Mwanaume asiye na Pesa hukosa mvuto ndani ya Jamii

Mwanaume asiye na Pesa hukosa mvuto ndani ya Jamii

Mwanaume asie na hela ni yupi na hiyo jamii unayoizungumzia ni ipi? Vijijini % kubwa wanalingana tu kiuchumi na gap ni dogo sana na bado wanaishi kwa kuheshimiana na kila kitu kinaenda. Tupe kiwango cha pesa ambacho kinatofautisha mwanaume asie na hela na ambae hana. Tanzania tuna mabilionea (in USD)wachache tu labda hata 10 hawafiki, kama unawareffer hao it means waliobaki wote hawana mvuto kwenye jamii? Mathalani Daktari tu wa binadamu anaweza kuonekana hana hela na kuna jamaa ameleta Uzi humu kua wana maslahi duni serikali iwaangalie, hapo unazungumzia mtu ambae basic salary yake ni 2.5M+, je huyu hana mvuto kwasababu kwenye jamii kwakua mapato yake hayafiki 20M per month? Huyu akiwa pale hospital ya Nzega DC atakua hana mvuto kwenye hiyo jamii ya watu wa Nzega? Tuje kwenye thamani na kusikilizwa kwenye jamii, mwanaume unaemzungumzia hapa anatakiwa kua na sh ngapi ili jamii imthamini na kumsikiliza na kumshirikisha kwenye maamuzi muhimu? Anyways hii maada sijaeielewa vizuri imekaaje, ila nachojua huwezi kubet na maisha ya mwanaume kwasababu kesho hujui atakua nani. Mwanaume anaweza maskini leo kesho akawa tajiri. Anaweza kua mtu wa kawaida leo kesho akaja kua mtu mkubwa tu and vice versa. Sasa mwanaume anadharauliwa vipi? Kuna jamii anaweza kua hana hiyo thamani lakini kwenye jamii yake akawa na heshima kubwa tu. So conclusively mwanaume ambae wewe unamwona hana pesa ya kiwango unachotaka ni mwanaume bora kabsa kwa mwanamke mwingine ndo maana nimeanza kwa kuuliza ni kiwango gani kinachomtofautisha mwanaume mwenye pesa na ambae hana, tuanze na wewe kwanza.
Asante kwa elimu nzuri na ufafanuzi mzuri.
 
Asante sana, hii ni habari njema kwangu..japo naitwa mzee wa hovyo!!
😅😅😅Utaweza mambo ya watu.
Si unajua huwezi pendwa na Kila mtu.
Tuishi nao.
 
Umenena lweli kabisa Mkuu, how come mwanamke anaandika uzi kama huu. Kamzarau mpaka baba yake. 😂

Nyuzi kama hizi wajukuu wa Bakhersa hawawezi kuandika huwa tunaandika sisi average life standards
Relax.
Hakuna mahali palipotaja wazazi.
 
Na wewe maoni yako ni yapi ?
Hata Baba yako ni Mwanaume kumbuka hilo.

Je ana hela au hana ? Mvuto , heshima na ushawishi kwenye jamii anao ?

Muwe mnaandika vitu vinavyoakisi uhalisia wa mambo sio motivation speech ambazo hubaki bila maana yoyote.

Mwenye pesa na asiye na pesa bado wanabaki kuwa ni wanaume.
Pesa ni muhimu lakini character ni muhimu zaidi kwenye hqya maisha.

Mzee Lowassa (rip) pamoja na mipesa yake yote alishindwa kupata afya timamu. Tuwe tunafikiria kwa kina na mapana
Umeenda mbali sana Bro.
Walioelewa wameelewa

Kumtaja Baba hata sio kitu Cha kushangaza wala kushtua kama akikosa pesa atakosa heshima vilevile tangu lini asie na pesa akaheshimiwa.

Kama kitu kilichoandikwa kimekukera unaweza kupita kimya kimya sawa.
 
Hakika mkuu!
Kuna watu wamezaliwa na hasira za ajabu ajabu 😅😅😅
Anaenda anakua nazo na kuzileta ndani ya Jamii.

Sehemu ya kutumia akili anatumia hasira 😅😅😅

Muda wa kuenjoy anatumia hasira.
 
Na wewe maoni yako ni yapi ?
Hata Baba yako ni Mwanaume kumbuka hilo.

Je ana hela au hana ? Mvuto , heshima na ushawishi kwenye jamii anao ?

Muwe mnaandika vitu vinavyoakisi uhalisia wa mambo sio motivation speech ambazo hubaki bila maana yoyote.

Mwenye pesa na asiye na pesa bado wanabaki kuwa ni wanaume.
Pesa ni muhimu lakini character ni muhimu zaidi kwenye hqya maisha.

Mzee Lowassa (rip) pamoja na mipesa yake yote alishindwa kupata afya timamu. Tuwe tunafikiria kwa kina na mapana
Kazungumzia hali halisi kwenye jamii zetu, na si tu mwanaume hata mwanamke asie na pesa nae hali ni hivyo hivyo. Umemuelewa tofauti au ni kwa sababu kamtaja mwanaume ndio ambacho hujapendezwa nacho ila alichoandika ndio uhalisia wenyewe.
 
Ni kweli, hata mapenzi hapewi bila hela, kuoa nako ni shughuli pevu kama hana hela hakuna mwanamke na wazazi wake kukubali mtoto wao aolewe na asiye na hela
 
Kazungumzia hali halisi kwenye jamii zetu, na si tu mwanaume hata mwanamke asie na pesa nae hali ni hivyo hivyo. Umemuelewa tofauti au kwa ni sababu kamtaja mwanaume ndio ambacho hujapendezwa nacho ila alichoandika ndio uhalisia wenyewe
Sawa Kelsea.
 
Sawa Kelsea
Ni kweli, hata mapenzi hapewi bila hela, kuoa nako ni shughuli pevu kama hana hela hakuna mwanamke na wazazi wake kukubali mtoto wao aolewe na asiye na hela
Umeona Loth ee
 
Mie mtu akifa mapema, huwa inanitafakirisha na mie kujiona wa siku yoyote, inanipa moyo wa kuishi vizuri sana na watu maana kesho tunaweza amka sipo milele
Una uoga mwingi sana wewe 😅
 
  • Kicheko
Reactions: Oho
Kuna watu wamezaliwa na hasira za ajabu ajabu 😅😅😅
Anaenda anakua nazo na kuzileta ndani ya Jamii.

Sehemu ya kutumia akili anatumia hasira 😅😅😅

Muda wa kuenjoy anatumia hasira.
Yote haya ni kwa sababu ya changamoto nyingi za maisha, kama hivi unasema pesa inamfanya mtu aheshimike kwenye jamii, kuna sehemu ukienda wadogo wanaheshimiwa kuliko wakubwa kisa pesa zao tu.

Dunia inatuendesha sana binadamu, bila pesa tunaonekana hatuna thamani.
 
Una uoga mwingi sana wewe 😅
Ndio maisha ya binadamu yalivyo siogopi kufa, ila unaacha mazingira gani baada ya kufa. Mwezi wa tatu au wa pili, nilikuwa na chart na rafiki yangu tunapiga story hadi tumekubaliana baada ya mda tukutane, imepita dk 30 baada ya mawasiliano naona status jamaa katutoka, napikicha macho nahisi sikuwa naona vizuri ila wapi
. kweli nakuja piga simu mtu kafariki na wakati kama dk 30 nyuma tulikuwa tunapiga mastoty yetu..
 
Yote haya ni kwa sababu ya changamoto nyingi za maisha, kama hivi unasema pesa inamfanya mtu aheshimike kwenye jamii, kuna sehemu ukienda wadogo wanaheshimiwa kuliko wakubwa kisa pesa zao tu.

Dunia inatuendesha sana binadamu, bila pesa tunaonekana hatuna thamani.
Hata kijijini kwetu ni hivo.
Kuna Baba wakubwa hawana pesa wanawaheshimu wadogo zao.
Kuna ma uncle hawana pesa na wanatia huruma.
Na hata maamuzi hawana.

Watu wanajifanya hawayajui hayo 😅😅
Ili mradi wajionyeshe kuwa wao ni miamba wa maneno machafu 😅.

Halafu mtu anamtaja Baba.
Kwani Baba asipokuwa na Hela nani atamheshimu.
Tena watoto watashuhudia anavyodharauliwa na hata na wadogo zake wa kike.
 
Back
Top Bottom