Binafsi nimeshangazwa na maelezo yake kuhusu iko kipande kukielezea kama layman applying literal meaning. Badala ya kutoa technical explanation za sheria kinatokea wapi kimsingi.
Ni hivi background ya hiko kipengele kuna aina mbili ya kutatua migogoro ya kibiashara.
1. Litigation
2. Alternative Dispute Resolution (ADR).
Litigation ni kupitia mahakama, mara nyingi za host nation. Process zake huwa ndefu na ushahidi mwingi unahitajika. Wafanyabiashara hasa international investors don’t like that jumlisha na possibilities maamuzi yake yanaweza kuwa influenced na viongozi wa nchi husika.
ADR ni njia nyingine ya kutatua mgogoro bila ya kutumia mahakama ila kwa kutumia experts wa industry husika. Zipo processes kadhaa ila main ni 5.
(i) Early Neutral Evaluation (ENE).
Hii inahusisha parties kuchagua mtu wanaedhani ni sahihi kukitokea sintofahamu kupelekewa mgogoro kama anaweza utatua. Ndio msingi wa article 3(2) kuundwa kwa ‘consultative committees’ teams za majadiliano kuongea mambo ya uwekezaji na mengine. Na wamesema wizara ya ujenzi kupitia katibu mkuu atapewa kipaumbele kwanza kutatua mgogoro wa DPW na TPA. Ikishindikana baada ya siku 90 bila ya kuafiki maamuzi yaliyo tolewa hapo mgogoro unaweza kwenda arbitration.
Kabla ya arbritration kuna hatua zingine zinaweza fatwa ila sio lazima kufuata huo mlolongo.
(ii) Adjudication hii ni kama arbitration anaitwa neutral expert kusikiliza mgogoro na kutoa maamuzi, ila sio legal binding.
(iii) Mediation more detailed compared to adjudication ila na yenyewe maamuzi yake sio legal binding.
(iv) Arbitration (final expert determination), watanzania wengi wanadhani hizi ni mahakama. Hapana hii aina tofauti na hatua yeyote hapo, huyo arbitrator pia anachaguliwa na pande mbili na huwa ni expert on the industry. Tofauti yake hatua za awali kwenye ADR sio legal binding, whereas maamuzi ya arbitration ni legal binding.
Ndio maana kwenye mikataba ya kimataifa uwezi kukosa hiko kipengele cha dispute resolution.
Sasa mwanasheria mkuu analeta porojo sijui za diplomasia ya nchi and other nonsense, wakati diplomatic process zinazo ongelewa ni hizo hatua za awali za ADR.
Unajiuliza sana huko kwenye LNG sijui wamesaini kitu gani kama hawa ndio wanasheria wa serikali, maana huko kuna hesabu za advanced management accounting na sheria juu; utatia akili. Ndio maana mtu kama January anavyoona rahisi hayo mambo unajichekea tu pembeni.