GE2025 Mwanasiasa anayetaka kwenda Ikulu kwa kudanganya watu hatoshi

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025
Tunapowatajia watu tunaibiwa ni vyema tukaweka wazi hao wawekezaji wanalipa nini na wanapata ni nini.

Cost ya kuzalisha hayo makaa/tone ni kiasi gani, gharama za kuuza hayo makaa Kwa ton ni kiasi gani...ndio maana haya mambo Kuna wakati yanabackfire.

ndani ya mitaa ya Khartoum Sudan.
Jibwa la mafisadi katika ubora wako !
 
Mzoga ulio anza kuvunda hata siku moja hauwezi kupata uhai tena.

Haya unayo eleza hapa usifikiri yana umuhimu wowote kwa waTanzania wanaojuwa hila zote zinazo tumika kubaki madarakani kwa nguvu, bila ya ridhaa ya waTanzania.

WaTanzania wanajuwa maovu yote yanayofanywa dhidi yao; na kuwapokonya HAKI yao ya kuwachagua viongozi wanao wataka wao lipo wazi kabisa; hata mkiigiza vipi!

Jibwa la mafisadi katika ubora wako !
Wewe ni mchochezi kwa madereva wa bodaboda ambao wanakimbizana na kesho zao. Huna takwimu kuhusu makaa ya mawe na uchimbaji wake. Kama yangekuwa na thamani kubwaaa hivyo wakoloni wangeyachima, Nyerere angeyachimba, Mzee Mwinyi asingeyaacha, Mkapa, JK na JPM wangeyachimba wapate hela nyingi. Watoto hawezi kukaa chini madarasani wakati chini ya ardhi yao Kuna utajiri mkubwa sana.

Makaa ya mawe ni madini ambayo yatapoteza thamani muda mfupi ujao kutokana na dunia kupambana na climate change. Makaa yanatoa carbon dioxide nyingi sana yanapochomwa. Hewa hii ndiyo inayochangia kwa kiasi kikubwa kwa upandaji wa joto duniani (global warming). Global warming ndiyo inayosababisha maji ya bahari kuimega nchi kavu, visiwa vidogo baharini kumezwa na maji, maji kusogelea malazi ya watu, joto Kali kwa mimea, wanyama, samaki, vimbunga, mafuriko na ukame mkubwa. Kwahiyo makaa ya mawe ni adui mkubwa wa mazingira, yanapogwa vita. Tuyachimbe Sasa wakati uvumilivu kwa makaa ya mawe haujafika mwisho kidunia.

Nina uhakika akina Prof. Kabudi wamefanya kazi yao sawasawa wakati wa kutoa uwekezaji kwenye makaa ya mawe, tunazozisikia ni porojo za kichochezi tu.
 
Alikosa mchimbaji tu, huwezi kwenda kukopa wakati una mali iko chini. Mbona almasi, dhahabu na vito alikuwa anachimba. Haya madini ya chuma na makaa yalilalamikiwa miaka mingi awamu zote mbona hayachimbwi. Kama kuna mzawa mbona hakujitokeza. Lakini ni kweli hatupati kitu hata kidogo? hata ajira hatupati?. Lissu alitakiwa kwenda kule na takwimu juu ya yanachimbwa kiasi gani kwa makubaliano gani na yanauzwa wapi kwa bei gani na sisi tunapata ngapi badala ya makaa makaa makaa makaa hotuba nzima, mara anahamia kwa kambona, mara watu wamedumaa. Ni nchi gani duniani inagawia watu wake chakula ili wasidumae? kama siasa ndiyo hivi basi sisi bado kabisa.
Hizo takwimu za kwamba tunapata kiasi gani, zinatakiwa kutolewa na mamlaka husika, na sio kufanya siri hadi Lissu atafute kwa tochi, in fact wananchi wote wanatakiwa wajue, ili kuwepo na uwajibikaji kisha maendeleo yanayotakiwa.
 
Kama hana takwimu hapaswi kusema kitu. Takwimu ndio kitu cha msingi.
 
Wewe ni mchochezi kwa madereva wa bodaboda ambao wanakimbizana na kesho zao. Huna takwimu kuhusu makaa ya mawe na uchimbaji wake. Kama yangekuwa na thamani kubwaaa hivyo wakoloni wangeyachima, Nyerere angeyachimba, Mzee Mwinyi asingeyaacha, Mkapa, JK na JPM wangeyachimba wapate hela nyingi. Watoto hawezi kukaa chini madarasani wakati chini ya ardhi yao Kuna utajiri mkubwa sana.

Makaa ya mawe ni madini ambayo yatapoteza thamani muda mfupi ujao kutokana na dunia kupambana na climate change. Makaa yanatoa carbon dioxide nyingi sana yanapochomwa. Hewa hii ndiyo inayochangia kwa kiasi kikubwa kwa upandaji wa joto duniani (global warming). Global warming ndiyo inayosababisha maji ya bahari kuimega nchi kavu, visiwa vidogo baharini kumezwa na maji, maji kusogelea malazi ya watu, joto Kali kwa mimea, wanyama, samaki, vimbunga, mafuriko na ukame mkubwa. Kwahiyo makaa ya mawe ni adui mkubwa wa mazingira, yanapogwa vita. Tuyachimbe Sasa wakati uvumilivu kwa makaa ya mawe haujafika mwisho kidunia.

Nina uhakika akina Prof. Kabudi wamefanya kazi yao sawasawa wakati wa kutoa uwekezaji kwenye makaa ya mawe, tunazozisikia ni porojo za kichochezi tu.
Najuwa MZOGA hauwezi kuwa na aiibu kutokana na hali yake halisi.

Wewe umenunuliwa kama bidhaa. Hata hujishangai MZOGA kuwa bidhaa inayonunuliwa na hao wanao kutumia?

Unajipa ujuaji wa mambo huku hujui chochote. Wewe hujui hao wanaokufuga, wanao yamiliki hayo makaa ya mawe wanazo akili kukushinda wewe unayekuja humu kila siku na kuwahangaikia?

Unataka waTanzania wamwamini nani wewe MZOGA; au hao wanaohangaikia hayo makaa ya mawe unayo sema wewe kuwa hayana thamani.
 
Swala sio kuchimba swala tunanufaika vipi kama wazawa, kwa maoni yako Nyerere aliyeyaacha alikuwa zuzu?
Ndio, alikuwa zuzu, kitendo cha kuacha kuchimba inaonyesha kabisa alikuwa kilaza..
Alitarajia nini huko mbeleni ambako ndio leo mbwa kala mbwa kama Trump
Alitakiwa kuchimba miaka ile wakati dunia ilikuwa na utu, angeweza kuweka misingi ya jinsi gani faida yake inasaidia watanzania, lakini kwa kuwa ni kilaza alikuwa hakuliona hilo.
 
Kama hana takwimu hapaswi kusema kitu. Takwimu ndio kitu cha msingi.
Ni wazi unasindikiza tu mada mbovu iendele kuchangiwa. Bila shaka hii ni kwa sababu makombo mnayotupiwa yanalazimisha muonyeshe uchafu mliojaza humu jukwaani.
 
Najuwa MZOGA hauwezi kuwa na aiibu kutokana na hali yake halisi.

Wewe umenunuliwa kama bidhaa. Hata hujishangai MZOGA kuwa bidhaa inayonunuliwa na hao wanao kutumia?

Unajipa ujuaji wa mambo huku hujui chochote. Wewe hujui hao wanaokufuga, wanao yamiliki hayo makaa ya mawe wanazo akili kukushinda wewe unayekuja humu kila siku na kuwahangaikia?

Unataka waTanzania wamwamini nani wewe MZOGA; au hao wanaohangaikia hayo makaa ya mawe unayo sema wewe kuwa hayana thamani.
Mimi Sina price tag, na hao CCM na watawala wala hatujuani. Ila uzalendo na kusema ukweli hakuhitaji kununuliwa kwanza. Mm ni miongoni mwa watu ambao mabeberu wlitaka kunitumia dhidi ya nchi yangu eti kwakuwa nina scholarship yao. Mimi sitaki hela nyingi ambazo zitanishinda kuzila na kuzimaliza kabla sijafa.

Shida yangu ni kushindwa kunyamaza ninapoona mtu anatumia uwelewa mdogo wa raia wenzake kwa manufaa yake.

CCM hii haiko safi tangu wakati wa Nyerere, ukatili ni mwingi sana kwa kutumia jicho la nchi za Magharibi. Lakini ukatili huu ni ukatili wenye nia njema kwa Taifa. CCM inaiba kura tunajua lakini ni wizi wenye nia njema ndani yake. Upinzani wetu bado kabisa, bado wanaokoteza watu waliosukumwa CCM kama jiwe kuu la pembeni Kila uchaguzi unapofika.
 
Hotuba nzima ni makaa, makaa, makaa, makaa kama vile watanzania walikatazwa kuchimba makaa ya mawe.

Makaa ya mawe yalikuwepo nchini kwa miaka 5,000,000 iliyopita. Eti watu wasiende kupiga kura kwasababu ya makaa ya mawe. Eti serikali iende ikalime mbambabei ili watoto wasidumae.

Watanzani wanapenda kuchimba dhahabu sio makaa ya mawe. Lissu alitakiwa kulalamika kuwa niliomba kuchimba makaa ya mawe lakini nilinyimwa akapewa mgeni.

Eti anasema ya kambona, jamani kufilisika gani huku.

View: https://youtu.be/TdCkjaIH2rU?si=blde7zqRnMC9R3No

Unajua thamani ya Makaa ya mawe wewe? Ona li chawa hili? Anataja Makaa maana ni raslimali ya Taifa inayoibwa na wahuni
 
Mimi Sina price tag, na hao CCM na watawala wala hatujuani. Ila uzalendo na kusema ukweli hakuhitaji kununuliwa kwanza. Mm ni miongoni mwa watu ambao mabeberu wlitaka kunitumia dhidi ya nchi yangu eti kwakuwa nina scholarship yao. Mimi sitaki hela nyingi ambazo zitanishinda kuzila na kuzimaliza kabla sijafa.

Shida yangu ni kushindwa kunyamaza ninapoona mtu anatumia uwelewa mdogo wa raia wenzake kwa manufaa yake.

CCM hii haiko safi tangu wakati wa Nyerere, ukatili ni mwingi sana kwa kutumia jicho la nchi za Magharibi. Lakini ukatili huu ni ukatili wenye nia njema kwa Taifa. CCM inaiba kura tunajua lakini ni wizi wenye nia njema ndani yake. Upinzani wetu bado kabisa, bado wanaokoteza watu waliosukumwa CCM kama jiwe kuu la pembeni Kila uchaguzi unapofika.
Acha ujinga wewe. Wewe ni chawa tu huna lolote. Eti wapinzani Bado sana. Rubbish! Huna hata aibu kuandika madudu kama haya
 
STOP RIGHT THERE Mr.!

Sasa unataka tuanze tena kurudi nyuma tukatazame "uzalendo" wako kwa maandishi yako ambayo yametapakaa kila mahali humu?
Hivi hata chembe ya aibu huna?

Wewe unadhani inanifurahisha mimi kumwita mTanzania mwenzangu kuwa ' MZOGA" wakati akionyesha wazi kwa matamko yake/maandishi yake kuwa yeye ni mtu anayeipenda nchi yake kwa dhat?

Haya unayojaza humu kila siku, kuwadharau waTanzania, huu ndio unaouita UZALENDO, kweli?

Ni hivi: kwa kila aina ya kigezo, wewe ni miongoni mwa maadui wakubwa sana wa nchi hii kwa hivi sasa, kutokana na mnayo yapigania yaendelee kuwepo katika utawala huu ulio laaniwa.
Huenda kuna maana nyingine ya uzalendo unayo ilenga wewe; lakini siyo maana ya kuipenda nchi yako na watu wake wote waliomo ndani ya nchi hiyo bila kujali tofauti zao za kidini, kikabila na mengineyo.

Sasa unanifanya nikusikitikie sana kwa jinsi ulivyo vurugikiwa kiakili.
 
Acha ujinga wewe. Wewe ni chawa tu huna lolote. Eti wapinzani Bado sana. Rubbish! Huna hata aibu kuandika madudu kama haya
Huyu mtu sasa namsikitikia, kwa sababu naona kachanganyikiwa, hajui kabisa analo liandika.
Mabandiko yake yote humu ni uchonganishi tu wa mifarakanyo, sasa hapa anakuja na kujibandika 'UZALENDO'!

Na eti anajieleza kuwa kasoma na anayo elimu ya kutosha kujua maswala muhimu ya maisha!
 
Mimi Sina price tag, na hao CCM na watawala wala hatujuani. Ila uzalendo na kusema ukweli hakuhitaji kununuliwa kwanza. Mm ni miongoni mwa watu ambao mabeberu wlitaka kunitumia dhidi ya nchi yangu eti kwakuwa nina scholarship yao. Mimi sitaki hela nyingi ambazo zitanishinda kuzila na kuzimaliza kabla sijafa.

Shida yangu ni kushindwa kunyamaza ninapoona mtu anatumia uwelewa mdogo wa raia wenzake kwa manufaa yake.

CCM hii haiko safi tangu wakati wa Nyerere, ukatili ni mwingi sana kwa kutumia jicho la nchi za Magharibi. Lakini ukatili huu ni ukatili wenye nia njema kwa Taifa. CCM inaiba kura tunajua lakini ni wizi wenye nia njema ndani yake. Upinzani wetu bado kabisa, bado wanaokoteza watu waliosukumwa CCM kama jiwe kuu la pembeni Kila uchaguzi unapofika.
Mkuu 'kavulata'; andiko lako hili limenifadhaisha kwa kiasi kikubwa sana hata nashindwa namna nzuri ya kuandika na kujibu yote uliyo eleza hapa.

Huwa sihitaji kusoma maandishi mara mbili ili nielewe kilichomo; ila imenilazimu nirudie tena kusoma ulicho andika hapa, nikiwa na kumbukumbu ya maandishi yako mengi sana yaliyo jazana kwenye jukwaa hili la JF. Yote ni wazi yanapingana na ulicho andika hapa leo!

Ila nikuombe tu, kama kweli unaguswa na hali mbovu inayolikabili taifa letu kwa sasa hivi; tuachane na ushabiki wa kimakundi ya aina yoyote inayo lielekeza taifa hili kwenye hali mbovu kabisa. Huko juu katika michango yako umegusia hali inayo waumiza wapalestina; na umeieleza vizuri vya kutosha kueleweka. Sasa ninakuomba, tambua kwamba Tanzania haiwezi kuwa tofauti sana na hao wapalestina kama hatutakuwa waangalifu katika kulinda taifa letu kwa umoja wetu.

Labda nimalize tu kwa kusema hivi: hapa Tanzania hatuna "Mungu" wa wakristo; au "Mungu" wa waislamu; au "Mungu" wa waTanganyika; "Mungu" wa wa Zanzibar, n.k., n.k.. Naamini kuwa tunaye "Mungu" wa waTanzania wote, hata wale wasio kuwa na imani yoyote.

Siamini kuwa "Mungu" huyo anatuongoza tuvurugane wenyewe kwa wenyewe ndani ya nchi hii.

Tukivurugana, kama hii CCM na viongozi tulio nao sasa wanavyo tupeleka; siyo kwa matakwa ya "Mungu" huyu; bali ni kwa matakwa ya hawa viongozi tulio nao.

Tusikubali kutumiwa kulivuruga taifa letu zuri sana.

Hao unaowaita "Wapinzani"; na wao ni waTanzania kama sisi wengine wote. Kwa nini tuwabague kwa kuwa wapinzani?
 
Kama hana takwimu hapaswi kusema kitu. Takwimu ndio kitu cha msingi.
Takwimu atazipataje na huku mnafanya siri, mikataba mibovu mnaingia kisiri siri hamtaki kuweka wazi hadi mtu mmoja / afisa ajitoe mhanga avujishe ndio tujue kama bandarini kule, sema cha msingi pamoja na kukaza kwenu shingo namba ndio tunaisoma wote hizo familia tatu kikwete, samia na rostam wenyewe mambo yakiharibika sana wanakwea mwewe makazi washajitayarishia uarabuni, kazi kwenu kajamba nani(wanyonge).
 
Acha ujinga wewe. Wewe ni chawa tu huna lolote. Eti wapinzani Bado sana. Rubbish! Huna hata aibu kuandika madudu kama haya

Mkuu 'kavulata'; andiko lako hili limenifadhaisha kwa kiasi kikubwa sana hata nashindwa namna nzuri ya kuandika na kujibu yote uliyo eleza hapa.

Huwa sihitaji kusoma maandishi mara mbili ili nielewe kilichomo; ila imenilazimu nirudie tena kusoma ulicho andika hapa, nikiwa na kumbukumbu ya maandishi yako mengi sana yaliyo jazana kwenye jukwaa hili la JF. Yote ni wazi yanapingana na ulicho andika hapa leo!

Ila nikuombe tu, kama kweli unaguswa na hali mbovu inayolikabili taifa letu kwa sasa hivi; tuachane na ushabiki wa kimakundi ya aina yoyote inayo lielekeza taifa hili kwenye hali mbovu kabisa. Huko juu katika michango yako umegusia hali inayo waumiza wapalestina; na umeieleza vizuri vya kutosha kueleweka. Sasa ninakuomba, tambua kwamba Tanzania haiwezi kuwa tofauti sana na hao wapalestina kama hatutakuwa waangalifu katika kulinda taifa letu kwa umoja wetu.

Labda nimalize tu kwa kusema hivi: hapa Tanzania hatuna "Mungu" wa wakristo; au "Mungu" wa waislamu; au "Mungu" wa waTanganyika; "Mungu" wa wa Zanzibar, n.k., n.k.. Naamini kuwa tunaye "Mungu" wa waTanzania wote, hata wale wasio kuwa na imani yoyote.

Siamini kuwa "Mungu" huyo anatuongoza tuvurugane wenyewe kwa wenyewe ndani ya nchi hii.

Tukivurugana, kama hii CCM na viongozi tulio nao sasa wanavyo tupeleka; siyo kwa matakwa ya "Mungu" huyu; bali ni kwa matakwa ya hawa viongozi tulio nao.

Tusikubali kutumiwa kulivuruga taifa letu zuri sana.

Hao unaowaita "Wapinzani"; na wao ni waTanzania kama sisi wengine wote. Kwa nini tuwabague kwa kuwa wapinzani?
Kwa mara ya kwanza umeongea kama mtu mwenye dini yake na mtanzania mwenye uchungu na taifa lake. Kuita watu mizoga sio kujibu hoja. Lengo letu sote ni kuona taifa ni Moja na Kila mtu anajivunia kuwa mtanzania.

Shida yetu kama taifa ilianzia pale Mwl Nyerere na wenzake waliposema Tanzania ni nchi ya kijamaa, na Kila mtu aliyempinga alikiona cha moto. Orodha ni ndefu ya walioadhilika kwa kupinga ujamaa na kujitegemea. CCM ni ileile Jana na leo, wanabadilisha viongozi tu. Bahati mbaya wanaCCM wote walikuwa waliimba hiyenahiyena hata pale tulipokuwa tunaibiwa, mfano Richmond, escrow, iptl, melemeta, kununua ndege bila kuwepo kwenye bajeti, nk, Akina Polepole walikaa kimya muda wote huo wakati taifa linapita kwenye vipindi vigumu chini ya CCM.

Ghafla Polepole anaibuka kutuambia kumbe ndani ya CCM Kuna makundi mawili ya CCM asili na CCM mtandao. Polepole anasema wanamtandao ndio walimuua Rais JPM, hii ikasababisha CCM asili wale njama za kukwamisha Rais Samia kushika nafasi ya Rais baada ya JPM (mwanaccm asilia kufa. Lakini Polepole anaficha ukweli kwanini hamtaki Samia kuwa Rais badala yake anajificha kwenye desturi na utamaduni wa chama, ana anataka watanzania wote wamuunge mkono kwenye jambo lake.

Kwaakili yangu mm nadhani hata huku kutekana kunaweza kuwa na mizizi kutoka huko kwa CCM asili na CCM mtandao na hata kelele za Polepole na Gwajima za watu kutekwa huenda Zina mizizi kutoka huko.
 
Kwa mara ya kwanza umeongea kama mtu mwenye dini yake na mtanzania mwenye uchungu na taifa lake. Kuita watu mizoga sio kujibu hoja. Lengo letu sote ni kuona taifa ni Moja na Kila mtu anajivunia kuwa mtanzania.
Unarudi kule kule tuliko anzia; wakati nikikusihi uone upotofu uliokuwa nao kabla ya kunilazimisha nikuweke kwenye kundi hilo la MIZOGA.
Sasa unataka kuniambia hujui chochote tuliwahi kujibishana kati yetu muda wote ule?
Kama unafikiri ninakuja humu kujifurahisha tu na watu wapuuzi, nakuomba tafadhali usinichukulie hivyo; I am deadly serious in discussing Tanzania's destiny. Sitanii na wala simna mzaha juu ya hili.

Rudi nyuma, tazama mada zako zote na michango mbalimbali uliyokuwa unaiweka humu kabla ya huo niliokujibu hapo kwa heshima; halafu uje hapA UNILALAMIKIE TENA KWA KUKUITA mzoga.

Sasa sijui hasa nia yenu ni ipi kwa kweli, maana mtindo huu wa hadaa siyo wewe pekee unaye utumia humu. Huyo Mwenzako Steven Joel Ntamu sana, na yeye tumezungushana hivi hivi. Mara anakuja kama mtu mwenye akili timamu kujadili jambo; akirudi siku mbili tatu kisha badilika tena kama hajui alichokwisha changia siku chache tu zilizo pita.
Sasa nikuulize, kuna shule maalum mnako fundishwa aina hii ya kujadili mambo?
 
Back
Top Bottom