Kwenye Ngoma ya Zali la Mentali
Jay anakutana na Viki pale Somora Avenue
Viki anamwambia:
Masikini Pole Sana mzigo mbona mzito kweli utafika nao salama ?
Jay anatabasamu kisha anamjibu : Ohhh nimeshazoea mama na namshukuru Mwenyezi Mungu kwani hii ni km karama,
Anakuwa mnyonge anang'ata kucha anantazama
Anaaza kulia anatoa lesso anainama
Namwambia, "bibie ni mara ya pili tunaonana
Na sidhani kama ni mbaya iwapo tukifahamiana"
"Naitwa Vicky nna miaka 22,
Ni mtoto wa kipekee kwenye familia ya kitajiri"
"Oh naitwa Jay ukiniita fukara haukosei
Na naishi kwa nguvu za macho siku zenyewe hazisogei"
Alishuka toka garini na kusema "Jay nakupenda"
Akaruka kwangu mdomoni na kuanza kupata denda
Nilichomoka kwake na kuanza kurudi nyuma
"Tafadhali mpenzi Jay jamani nionee huruma
Acha kubeba mizigo panda ndani kwenye mchuma
Twende Mbezi Beach kwangu upepo unapovuma"
"Sikiliza Vicky napenda tuwe marafiki
Lakini hadhi yako hutakiwi kuwa na mtu wa dhiki
Hata wazazi wako naaamini hawataafiki
Tajiri na tajiri, maskini sithaminiki
Tafuta kibopa mwenzio ili usishushe hadhi yako
Mimi sistahili hata kuwa kijakazi wako"
"Tafadhali Jay usitamke maneno hayo
Naomba unielewe haya machache niyasemayo
Hadi huu wakati mimi nimekupenda kwa dhati
Ukikubali niwe wako nitajiita mwenye bahati"
"Nimeelewa Vicky naomba niwahishe mzigo
Tajiri ni mkorofi anansubiri Migomigo
Na kila nikichelewa mwenzako napata kipigo
Nasaga na rumba jua na mvua kwa mpigo"
Tuliongea mengi akanipa
hela za matumizi
Sikuwahi hata kuziona nilikuwa kama chizi
Niliacha kubeba mizigo penzi letu likaota mizizi
Watu wa uswahili wakasema natumia kizizi
Zali la Mentali - Prof Jay ft J Nature & Muny