Mwambieni CAG, sisi tumeridhika kwa kuwa tumezoea kuibiwa

Heheh, kuna Uzi mwingine upo kama huu, mmeamua kususa wazee wa Chatu joka kuu. Mkisusa sisi twala. Mlizoea vya kunyonga sasa kuwinda hamuwezi πŸ˜ƒ shenzi zenu. Mlikuwa malaika sisi tukawa mashetani, sasa nanyi ni zamu yenu tena mtulie kabisaaaaaa maana nasi tulikaa kimyaaa mkafanya maushenzi yenu tulikuwa tunawaangalia tu. Sasa mtulie otherwise mrudi mkavue samaki, sangara bado wapo sio lazima mkae mjini.
 
TUMIA AKILI YA KAWAIDA TU

Hivi kwanini CAG hajaigusa Ofisi ya makamu wa Rais , kipindi hicho Mama alikuwa huko, tuseme yenyewe haikuwa na matumizi?.......

Fikria Tena kwanini hawajaigusa ofisi ya WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO, kipindi hicho alikuwa Kaka yetu ambae saizi Ni Makamu, tusema Ofisi yake haikuwa na matumizi ?.......

TUTAVURUGWA VURUGWA HADI LINI?
 
Warundi mnahakikisha mnaanzisha thread Hazina kichwa Wala mguu. Bahati mbaya kwa sasa mnapoteza muda, why hamtaki kuamini ameshakufa na ameshazikwa? Na kwa nini hamtaki kuamini tuna Rais mpya?

Nyie ndio mnaoigawa CCM yenu wenyewe. Lakini ndio vizuri kafufueni chama cha Cheyo kile cha wasukuma muanze kampeni so mnasema mpo wengi sana nyie?
 
Daah ,,,ndugu zangu CCM sa hivi kazi mnayo aiseee... Threads zenu HAZISOMWI KABISA.
Problem wamejichanganya wenyewe wamegeuka wapinzani wa CCM kwa hiyo hata wapinzani halisi wa CCM wamebaki kwenye winning side ya kuendana na mama and Samia ili kumpima taratibu wakati wao wanaendelea kuvurugana.

Sukumagang nawashauri wakifufue chama cha John Cheyo kitawafaa wamuweke Andrew Chenge awe Mwenyekiti wao waanze mapambano, wao nasikia ni kabila kubwa sana πŸ˜ƒ
 
TUMIA AKILI YA KAWAIDA TU

Hivi kwanini CAG hajaigusa Ofisi ya makamu wa Rais , kipindi hicho Mama alikuwa huko, tuseme yenyewe haikuwa na matumizi?...
Wewe ndo mjinga unayetakiwa kutumia hata akili kidogo uliyonayo ya Darasa la 7 kujua kwa nini CAG hakupitia kabisa Taasisi unazotaja. CAG Kichere akiteuliwa na Magufuli baada ya kumtumbua Professor kwa kufanya kazi yake kwa weledi na haki na kazi ya Ripoti ya Kichere alifanywa kabla Mwendazake hajaenda, Ripoti ikaandikwa, ikachapwa na kubind Marehemu akiwa bado typo na alikuwa akabidhiwe yeye sote tunajua nini kingetokea kwa CAG.

Ofisi ya Makamu ni Ofisi ya Rais na iko Ikulu na Wizara ya Fedha Mpwa wa Rais alikuwa anaongoza Wizara kwa hiyo kama Covid-19 ingechelewa kidogo tu kufanya kazi yake, CAG Kichere angekuwa tayari ameungana na Professor.

Kama Kichere angejua kuwa mashine za kujifukiza hazisaidii kumlinda hata mtaalamu wa nyungu, asingehariri Ripoti na angemwaga madudu yote aliyoyakuta huko alikokagua.
 
Umekata tamaa πŸ˜…πŸ˜…πŸ˜…
 
Kwa sasa wanabutuana wenyewe kwa wenyewe laana inawatafuna.
 
Alikuwa fisadi mkubwa sana huyu jamaa sasa nchi itakuwa shwari.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…