta mfumo wa serikali ili kujipa yeye madaraka makubwa. Madhara yake tumeyaona tulipopata Marais vichaa wanaua mpaka wananchi wao.

Mimi binafsi sikuona umuhimu wowote wa kuleta mfumo wa serikali kuu, Bali tungebaki na mifumo ya asili lakini yangekua yanatambulika kama majimbo.

Leo Kuna takataka zinaitwa wabunge zinakula Kodi zetu Kwa kigezo Cha uwakilishi wa wananchi na kuisimamia serikali. Kwakweli kazi ya hao wabunge hata sizioni naona ni watu waliopo kwaajili ya maslahi yao.

3. Nyerere alileta mfumo wa kijamaa na aliposhindwa kuusimamia alitumia kigezo Cha kung'atuka lakini huku nyuma aliacha mashimo makubwa sana yailyoharibu uchumi wa nchi yetu kabisa.
Hata hivyo kabla yakung'atuka ni vyema angetangaza kuufuta rasmi mfumo wa kijamaa. Lakini aliishia kumtwika mzigo mzito Mhe.Mwinyi huku akimshauri Mwinyi akakope world bank na IMF wakati yeye aliwapinga.

4. Nyerere alituachia katiba mbovu sana, Katiba yetu ilitungwa mwaka77 na CCM ilianzishwa mwaka 77 baada ya TANU kuungana na A.S.P, Katiba hii ilitungwa ili kukipa madaraka chama Cha CCM na ilitungwa na hao niliowasema hapo juu kwamba Nyerere alikua kibaraka wao.
Nyerere alijua anachokifanya na ndio maana aliishia kuongea tuu kwamba tunakatiba mbovu ila hajawahi kutaka mabadiliko yake.

5. Nyerere alifanya madudu mengi lakini pia alikua na mazuri yake.

Kwa heshima na tahadhima napenda kumpongeza Nyerere kwa kulielimisha hili Taifa. Nyerere aliipokea hii nchi ikiwa na wasomi wasiozidi 100. Baada ya kuchukua madaraka alianzisha elimu ya watu wazima MEMKWA.
Alijitahidi sana katika hili, alifanya bidiii sana mpaka watu wakajua kusoma, kuandika na kuhesabu. Yes! Yes! Yes! Elimu Yao waliita K,K,K,K Yaani Kujua Kusoma,Kuandika na Kuhesabu.
Babu yangu alijua kusoma na kuandika hivyo walimchagua pia awe mwalimu kwa jamii yake.

Mwisho niseme hii nchi itapata ukombozi siku ukweli utakapowekwa wazi.

Uingereza inatikiswa na CCM inatikisika😂😂😂, pale Uingereza kiti Cha waziri mkuu hakikaliki🤣🤣🤣, Brexit imesimama, Ireland, Scotland na Wales wanasubiri kula za maoni.

Ukisoma historia ya Nigeria na yule jamaa yao wa kuitwa BABANGIDA ndio yaliyopo Tz na CCM.

Nb: Maelezo ya ziada ni ndio njia tunaweza kupita ili kumpata baba wa Taifa mpya nje ya hapo tuendelee kuimba Iyena Iyena.

Ni mimi Zirlovimovic Vladimilovic Zirkov a man from the past and the future.
 
Hongera mkuu kwa maada murua kabisa.
Asante sana mkuu
Aiseeeeeee hapa nimeishia kusoma na kutosheka na post hii sijapata swali la kuuliza na sijapata cha kuongeza
Kama nikipata nitarejea asante sana kwa ufafanuzi huu
Nchi ilikua na wasomi wasiozidi 100
Upande huu aliupiga mwingi pongezi kwake
Mwisho niseme hii nchi itapata ukombozi siku ukweli utakapowekwa wazi.
Nani wa kuweka ukweli wazi🤔
au tayari ukweli upo wazi ila hatuoni?
Uingereza inatikiswa na CCM inatikisika😂😂😂, pale Uingereza kiti Cha waziri mkuu hakikaliki🤣🤣🤣, Brexit imesimama, Ireland, Scotland na Wales wanasubiri kula za maoni.
Ndio kusema koloni letu bado tunatamba nalo sio?
Ukisoma historia ya Nigeria na yule jamaa yao wa kuitwa BABANGIDA ndio yaliyopo Tz na CCM.
Hii nitapitia Shukran
Nb: Maelezo ya ziada ni ndio njia tunaweza kupita ili kumpata baba wa Taifa mpya nje ya hapo tuendelee kuimba Iyena Iyena.
Maelekezo ya ziada😊
Ni mimi Zirlovimovic Vladimilovic Zirkov a man from the past and the future.
Karibu tena Mkuu🙏🙏
 
Aiseee😢😢
Kwakweli kwa ushawishi alikua nao angefanya kitu kwa sababu yeye mwenyewe aliona kabisa katiba ina mapungufu mengi
Naomba mniruhusu niseme Nyererea amechangia mauaji ya oktoba 29.
Ki vipi mkuu?
 
Asante sana mkuu
🙏🙏🙏
Aiseeeeeee hapa nimeishia kusoma na kutosheka na post hii sijapata swali la kuuliza na sijapata cha kuongeza
Kama nikipata nitarejea asante sana kwa ufafanuzi huu
Aminia sana mkuu🔥🔥🙏
Nchi ilikua na wasomi wasiozidi 100
Upande huu aliupiga mwingi pongezi kwake
Hapa alicheza zaidi ya Pele, apewe maua yake tuu.
Nani wa kuweka ukweli wazi🤔
au tayari ukweli upo wazi ila hatuoni?
Baadhi ya ukweli upo wazi, mengine yamefichwa sana.
Ni kazi ya watunza Siri Sasa kuziweka wazi maana mwisho wa siku Kila jambo litakuja kuwa wazi tuu.
Ndio kusema koloni letu bado tunatamba nalo sio?
Mkuu, nchi zote Africa bado ni makoloni ya nchi za ulaya, Marekani ni kiranja tuu. Hamiliki koloni lolote ila anakula kwa mgongo wa nchi za ulaya.

Ukiona nchi ya Dunia ya tatu imetulia bhasi anayewamiliki ameshaweka sawa maslahi yake na wananchi wa hiyo nchi.

Inshort jamaa bado wamejituliza na koloni lao, japokuwa wanapitia mengi sana. Angalia siku ya uapisho gari zilizotumika kumbeba yule naniliu. Zilikua ni LRR.
Hii nitapitia Shukran
Ukimsoma Rudi bongo muangalie yule anaishi jirani na msata. Yule ndio BABANGIDA wa TZ

Maelekezo ya ziada😊

Karibu tena Mkuu🙏🙏
Asante mkuu, majukumu tuu ndio yanatufunga but always I will be here.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…